Natamani sana andiko hili la hukumu ya Afande Bageni lisomwe vituo vya Polisi na Makazi yao kwenye Paredi

kwa bahati mbaya, polisi hata wapate mateso au maumivu gani huwa hawatetewi, wanachukiwa, though kwa upande mwingine kazi yao inafanya wengi tulale usingizi. tung'ate na kupiliza, ni watoto wetu hao, kaka zetu, dada zetu, mama zetu na kadhalika.
 
Kombani!!??
 
Selina Kombani?
 
Bado tunasubiri wale wa mtwara nao wale kamba.
 
kwa bahati mbaya, polisi hata wapate mateso au maumivu gani huwa hawatetewi, wanachukiwa, though kwa upande mwingine kazi yao inafanya wengi tulale usingizi. tung'ate na kupiliza, ni watoto wetu hao, kaka zetu, dada zetu, mama zetu na kadhalika.
Ukweli mchungu ni kwamba Askari Polisi wengi zaidi ni Wahalifu wabaya Sana, wengi wao wamemwaga damu nyingi sana za watu wasio na hatia. Askari Polisi ambao ni raia wema watenda haki ni wachache Sana kupita kiasi. Polisi Wahalifu ndio ambao wameliteka Jeshi hilo.
Kumbuka: Ubaya ndio unaovuma zaidi kuliko wema.
 
Ingependa na aliyewatuma akaunganishwa katika hiyo Kesi.

Kumuachia Huru Huyo Mkuu wao inafikirisha namna haki inavyotendeka.
Nakumbuka Sana jinsi huyo aliyewatuma akijibu hoja za baadhi ya watu. Alisema bila kusita kwamba yeye hatofanyiwa lolote na wala hatafungwa kwa vile anajua Sheria ilivyo. Hapakuwepo na ushahidi wa moja kwa moja wa kumuhusisha yeye na mauaji hayo.

Ila ukijiuliza kuwa mtu akikutuma kuua mwenzio pasi na ushahidi wa maandishi wala mtu yeyote aliyesikia kuhusu hayo je wewe uliyeua utajitetea vipi?
 
Amen, kila upandacho ndicho uvunacho. Si kila aliyepo hospitalini, gerezani, masikini, familia mbaya n.k basi ameonewa, wengine ni mkono wa Mungu upo juu yao
 
Ndio maana nasisitiza tukatae ulevi wa Dini.

Sio vibaya kuwa na dini ila kuendekeza dini sana kila unayemuangalia hutaiona status yake wala ubinadamu wake bali dini yake.
Namshukuru Mzee wangu alitoa huo ulevi nikiwa bado nakua kwa hiyo sina huo ujinga maana yeye alikua anasema kumuona mtu mwingine ni tofauti na wewe kwa sababu ya dini yake huo ni ujinga toeni ujinga kwa kutotofautiana kwa dini zenu..
 
Kwanza sheria yakunyongwa inafanya kazi kwa usahihi au ni maneno maneno tu .
Hata isipofanya!

Kusoteshwa condemn kwa maisha yote, si afadhali kunyongwa!
Unasota kwa stress za kila siku na uhai wako utategemea kudra za wanasiasa.

Wafungwa wa kunyongwa ambao hukumu yao ilikuwa haijatekelezwa katika utawala wa Nyerere, lakini Rais Mwinyi alipoingia madarakani, kaja kuidhinisha wanyongwe.

Kifupi mfungwa aliyepo condemn, anapigania kupata uhuru wa mfungwa wa kawaida, yaani kutolewa condemn na kufungwa hata maisha, mateso yaliyoje!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…