Kuna mateso ya ndani ya ndoa hayavumiliki
Nimeona ndoa zinatesana kwasababu za kishirikina za kutoa makafara tena ya watu.
Dada kaolewa hakuwa anajua ya ndani alipojifungua tu mtt siku ya 7 kaenda Hosp kutolewa nyuzi, mama mkwe akachukua mtt wake machanga wa siku 7 akaenda naye kwake. Dada anarudi hakuti mtt na anamuambia mume mume anasema ni kawaida ya mila zetu. Akahoji mbona hukuniambia akaambiwa utayajua baadae.
Mama akanyanyuka kumfwata mtt huko kwa mkwe. Akakuta mtt analia balaa. Anamuuliza Dada wa kazi mbona Sasa humbebi anasema Bibi hamtaki
Toka siku hiyo mtt akapata ugonjwa akawa mlemavu wa Akali.
Dada akaanza ukisoma namba mara Bibi anakujaga home anaingia hadi bdrum kwake, anatandika kitanda alimradi fujo tuu huku mume yuko pamoja na mama. Kumbe maskini wanatafuta njama za kumtoa mtt kafara. Siku wifi yake akamwambia live.
Ikabidi huyu Dada aondoke na mwanae kwenda kujificha. Ndio baadae babu mtu akatafuta njia akawapata walioko mafichon wakamnyang'anya mama mtt. Mamma akaenda kanisan, babu akatukana kanisa vby sana. Huku Hali ya mtt unazidi kuwa mbaya.
Mama akatoka akaenda mahakaman, mahakaman akapewe divorce babu na Bibi wakaja wakaweka pingamizi eti wabaki na mtt kwan ni mlemavu wa akili so mama hataweza kumuhudumia. Kesi mpaka Sasa inaendelea.
Je katika Hali kama hii utasemaje?
Sent using
Jamii Forums mobile app