Natamani sana andiko hili la hukumu ya Afande Bageni lisomwe vituo vya Polisi na Makazi yao kwenye Paredi

Ingependa na aliyewatuma akaunganishwa katika hiyo Kesi.

Kumuachia Huru Huyo Mkuu wao inafikirisha namna haki inavyotendeka.
Yaani alieita Waandishi wa Habari anaachiwa ananyongwa mtu mwingine na kumbuka hiyo kwenye hiyo kesi yupo askari alifia wakiwa jela kifo cha utata sana na huyo ndio alikua na ushahidi wa kesi yote..
 
Inashangaza Sana Mwaka 2009 ilipotolewa hukumu nilipata Goosebumps kuona Abdallah zombie Anaachiwa huru
 
Hatanyongwa huyo atabaki jela mpaka kifo kinamchukua mara nyingi huwa wanakufa kwa msongo wa mawazo tu...
Hao waliokumiwa kunyongwa huwa wanapewa special treatment wanakula vizuri , hawafokewi , na hulala sehemu nzuri.

Na maaskari wanaowalinda hawaruhusiwi kuvaa viatu wala mkanda na huwa hayo malindo yanombaniwa ukipangwa huko unakuwa upo stress free
 
Inashangaza Sana Mwaka 2009 ilipotolewa hukumu nilipata Goosebumps kuona Abdallah zombie Anaachiwa huru
Katika hukumu zilizonishangaza na hii pia mpaka naona huyo Bageni ni kama mbuzi wa kafala tu hii hukumu kwangu ingekua na nguvu huyo Zombie nae angekua anahangaika kukata rufaa maana kupitia yeye ndio tulijua kuna majambazi kutoka Mahenge alietangaza yupo huru.
 
Hao waliokumiwa kunyongwa huwa wanapewa special treatment wanakula vizuri , hawafokewi , na hulala sehemu nzuri.

Na maaskari wanaowalinda hawaruhusiwi kuvaa viatu wala mkanda na huwa hayo malindo yanombaniwa ukipangwa huko unakuwa upo stress free
Hakuna chakula kizuri jela kaka labda kitoke nje familia ndio walete ila sio cha wao kupika hakuna..
 
Katika hukumu zilizonishangaza na hii pia mpaka naona huyo Bageni ni kama mbuzi wa kafala tu hii hukumu kwangu ingekua na nguvu huyo Zombie nae angekua anahangaika kukata rufaa maana kupitia yeye ndio tulijua kuna majambazi kutoka Mahenge alietangaza yupo huru.

Hakuna dili litapigwa bila kuwashirikisha wakubwa hasa madili Makubwa ya kuanzia mil 200

Na ukiangalia mil 200 ya mwaka 2006 ilikuwa hela nyingi Sana .

So kilichofanyika ni kumtoa mtu kafara
 
Kama unakumbuka vizuri hili lilikua kundi la pili kupotea watu wa madini wakitokea Mahenge kwa kelele za Wananchi ikabidi Mzee Kikwete aunde tume na kabla ya hapo pana hela nyingi ziliibiwa kariakoo na foleni ile na majambazi hawakukamatwa alipigwa risasi mpita njia aliekua anaonyesha njia waliyopita..
 
Duh
 
Haki imetendeka lakini bado haitoshi kurudisha imani kwa jeshi la polisi bado kuna matukio yenye kutia mashaka na kuogopesha yanaendelea kutokea. Serikali inapaswa kuupitia upya mfumo wa jeshi la polisi.
 
(Ameandika Malisa G. )
SSP Christopher Bageni atanyongwa hadi kufa. Ndivyo mahakama ya rufaa ilivyoamua. Maamuzi ya leo ni ya mwisho ktk mwenendo wa kesi yake. Hana pengine pa kukata rufaa, pa kukimbilia, wala pa kupinga. Mahakama imeamua anyongwe hadi afe. Jaji Stellah Mugasha amegonga nyundo. Itz over.

Hawezi kukata rufaa tena kwa sababu hukumu ya leo ni review ya hukumu iliyotolewa na mahakama hiyo September 16, 2016, ambapo alihukumiwa kunyongwa hadi kufa na jopo la majaji watatu wakiongozwa na Jaji Benard Luanda. So hakuna mahakama ya kujadili tena shauri lake, labda Rais ampe msamaha.

Kwa wasiokumbuka Bageni alikua Mkuu wa Upelelezi wilaya ya Kinondoni. Mwaka 2006 yeye na wenzie wakiongozwa na aliyekua Kaimu RPC Dar, Abdalah Zombe, walituhumiwa kupanga njama za kuwauwa wafanyabiashara watatu wa Morogoro.

Zombe anadaiwa ndiye aliyeongoza wenzie kwenye mpango huo, baada ya kujulishwa kuwa wana madini na fedha kiasi cha shilingi milioni 200.

Walikamata gari waliyokua wameikodi. Wakamuongoza dereva hadi msitu wa Mabwepande. Wakapora madini pamoja na fedha zote walizokua nazo. Kisha wakawafunga vitambaa vyeusi usoni na pingu mikononi. Kisha wakawapiga risasi za kisogoni na kuwauwa wote akiwemo dereva wa taxi waliyemkodisha.

Kesho yake Zombe akaita media na kusema wameua majambazi yaliyokua yanarushiana risasi na Polisi. Rais Kikwete akaunda tume ya Jaji Kipenka kuchunguza. Ikabainika hawakuwa majambazi. Kilichouma zaidi walikua ndugu wa familia moja. Mama mmoja alipoteza wanae watatu. Watoto wa familia 4 wakapoteza baba zao, na wake wanne wakawa wajane kwa tamaa za polisi.

Zombe alifanikiwa "kuchomoka" kwenye kesi hii baada ya kusota rumande kwa miaka kadhaa. Lakini Bageni alipatikana na hatia akahukumiwa kunyongwa. Akakata rufaa ikafeli, akaomba review ya kesi, na rulling imesomwa leo kuwa ANYONGWE HADI KUFA.

Waliomtuma hawapo nae Segerea, wala hawatanyongwa pamoja nae. Atanyongwa peke yake. Wanaohangaika nae saivi angalau kumfariji ni familia yake. Zombe hayupo, OCD wake hayupo hata IGP wa wakati huo hayupo. Ni yeye mwenyewe, na atanyongwa mwenyewe.

Hii iwe fundisho kwa wote wanaotumwa kufanya maovu leo e.g kuteka, kuua na kupoteza watu. Ipo siku utajikuta peke yako. Anayekutuma hatakuwepo. Utasimama wewe mwenyewe kutoa hesabu ya maovu yako. Kama si hapa duniani basi hata mbinguni, lakini ipo siku utalipa. Kama ambavyo wema ni mbegu, na ubaya pia ni mbegu. Humea, hukomaa, na ni lazima UVUNE.!
Story tu. Zombe alitoka sababu ya dini yake.
 
Inasikitisha sana
 
Mbaya zaidi kikosi hicho kilikua kinatokea hapo Urafiki kituo cha Polisi wakiwepo na Wanawake Polisi wakatili nao walifariki baada ya kuachiwa huru damu za watu ni nzito sana.
Karma lazima ifanye Kazi .

Nimekaa kota , hawa jamaa maisha yao huwa sio mazuri karma huwa zinasambaratisha familia zao na wao wenyewe . nimeishi nao nawaelewa Sana .dhulumati.
 
Back
Top Bottom