Natangaza rasmi kuachana na siasa

Wewe ulichelewa sana,wenzio tulivyoona Mbowe amemzunguka Slaa pamoja na Lissu wake na kumkabidhi Lowassa bendera ya chadema tokea hapo niliona Mbowe ni mfanyabiashara sio mwanasiasa makini mpaka Sasahivi siwezi amini chadema ya Mbowe na Lissu wake tena.
 
Kaka umeongea point kubwa sana. Mbowe jana amedhihirisha personal conflict. Nakuunga Mkono nimeamua kuachana pia na siasa ya kitanzania. Hii ni Kutokana na anguko kubwa sana la CHADEMA ninalo liona mbele.
 
Pole ulikosa elimu sahihi kuhusu siasa zetu!kuamini Tz Kuna upinzani was kuchukua Dola no tatizo la akili!

Why!!?

Coz misingi ya ccm sio chama Chama Cha siasa Bali ni Imani ya kidini na Dola inayoilinda iendelee kuwepo Kwa madaraka!!

Vyama vya upinzani KAZI Yao kubwa ni kuisaidia ccm kutawala Kwa kuhodhi mawazo mbadala ya wananchi Ili wananchi wasije leta machafuko Kwa kukosa chombo Cha kuwasemea !!yaani hizo vurugu za hoja zinatibu hisiamoyo za wananchi!!!

Pole man!
 
I support u my brother... Mimi nilishtuka mapema mwaka huu nika mute
 
Ukiwa mwanasiasa ni sawa na mpigania uhuru. Mpigania uhuru hapiganii kwa ajili yake au familia yake Bali kwa ajili ya taifa lake.
Utafanya kosa kubwa ukijitoa kwenye siasa kisa tu umekosana mtazamo na kiongozi wa chama Cha siasa.
 
Ndugu kabla ya kuondoka CHADEMA, nikuulize,

Umewahi kusoma kisa Cha kamanda mmoja, jemedari, hero aliyeshinda vita nyingi lakini mwisho wake alikuja kuuwawa na mwanamke kirahisi tu!!

Yaani mlisurvive Kwa Magu, Leo mnapoteana chini ya uongozi wa Sa100?

Futa thread Yako wewe ni jemedari, pambana, njia IPO mbeleni Sema huioni.

Ubarikiwe πŸ™
 
Lipumba aliandika~ga na barua wakati ule, alipomaliza kula hela za wale jamaa akarudi kwenye chama. Wilbroad akatangaza kustaafu siasa....vina muda basi! kiko wapi ? Leo hii amejaa tele kwenye majukwaa ya siasa.

Siasa ni uongo. Ukilazimisha kuwa ukweli utaishia kuumia. Siasa ni UCHAFU, ukiingia kwenye siasa lazima uchafuke kwa namna yyt. Siasa ni propaganda. Siasa ni uuaji, ufisadi, ubadhirifu, utapeli, uvivu, uchochezi, ulafi, ujambazi, utekaji, uadui na mengine mengi.

Lakini siasa ni ajira. Hii ya kusimama majukwaani kuhadaa watu kwamba unaomba wakuchague ili ukawatetee ni utapeli tu kama ilivyo kwa utapeli mwingine. Ndio sababu mwanasiasa analipwa mshahara na marupurupu kedekede.


Wanasiasa wote ni walewale hakuna mwenye afadhali kwasababu ya nature ya siasa ilivyo. Huwezi kuwa mkweli ukadumu kwenye siasa katu asilani abadani haitokaa itokee.

If you can't fight them join them
 
Nakumbuka 1995 NCCR chini ya hayati Agustine Lyatonga Mrema Vs BWMkapa.Mrema alikuwa na sera nzuri sana na CV nzuri sana na experience kubwa sana.Alikuwa anabebwa juu anaambiwa mzee zima gari acha tukusukume .Wanachama wa NCCR mageuzi walijitoa kusapoti chama usiku na mchana kwa hali na mali wakiamini kuna mageuzi au kuna u seriuous ..mwisho wa siku kuja kugundua ni PLACEBO..(maigizo/kitu bandia)
Mfumo ule ule na kilichofanywa na hayati Mrema na upinzani uliofanywa kipindi kile ndio unaoendelea miaka yote(BANDIA/MAIGIZO)
Nafikiri na naamini tupo kwenye mfumo wa chama kimoja.(vyama vingi vilivyopo ni bandia)
At least miaka ya nyuma kidogo kulikuwa na at least na bunge la vyama vingi na ilisaidia kidogo kuleta chachu ya maendeleo .
Ila kwa sasa naona ni tumeridi rasmi mfumo wa chama kimoja kwa 100% kuanzia ngazi ya serikali ya mitaa mpaka juu.
NAAMINI NA NAFIKIRI BONGO kuna chama kimoja tu na vivuli (BANDIA-vyama vingine vinavyosemekana ni vya upinzani bandia)
 
Upinzani sio chama ni ideology, unabaki vipi chadema wakati unajua kabisa uongozi wa juu umewasaliti?
 
Japo sikuwa mwanachama kama wewe ila naungana na wewe kwa hatua ulichozukua.
CDM ni ya Mbowe, aachiwe mali yake.

Japo siungi mkono Lissu kuhama chama, naona aendelee kubaki. Mwisho wa Mbowe utafika tu.
 
Ukiachana na Siasa, umetangaza Rasimi kuyakabidhi Maisha yako Kwa wengine.

Cha msingi, palipo na Nuru ndiko pakwenda.

Subiri baada ya Uchaguzi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…