Natamani sana kila member humu wa JamiiForums atumie jina na pamoja na picha yake halisi

Natamani sana kila member humu wa JamiiForums atumie jina na pamoja na picha yake halisi

Umeangalia upande mmoja tu. Hii haikuja tu kibahati kama unavyoifikiria. Hii hivi ilivyo inafanya mtu aongee uwazi ulivyo,bila kificho. Hakuna media yoyote hapa Tz inayoweza kuweka kitu kwa uwazi zaidi ya hii. Kitu ambacho walio kwenye madaraka hawakipendi,ksbb ya uwazi uliomo humu ambao hawataki kuusikia. Kwa hiyo tukiwa wazi hakuna atakaejaribu kukosoa kwa uwazi. Hii ilipiganiwa mpaka kuwa hivi. Kuna watu wamelala ndani kwa ajili ya hili

Kwa hiyo kama umetumwa na systems kujaribu kusukuma hiyo mada mbele utachemka tu. Kama unataka iwe hivyo nenda huko what'sup
 
HAhahah mkuu me sihusiki huko nimetoa mada nione maoni ya wadau wa humu jf tu

Mkuu hata wanaohusika huko nao wanasema hawahusiki. Unaona ngoma ilipo?

Suala la msingi linabakia:

IMG_20211015_144814_546.jpg

Au nasema uongo ndugu yangu?
 
Umeangalia upande mmoja tu. Hii haikuja tu kibahati kama unavyoifikiria. Hii hivi ilivyo inafanya mtu aongee uwazi ulivyo,bila kificho. Hakuna media yoyote hapa Tz inayoweza kuweka kitu kwa uwazi zaidi ya hii. Kitu ambacho walio kwenye madaraka hawakipendi,ksbb ya uwazi uliomo humu ambao hawataki kuusikia. Kwa hiyo tukiwa wazi hakuna atakaejaribu kukosoa kwa uwazi. Hii ilipiganiwa mpaka kuwa hivi. Kuna watu wamelala ndani kwa ajili ya hili

Kwa hiyo kama umetumwa na systems kujaribu kusukuma hiyo mada mbele utachemka tu. Kama unataka iwe hivyo nenda huko what'sup
Sijatumwa mkuu nimejaribu kuleta mazo tu wala sikua na nia mbaya mkuu, pia hongera kwa mchango wako mkuu
 
Leo nimetafakari sana juu ya hili jambo, kwa maana wanachama wa humu wa jf wakitumia majina pamoja na picha zao halisi kutaleta faida zifuatazo:

1. Kutaongeza kuheshimiana, endapo kila member humu atatumia jina pamoja na picha yake halisi kutapelekea kuheshimiana kwa kuwa member wengi humu wanachukuliana poa kwa kuwa ID sio halisi kwahiyo unaweza kuta katoto ka mwaka 2000 kanamtimulia vumbi mtu mzima tena wa miaka 70 huko.

2. Kutapunguza idadi ya watu kutumia ID zaidi ya moja , kama mjuavyo wengi humu wana ID's hata 10 kwa ajiri ya maslai yao binafsi hivyo kama mtu ili afungue account lazima atumie jina pamoja na picha yake original itakua ngumu mtu huyo kuwa na ID's zaid ya moja.

3.Kutarahisisha upanikanaji wa mchumba, mpenzi humu jukwaani, Hii naisema kwa kuwa wanawake wengi humu jukwaani wanachukulia sana poa wanaume wa humu jukwaani kwa kuwa awajawaona wanavyofanania, hivyo kama members humu wakitumia utambulisho wao halisi itakua ni rahisi kumpata mchumba tena ata mke humu jukwaani.

4. Kutapunguza utapeli, wengi humu wanatumia ID ambazo hazima taarifa za ukweli kwa ajiri ya kufanya utapeli hivyo endapo kama members humu watatumia majina na picha zao itakua rahisi ata kuwapata kwani picha na jina ni halisi.

Ni hayo tu wakuu kama kuna sehemu nimesahau kugusia unaweza kuongezea nyama

NAWASILISHA.
Kuwa mfano
 
Sijatumwa mkuu nimejaribu kuleta mazo tu wala sikua na nia mbaya mkuu, pia hongera kwa mchango wako mkuu

Hadi hapo mpaka sasa unasema je?

Mwendelezo "solo" hivi hivi au bado unaona na namba za NIDA kabisa ingekupendeza zaidi 😁😁?
 
Hadi hapo mpaka sasa unasema je?

Mwendelezo "solo" hivi hivi au bado unaona na namba za NIDA kabisa ingekupendeza zaidi 😁😁?
Hahah mkuu me naona kama mtu itampendeza kuweka picha aweke na asietaka aache maana hakuna ulazima
 
PM zipo kwa wanaodhani wamefikia levels za kujuana kiundani.....
Alafu fake ID's zina raha yake coz mtu unakuwa huru.
Wengine n most wanted[emoji23][emoji23], mtatukosesha haki ya kushiriki humu.
 
Hahah mkuu me naona kama mtu itampendeza kuweka picha aweke na asietaka aache maana hakuna ulazima

Tatizo lililopo ni kuwa hata Kingai, Sirro, Lion Chawene na wasiojulikana wanamsimamo kama wako 😁😁.

Nakumbuka bwana Max (mola ampe ustahamilivu) amekaa sana central, kesi na faini juu kwa kudinda kumtambulisha memba kama bwana zinc ili waliojimilkisha nchi kinyemela wamchukulie hatua kali kwa kile tu alichoandika.

Ni kwa sababu hizo hata kama wewe ni unyasi kweli tukikuona tusistuke?

Mwone mwenzio huyu.

IMG_20211018_151514_922.jpg

Inawezekana je?

Hiiiiii bagosha!
 
PM zipo kwa wanaodhani wamefikia levels za kujuana kiundani.....
Alafu fake ID's zina raha yake coz mtu unakuwa huru.
Wengine n most wanted[emoji23][emoji23], mtatukosesha haki ya kushiriki humu.
Sawa mkuu nimekupata ID's fake zina umuhimu lakini sometimes humu jf dharau nyingi
 
Tatizo lililopo ni kuwa hata Kingai, Sirro, Lion Chawene na wasiojulikana wanamsimamo kama wako 😁😁.

Nakumbuka bwana Max (mola ampe ustahamilivu) amekaa sana central, kesi na faini juu kwa kudinda kumtambulisha memba kama bwana zinc ili waliojimilkisha nchi kinyemela wamchukulie hatua kali kwa kile tu alichoandika.

Ni kwa sababu hizo hata kama wewe ni unyasi kweli tukikuona tusistuke?

Mwone mwenzio huyu.

View attachment 1978879

Inawezekana je?

Hiiiiii bagosha!
Aisee ni kweli mkuu lakini mimi sikua na nia hiyo kama watu wanavyonitafsiri humu
 
Back
Top Bottom