Kwani utajiri ni nini!!?
Mimi nina bus za mikoani 4, fuso 3, "vichanja" viwili, mashamba nane(hekari 16200),lodges (1* mpaka 3* saba), nyumba za kupangisha 17.
Je mimi ni tajiri au sio tajiri!?
Kama ni tajiri,kwani namfikia "mooo" wako!!??
Ni masikini wa shukrani, akili na elimu pekee ambaye anaweza kujivunia umasikini.
Utajiri ni neema,na kukiri kuwa u tajiri ni ibada ya sifa na shukrani kwa yule atoaye utajiri na kila kilicho chema, yaani Mungu Baba wa Mbinguni.
Umasikini ni laana. Kujisifia kuwa wewe ni masikini ni kutomshukuru Mungu kwa kukuumba kwa mfano wake.
Maana yake ni kumwambia Mungu kuwa wewe si mfano wake.