Kesho kunani
Member
- Sep 10, 2023
- 72
- 191
Kama ningefeli shule Ninayopitia Sasa bila Shaka nisingeyapitia.
Kama ningefeli shule bila Shaka ningeenda veta na Sasa ningekuwa na ujuzi Fulani.
Kama ningefeli shule bila Shaka jamii isingekuwa inaniangalia Kama inavyoniangalia Sasa,ningekuwa huru,nisingenyoshewa vidole ninapoendesha boda boda au ninavyopakia mchanga kwenye magari.
Kama ningefeli shule bila Shaka ningekuwa na amani, majuto niliyokuwa nayo ya kupoteza muda shule nisingekuwa nayo.
Kama ningefeli shule classmate wangu wasingejadili kila ninachofanya,maana saizi kila ninachofanya watu wanajadili , nikiuza viepe utasikia kunani kesho anauza chips siku hizi, nikiendesha boda utasikia kunani kesho kawa boda boda licha ya kufaulu kote kule.
Kama ningefeli shule bila Shaka nisingekuwa na ugomvi muda wote na mke wangu,maana naamini alinikubalia kwakuangalia ufaulu wangu,alijua nitakuwa mtu mkubwa na haijawa hivyo,kwasaaa ndani ya nyumba ni miguno na misonyoo isiyokuwa na mwisho.
Kama ningefeli shule bila Shaka ningekuwa na amani Sana.
Kunani kesho.
Kwasasa songea.