Natamani shuleni tungekuwa tunafundishwa teknolojia ya nguvu za giza na kiroho

Natamani shuleni tungekuwa tunafundishwa teknolojia ya nguvu za giza na kiroho

Kwanza pole kiongoz..
Naona watu humu wanapinga uchawi haupo au haohao ndo wachaw wenyew huwez juwa, ukitaka ujue uchawi upo ingia baadhi ya sekta haswaa mambo ya biashara wanarogana sana hawa, au mambo yakuendee poa mitaan/shulen/kanisan au kijijn kwenu. Jua litakuwakia kama hujajipanga kimwil na kiroho.

Viongoz weng % kubwa wapo pale uchawi umewasaidia.

Kiuharisia UKUBARI au UKATAE Ukitaka mafanikio either ULOGE SANA nor USALI SANA. Huwa ni sir ya mtu ila ukiulza utaambiwa PAMBANA SANA

OVA
Uko sahihi kabisa.
Huwa napenda watu kama wewe , ni watu open minded
 
Hongera kwakuweza kufikiri nje ya Box. Uko na idea nzuri ila jaribu kulifanyia maboresho idea yako na mwisho wako utakuja kujua nini unataka uwe.

Kwa sasa hivi uko na general idea ila fanyia tafiti unachokitaka kisha utakuja kukipata
Ahsante sana. Kwa sasa nataka kusoma teknolojia hii ya kishirikina niijue kwa undani .niwe jeshi kali.
 
Hata hao wanaosema wamewahi kushuhudia uchawi ukifuatilia vizuri utakuta ni story tu iliyosambaa kutoka kwa mtu mmoja hadi mwingine lakini kiuhalisia hakuna mtu aliyeshuhudia chochote.

Kwa mfano anaweza kukutwa mtu njia panda amekaa juu ya ungo amejipaka majivu, unga au masinzi, yuko na nazi, mayai pamoja na vibuyu mtu akaruka na story kuna mtu ameanguka na ungo ila hajashudia huyo mtu kuanguka na ungo, watakuja watu wengi hapo kumzunguka na wataondoka na story kuna mtu ameanguka na ungo ila ukweli ni kwamba hakuna hata mmoja aliyeshuhudia huyo mtu akianguka na ungo.
Wewe sio Bure una matatizo!

Kwa mfano umri gani wewe?
 
Hivi kwanini watu wenye kupinga uchawi huwa hawakutani na matukio yeyote yenye kuhusishwa na uchawi kwenye maisha yao? Yani huwezi kukuta yeye kuwahi kukutana na tukio lenye kuhusishwa na uchawi wala hata kuelezea tukio la ndugu au rafiki lenye kuhusu uchawi? Yani wapinga uchawi ni kama wanapinga historia ya karne hizo vitu ambavyo havipo tena kwenye jamii.

Ni sawa na wenye kusema ndoto hazina maana yeyote nao hukuti wakisema wanaota yani kama wao hawaoti kabisa.

Hivi ni kwa nini ipo hivyo?
Hawapendi kuwa wakweli ! Wanaweza kuwa wachawi wenyewe au washamba mjini
 
Hakika bruh huyu jamaa anajua mambo yangu. Nasikia hata anasafiria nyota yangu.
Na huwa hapendi mafanikio yangu.
Unasikia?? Kwann unamtuhumu hivyo mkuu, una hakika gani??

Kwenye maisha wengine kutoboa na wengine kutotoboa ni kawaida.
 
Ahsante sana. Kwa sasa nataka kusoma teknolojia hii ya kishirikina niijue kwa undani .niwe jeshi kali.
Tumia simu yako ya android vizuri, hakika ndio mwalimu wako Google ina kila kitu unachokitaka ikisaidiana na YouTube, changamoto ni kujua nini unachokitaka na je nitakipataje kwa kutafuta hayo maarifa google na YouTube....

Kila la kheri
 
anaesema uchawi haupo ujue ni kichaa,biblia,quran imekili unani ubishe....au nyi ndo wachawi wenyewe?
 
Tumia simu yako ya android vizuri, hakika ndio mwalimu wako Google ina kila kitu unachokitaka ikisaidiana na YouTube, changamoto ni kujua nini unachokitaka na je nitakipataje kwa kutafuta hayo maarifa google na YouTube....

Kila la kheri
Shukrani ndugu. Naiweza hata kujua namna ya kujitibu huko.
 
Hata hao wanaosema wamewahi kushuhudia uchawi ukifuatilia vizuri utakuta ni story tu iliyosambaa kutoka kwa mtu mmoja hadi mwingine lakini kiuhalisia hakuna mtu aliyeshuhudia chochote.

Kwa mfano anaweza kukutwa mtu njia panda amekaa juu ya ungo amejipaka majivu, unga au masinzi, yuko na nazi, mayai pamoja na vibuyu mtu akaruka na story kuna mtu ameanguka na ungo ila hajashudia huyo mtu kuanguka na ungo, watakuja watu wengi hapo kumzunguka na wataondoka na story kuna mtu ameanguka na ungo ila ukweli ni kwamba hakuna hata mmoja aliyeshuhudia huyo mtu akianguka na ungo.
Unaweza ukawa sahihi kwa matukio kama hayo ila uchawi ni zaidi ya matukio kama hayo, kwa maana wapo watu wengi wanaoenda kwa waganga kwa shida zenye kuhusishwa na uchawi au wenye kufanya wenyewe mambo yenye athari zenye kuaminika ni uchawi.

Tatizo humu unajadiliwa uchawi kama ni matukio ya maajabu ndio kama hayo ya kuona sijui mchawi n.k ila kiuhalisia hiyo ni sehemu ndogo sana ya kinachohusishwa na uchawi.
 
Ahsante sana. Kwa sasa nataka kusoma teknolojia hii ya kishirikina niijue kwa undani .niwe jeshi kali.
Pengine sio lazima usomee uchawi, uchawi ni energy tu hivyo unaweza ukajifunza mambo ya energy kwa aina nyengine isiyo ya uchawi na ukaweza kujikinga na uchawi na mengine yasio ya uchawi ambayo huathiri watu pia.
 
Habari yenu ndugu na jamaa zangu !

Kwanza ninge elezea kuwa hiki nilicho andika hapa sio hadithi ya kufikirika bali ni mambo halisi yaliyopo mitaani na kwenye yetu.

Kwanza nianze na historia Fupi ya maisha yangu shuleni.

Nisingependa kutaja jina langu ,ila kwa ufupi nilianza shule ya msingi ya msasani A iliyopo hapa dar.
Nilipata marafiki wengi shuleni na Mungu alinijalia uwezo wa kiakili darasani.

Katika mtihani wa taifa darasa la 7 nilifaulu vizuri na kuchaguliwa kwenda kawe ukwamani secondary school.Pia rafiki yangu wa darasa la saba aliyeitwa MENGI FESTO alifaulu sio kivile ,ila alichaguliwa kwenda GOBA secondary school.

Nikiwa nasoma secondary, watu wa mtaani ,wanao jua na kuutumia sana ushirikina/uchawi wakaanza kunichezea bhana.

Nilipata ugonjwa wa masikio ghafla ,nikawa sisikii vizuri.
Baada ya wiki nikapigwa homa kali sana,tukaenda kwa mganga nikapona.
Mambo hayakuishia hapo Kuna kipindi nikiamka asubuhi kwenda shule ,naamka nikiwa nimechoka sana.

Watu fulani mitaani walikuwa wakiniangalia kwa jicho baya sana, sikutilia maanani.

Pia sikuwa najua chochote kuhusu teknolojia ya ushirikina.

Basi nikawa mdoli wa kuchezea ,Mara nachukiwa shuleni ,naadhibiwa bila sababu, kusinzia hovyo darasani, Kuna kipindi nilikuwa napoteza KumbuKumbu.

Kuna baadhi ya wanafunzi nilikuwa nakaa nao mtaa mmoja. Hao walikuwa ni washirikina pia. Hawa washenzi hawakuwa na akili sana ,ila waliishi kwa raha huku wakinipiga kijicho kisha wanapeleka ujasusi wao huko uchawini.

Kuna kiongozi wa dini , shekhe aliwahi kutuambia shuleni , HATA USOME VIPI KAMA HUJUI MANBO YA ULIMWENGU WA NGUVU ZA GIZA HUJAKAMILIKA.
Nilimdharau huyu shekhe ila leo ninaamini.

Mtaani niliona matangazo ya waganga.
*TUNA SAFISHA NYOTA
*TUNAONDOA NUKSI
*TUNATOA TIBA
*TUNAWEKA KINGA MWILI, BIASHARA,NYUMBA

Matangazo hayo niliyadharau pia.Niliamini mimi Nina akili sana.

Nilipofika form 4 nikafanya mtihani wa taifa mwaka 2014.Siku tunayo Fanya mtihani nilishuhudia mwanafunzi akichanganyikiwa kisha akatoka kwenye chumba Cha mtihani na kukimbia kurudi nyumbani kwao.
Naamini ni Shambulio la kishirikina.

Mimi pia machozi yalikuwa yakinitoka bila kujizuia.Sio kama nilikuwa nalia huku nafanya mtihani,hapana machozi yalikuwa yakinitoka tu kama maji.
Lakini nashukuru nilimaliza mtihani salama.

Matokea yalipotoka nilikuwa nimefaulu.Rafiki yangu MENGI FESTO wa GOBA alifeli .

Habari za kufaulu mtihani wangu zikasambaa mtaani kwetu.Aisee majimama na vibibi hivyi mnavyo vionea huruma, walikuwa na vijicho vya husuda sana.
Waliniangalia huku wakibinua midomo.

Nikaanza shule ya makongo high school,kule kawe jeshini.
Vijicho mtaani vikawa vikali zaidi .

Baada miezi mnne mambo yangu yalianza kuharibika.Nilipata ugonjwa wa miguu kufa ganzi,ute joints za mwili ukapungua nikawa siwezi kutembea .Hivyo sikuenda shule tena.

Siku zilikatika ,miezi ikapita na mwaka ukasonga ,maisha yangu yakawa kupambana na Hawa washenzi.Nimeshuhudia mauza uza mengi aisee.

Mpaka Leo hii ninapo andika haya napambana.Ndani nimeweka box la dawa asilia na nina vitabu vya tiba asilia.

Hapa nilipo mimi ni mgonjwa.
Karibia viungo vyangu vyote vya mwili vimerogwa.

Ubongo,ngozi,pua,macho,misuli,tumbo,damu,mifupa,nywele,joints , vyote hivi vimerogwa . Nina magonjwa yote hapo.

Pia nina jini mbaya mwilini,Nina nuksi kali na vifungo vya kichawi yaani nisipate mafanikio.

Nilienda kwa mwaposa lakini wapi hali iko palepale.Naendelea kupambana.

Wakati huu rafiki yangu MENGI,anaendelea kuishi kwa raha na mafanikio tele.Sio kwa sababu ana akili sana bali ni mwenye maarifa ya uchawi.

Natamani shuleni tungekuwa tunafundishwa kuhusu technology hii ya nguvu za Giza ,hakika mitaani wasingekuwa na uwezo wa kuharibu maisha yangu.

Naendelea kutafuta msaada nipate tiba. Shukrani!View attachment 3245104
Nenda madrasat, kule utafundishwa kila kitu kuanzia kufuga majini na kuaminishwa vitu visivyo na ukweli juu ya Muddy. Ukitoka hapo tu full mchawi wa vitabu.
 
Pengine sio lazima usomee uchawi, uchawi ni energy tu hivyo unaweza ukajifunza mambo ya energy kwa aina nyengine isiyo ya uchawi na ukaweza kujikinga na uchawi na mengine yasio ya uchawi ambayo huathiri watu pia.
Wazo la elimu ya energy ni jipya kwangu. Je topic hiyo inaitwa je? Kama Kuna somo nipe jina lake!
 
Mfano mtu kasoma halafu mtaani watu wenye husuda wana mfunga asifanikiwe.Msomi hajui chochote masikini .Anaanza kuteseka .Nyota yake inatumiwa.

Hiyo elimu na cheti vitakuwa na faida gani?
nakubaliana na wewe nchi zilizoendelea elimu ya ulimwengu wa roho inafundishwa vyuoni ni elimu nzuri sana ukiijua hakuna kitakachokusumbua watu wote waliofanikiwa kwa kiwango cha juu wanaitumia elimu hii
 
Dah kumbe ndio maana wenzetu wako mbali aisee. Nasikia hadi mahospitalini wanatibu magonjwa aina yote
 
Back
Top Bottom