Song of Solomon
JF-Expert Member
- Aug 5, 2021
- 2,752
- 5,609
Naumia si kwasababu Mungu amekuchukua bali ni kwakua sikupata kuwa mume wako katika kipindi chote cha miaka sita ya ndoa yetu. Bado nakumbuka meseji yako ya mwisho uliyonitumia uliniambia “Mume wangu njoo tu nyumbani, samahani kwa kukusumbua lakini nataka tu nikuone sijisikii vizuri!”
Niliisoma na ulipoona siijibu ulipiga simu, natamani hata ningepokea mimi na kusikia sauti yako kwa mara ya mwisho lakini nilimpa mwanamke mwingine akapokea.
Sijui kama ulijua lakini ulimuambia aniambie kwa heri. Nikijua ni vile vitisho vyako vya kila siku kuwa utaondoka nilipuuza na kuamua kulala huko huko mpaka saa sita usiku rafiki yangu mmoja alipokuja kunigongea usiku.
Nilizima simu na hakuna mtu aliyekua akijua nilipokua kasoro yeye hivyo alitafutwa na kuja kunipa taraifa, alikuja na kugonga kisha kuniambia tuondoke, hata hakunionea huruma aliniambia kuwa “Mke wako hayuko tena, amefariki!”
Niliishiwa nguvu sijui nini cha kufanya, nilirudi nyumbani na kuwakuta wenetu wadogo wakilia hawajui wanalia nini lakini walilia kwakua wanaona watu wengine wanalia.
Waliniona badala ya kunikumbatia walikua wananikwepa, walikua wanaogopa kwakua Mama yao hayupo tena. Mimi ni kama mgeni kwao, hawanijui na mimi siwajui. Mke wangu baada ya mazishi watu wote wameondoka.
Nimebaki mimi nawatoto tu, ndugu zangu wote wamerudi kuendelea na familia zao, michepuko yangu nayo hata hainitafuti tena, wale wanawake wote waliokua wanakupigia simu kukutukana hawanipigii tena simu.
Binti wa kazi uliyemuacha ameondoka siku mbili tu baada ya mazishi. Nakumbuka mara ya mwisho niliyokupiga nilikuambia kama umechoka ondoka uniachie wanangu.
Naona umechoka kweli umeondoka na kuniachia wanangu lakini sasa sijui hata niwapeleke wapi? Kila siku wanamuulizia mama, naumia zaidi kwani mimi wananiogopa, wananiangalia kama shetani wananiona kama natisha, hii ni kwasababu sikuwahi kuwa Baba yao, siku zote nilikua bize na starehe.
Nakukumbuka sana mke wangu ni miezi miwili tu tangu uondoke lakini naona kama miaka mia, kweli nilikukosea natamani hata urudi kwa dakika tano tu ili niwe mume wako nikuonyeshe namna ninavyojutia.