Vishu Mtata
JF-Expert Member
- Dec 15, 2019
- 15,954
- 35,415
Mkuu kwanini kwenye uzi wako umemtaja sana huyo class mate wako, anahusika vipi na wewe kuumwa??
Ndie unaamini anakuroga??
Ndie unaamini anakuroga??
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Kama hayajakukuta kaa kimya mkuu,,dunia ni zaidi ya uijuavyo,,,vitabu vya dini vyote vinatambua izo nguvuUtakuumiza (Mind over matter) hata kama haupo ukishauamini unaweza hata kukuua (unakuwa hujiamini na kukosa confidence) in short wewe ndio unajiroga, na watu kama wewe ni hatarishi kwa jamii huchelewi kugombanisha watu kwa kuwaita wachawi
Nisaidie angalau namba yake mkuuMtafute Yesu Kristo, sio mchungaji, mtume wala nabii.
Namba yake ni: YESU KRISTO, mwite.Nisaidie angalau namba yake mkuu
Hajawahi kukutwaa, muache aongee atakavyo.Afadhali dada endelea kunitetea.
Maana Hawa wengine wana vichwa vigumu sana!
Kwahio sababu wazungu walishafanya na wewe leo ufanye ? Ushauri wa bure kujikita kwenye hizi Imani au kushiriki ni kupotea (Akili ina nguvu sana) hata leo hapa ukianza kuwaza kwamba unakufa unakufa na kujikosesha raha na kunungunika mwisho wa wiki kweli utakufa (mind over matter)Kama hayajakukuta kaa kimya mkuu,,dunia ni zaidi ya uijuavyo,,,vitabu vya dini vyote vinatambua izo nguvu
Hao wazungu wenyewe walishafanya sana hayo mambo
Mambo ya Giza yanazingua sana, yanaharibu sana maisha yetu. Ushauri wangu, manabii hawatakusaidia. Tafuta watumishi wa ukweli watakuombea, lakini na wewe jitahidi sana kufanya kwanza Toba, kuna uzi mmoja walishare wanaJF kuhusiana na toba, iligusa kuiombea ardhi, wazazi, wazee na wadau waliweka mistari ya biblia. Ukifatisha na kukiri kwa imani, utaanza ona utofauti. Pia kuna uzi wa matumizi ya Chumvi ya mawe, nadhani Mshana Jr alishea huu uzi. Unaweza ukakusaidia. Mungu akusaidie kushinda huo mtihani.Habari yenu ndugu na jamaa zangu !
Kwanza ninge elezea kuwa hiki nilicho andika hapa sio hadithi ya kufikirika bali ni mambo halisi yaliyopo mitaani na kwenye yetu.
Kwanza nianze na historia Fupi ya maisha yangu shuleni.
Nisingependa kutaja jina langu ,ila kwa ufupi nilianza shule ya msingi ya msasani A iliyopo hapa dar.
Nilipata marafiki wengi shuleni na Mungu alinijalia uwezo wa kiakili darasani.
Katika mtihani wa taifa darasa la 7 nilifaulu vizuri na kuchaguliwa kwenda kawe ukwamani secondary school.Pia rafiki yangu wa darasa la saba aliyeitwa MENGI FESTO alifaulu sio kivile ,ila alichaguliwa kwenda GOBA secondary school.
Nikiwa nasoma secondary, watu wa mtaani ,wanao jua na kuutumia sana ushirikina/uchawi wakaanza kunichezea bhana.
Nilipata ugonjwa wa masikio ghafla ,nikawa sisikii vizuri.
Baada ya wiki nikapigwa homa kali sana,tukaenda kwa mganga nikapona.
Mambo hayakuishia hapo Kuna kipindi nikiamka asubuhi kwenda shule ,naamka nikiwa nimechoka sana.
Watu fulani mitaani walikuwa wakiniangalia kwa jicho baya sana, sikutilia maanani.
Pia sikuwa najua chochote kuhusu teknolojia ya ushirikina.
Basi nikawa mdoli wa kuchezea ,Mara nachukiwa shuleni ,naadhibiwa bila sababu, kusinzia hovyo darasani, Kuna kipindi nilikuwa napoteza KumbuKumbu.
Kuna baadhi ya wanafunzi nilikuwa nakaa nao mtaa mmoja. Hao walikuwa ni washirikina pia. Hawa washenzi hawakuwa na akili sana ,ila waliishi kwa raha huku wakinipiga kijicho kisha wanapeleka ujasusi wao huko uchawini.
Kuna kiongozi wa dini , shekhe aliwahi kutuambia shuleni , HATA USOME VIPI KAMA HUJUI MANBO YA ULIMWENGU WA NGUVU ZA GIZA HUJAKAMILIKA.
Nilimdharau huyu shekhe ila leo ninaamini.
Mtaani niliona matangazo ya waganga.
*TUNA SAFISHA NYOTA
*TUNAONDOA NUKSI
*TUNATOA TIBA
*TUNAWEKA KINGA MWILI, BIASHARA,NYUMBA
Matangazo hayo niliyadharau pia.Niliamini mimi Nina akili sana.
Nilipofika form 4 nikafanya mtihani wa taifa mwaka 2014.Siku tunayo Fanya mtihani nilishuhudia mwanafunzi akichanganyikiwa kisha akatoka kwenye chumba Cha mtihani na kukimbia kurudi nyumbani kwao.
Naamini ni Shambulio la kishirikina.
Mimi pia machozi yalikuwa yakinitoka bila kujizuia.Sio kama nilikuwa nalia huku nafanya mtihani,hapana machozi yalikuwa yakinitoka tu kama maji.
Lakini nashukuru nilimaliza mtihani salama.
Matokea yalipotoka nilikuwa nimefaulu.Rafiki yangu MENGI FESTO wa GOBA alifeli .
Habari za kufaulu mtihani wangu zikasambaa mtaani kwetu.Aisee majimama na vibibi hivyi mnavyo vionea huruma, walikuwa na vijicho vya husuda sana.
Waliniangalia huku wakibinua midomo.
Nikaanza shule ya makongo high school,kule kawe jeshini.
Vijicho mtaani vikawa vikali zaidi .
Baada miezi mnne mambo yangu yalianza kuharibika.Nilipata ugonjwa wa miguu kufa ganzi,ute joints za mwili ukapungua nikawa siwezi kutembea .Hivyo sikuenda shule tena.
Siku zilikatika ,miezi ikapita na mwaka ukasonga ,maisha yangu yakawa kupambana na Hawa washenzi.Nimeshuhudia mauza uza mengi aisee.
Mpaka Leo hii ninapo andika haya napambana.Ndani nimeweka box la dawa asilia na nina vitabu vya tiba asilia.
Hapa nilipo mimi ni mgonjwa.
Karibia viungo vyangu vyote vya mwili vimerogwa.
Ubongo,ngozi,pua,macho,misuli,tumbo,damu,mifupa,nywele,joints , vyote hivi vimerogwa . Nina magonjwa yote hapo.
Pia nina jini mbaya mwilini,Nina nuksi kali na vifungo vya kichawi yaani nisipate mafanikio.
Nilienda kwa mwaposa lakini wapi hali iko palepale.Naendelea kupambana.
Wakati huu rafiki yangu MENGI,anaendelea kuishi kwa raha na mafanikio tele.Sio kwa sababu ana akili sana bali ni mwenye maarifa ya uchawi.
Natamani shuleni tungekuwa tunafundishwa kuhusu technology hii ya nguvu za Giza ,hakika mitaani wasingekuwa na uwezo wa kuharibu maisha yangu.
Naendelea kutafuta msaada nipate tiba. Shukrani!View attachment 3245104
Hizo ni stori tu za vijiweni.
Naweza kwa upande mmoja nikakubaliana na wewe, ila uchawi upo,,,,cha msingi ajitahidi kufikiria positive things katika ubongo wake, aachane na negativity na pia amuombe Mungu na aamini yeye ni mzima na atapona, asiingize negativities zozoteUchawi haupo, sitochoka kuwaambia.
Mauza uza unayoona kwenye maisha yako ni njia fupi ambazo ubongo wako hutumia kuchakata mambo yasiyo rahisi kuelewa(cognitive biases)
Ubongo wako una kazi kubwa mno, hauwezi fanya kila kitu kikamilifu.
Kama mdau mwana JF alivyokueleza, ukishaanza dawa za waganga, umewafungulia njia. Sali kwa imani, stay Positive usiruhusu kuwaza mambo ya kurogwa, japo ni ngumu kwa mwanzo, ukizoesha akili kua wewe ni mzima, utakua mzima. Nguvu ipo ndani yako.Nimeshuhudia marafiki zangu wengi ma Genius wakifa Bado vijana! Eti mtu msomi anakufa kwa sababu ya homa , pharmas na hospital dawa hazifany kazi ?
Hao wanao waroga hawana elimu sana.Mfano mmama ameishia darasa la tatu.
Ila kama elimu ya teknolojia ya kishirikina ingefundishwa shuleni hakika wasomi tungeshinda maishani.
Ruksaaaaa
Usiku huu.........................................................Ruksaaaaa
NdiyoUsiku huu.........................................................
Hii Same mji sijui kimji kijiji cha Wachaga iliwahi kutufelisha Pepa darasa zima, sisi tulikua tunaona same kumbe ni Same Kilimanjaro hukofundi Yuko same
Ukukuta Chungu kimevunja au Nazi imevunjwa kwenye njia panda na wewe ukawa hima ndio mtu wa kwanza kupita hio njia km Mungu wako akikuonesha mapema na ukaona kabla haujaviruka au haujavivuka ndugu usiviruke hivyo vitu wala usivipige mateke wala usijitie ujanja kutaka kuvihamisha rudi ulipotoka acha mtu mwingine aje kuviruka fanya km umekutana na Chatu au Anaconda rudi ulipotokaHapo kwenye fikra huru napingana nako, watu wengi wenye kusema hakuna uchawi hasa humu ukitizama hoja zao wote zinafanana wanarudia mambo yale yale tu na wanazungumzia uchawi kwa mitazamo ya wazungu ambako watu wengi hawaamini wala kujihusisha sana na uchawi.
Uchawi upo mkuu wewe amini hivyo uchawi upo uswahilini uchawi upo ushuani kote kumejaa uchawi mtupu tena kwenye miji ya biashara au maeneo ya biashara ni kuna uchawi wa wazi wazi kabisa watu wanaroga asubuhi wanaroga mchana wanaroga usikuUchawi haupo, sitochoka kuwaambia.
Mauza uza unayoona kwenye maisha yako ni njia fupi ambazo ubongo wako hutumia kuchakata mambo yasiyo rahisi kuelewa(cognitive biases)
Ubongo wako una kazi kubwa mno, hauwezi fanya kila kitu kikamilifu.
Hahaha mkuu wewe bado sana utoto umekujaa ukikua utaelewa wewe subiri jamaa wakufungie kazi upate pigo moja takatifu km alilopigwa farao ndio utaamini kweli uchawi upo, farao alinyoosha mikono juu pigwa urogozeo mpaka akaelewa, hio inaelezwa kwenye kitabu cha dini Biblia na Quran yaan hata hapo bado huamini km uchawi upo?Ungekuwepo tungekuwa tunautumia maeneo kama hospitalini,
Ungerahisisha sana maisha.
Bado hayajakufika bado hujaingia kwenye 18 zao ukawekwa mtu kati usiombeeHizo ni stori tu za vijiweni.