Hatupendi kujibu wala kubishana!
Ni bora tufundishane.
Tutajibu kutokana na kiwango cha hoja yako.
Mtu yeyote akizungumzia suala la Israeli "Huitwa Anti-Semites." Yaani chuki dhidi ya Wasemaiti.
Hili sio suala la Imani wala dini. Hili ni Suala la "Haki za Kinaadamu".
Na mpaka sasa kitu ambacho kinatishia Taifa la Israeli ni wananchi wake wenyewe ambao wameshaanza kujua ukweli na wanalipinga Taifa hilo kwa sera zao za UbaguZi. Sauti hizi zinazosema Ukweli ndizo sasa zinatakiwa.
Suala la Intelijensia. China na Urusi ndio wanajua sana ukweli na hatari ya Israel hapa Afrika. Historia itazungumza. Tunatumaini Maofisa wetu wako macho kwa hilo.
Waisraeli hawana Teknolojia yeyote, wao pia hununua au kuchukua Udau. Ni nchi inayegemea misaada kutoka Marekani.
Wakati tuliposimama tukiwapinga Makaburu na sera zao za Ubaguzi, hatukuangalia dini zao.
Harakati ni hizi hizi.
Umoja wa nchi za Afrika zimezumgumzia Ubaguzi huu. Umoja wa Mataifa. Wanaharakati wote duniani pamoja na Amnesty International pia wanalizungumzia suala hili.
Sidhani kama Watanzania wanajua ni nini kinachoendelea huko Palestina. Tunaomba muende mukaone na macho yenu. Yeyote yule anakwenda huko, na kuonda udhalimu wa hali ya juu, huwa wanabadilisha fikra zao juu ya Israel.
Israel imekuwa chanzo cha matatizo yote, kutokuwa na amani Mashariki ya Kati.
Mgomo baridi ndio njia pekee ya Amani itayoweza kuifanya Israel iheshimu sheria za Kimataifa na kutokomeza Ubaguzi na kuwapa waPalestina haki zao.
Kuhusiana na Obama, sasa ndio ndugu yetu ataanza kufanya kazi yake sawa sawa, na tunategemea atafuata nyayo za akina Mwl Nyerere, Mandela na Jimmy Carter kwenye suala la kutafuta haki za wanyonge huko Palestina.