Chakaza
JF-Expert Member
- Mar 10, 2007
- 40,455
- 73,145
(Ameandika Malisa G. )
SSP Christopher Bageni atanyongwa hadi kufa. Ndivyo mahakama ya rufaa ilivyoamua. Maamuzi ya leo ni ya mwisho ktk mwenendo wa kesi yake. Hana pengine pa kukata rufaa, pa kukimbilia, wala pa kupinga. Mahakama imeamua anyongwe hadi afe. Jaji Stellah Mugasha amegonga nyundo. Itz over.
Hawezi kukata rufaa tena kwa sababu hukumu ya leo ni review ya hukumu iliyotolewa na mahakama hiyo September 16, 2016, ambapo alihukumiwa kunyongwa hadi kufa na jopo la majaji watatu wakiongozwa na Jaji Benard Luanda. So hakuna mahakama ya kujadili tena shauri lake, labda Rais ampe msamaha.
Kwa wasiokumbuka Bageni alikua Mkuu wa Upelelezi wilaya ya Kinondoni. Mwaka 2006 yeye na wenzie wakiongozwa na aliyekua Kaimu RPC Dar, Abdalah Zombe, walituhumiwa kupanga njama za kuwauwa wafanyabiashara watatu wa Morogoro.
Zombe anadaiwa ndiye aliyeongoza wenzie kwenye mpango huo, baada ya kujulishwa kuwa wana madini na fedha kiasi cha shilingi milioni 200.
Walikamata gari waliyokua wameikodi. Wakamuongoza dereva hadi msitu wa Mabwepande. Wakapora madini pamoja na fedha zote walizokua nazo. Kisha wakawafunga vitambaa vyeusi usoni na pingu mikononi. Kisha wakawapiga risasi za kisogoni na kuwauwa wote akiwemo dereva wa taxi waliyemkodisha.
Kesho yake Zombe akaita media na kusema wameua majambazi yaliyokua yanarushiana risasi na Polisi. Rais Kikwete akaunda tume ya Jaji Kipenka kuchunguza. Ikabainika hawakuwa majambazi. Kilichouma zaidi walikua ndugu wa familia moja. Mama mmoja alipoteza wanae watatu. Watoto wa familia 4 wakapoteza baba zao, na wake wanne wakawa wajane kwa tamaa za polisi.
Zombe alifanikiwa "kuchomoka" kwenye kesi hii baada ya kusota rumande kwa miaka kadhaa. Lakini Bageni alipatikana na hatia akahukumiwa kunyongwa. Akakata rufaa ikafeli, akaomba review ya kesi, na rulling imesomwa leo kuwa ANYONGWE HADI KUFA.
Waliomtuma hawapo nae Segerea, wala hawatanyongwa pamoja nae. Atanyongwa peke yake. Wanaohangaika nae saivi angalau kumfariji ni familia yake. Zombe hayupo, OCD wake hayupo hata IGP wa wakati huo hayupo. Ni yeye mwenyewe, na atanyongwa mwenyewe.
Hii iwe fundisho kwa wote wanaotumwa kufanya maovu leo e.g kuteka, kuua na kupoteza watu. Ipo siku utajikuta peke yako. Anayekutuma hatakuwepo. Utasimama wewe mwenyewe kutoa hesabu ya maovu yako. Kama si hapa duniani basi hata mbinguni, lakini ipo siku utalipa. Kama ambavyo wema ni mbegu, na ubaya pia ni mbegu. Humea, hukomaa, na ni lazima UVUNE.!