Kwa taste yako, unaonekana unataka gari ya "youth generation ' tuseme.
Kama hauna experience ya gari kabisa, ungetafuta nyingine, lakini kama umefanya research na hautaki kutoka kwenye izo tatu, mi naona ungeipa kipaumbele
Subaru kisha
Crown kisha
BMW.
Sijui unataka ukae nayo siku ngapi kisha uuze na unanunua JP au kwa mtu hapa Dar na budget yako ni kiasi gani.
Ila Subaru itakua cheap kununua, cheap ku-run especially kwenye mafuta baadhi ya spare, lakini itakua na resale value ndogo sana. Jana
politics observer ameleta hii topic kwamba kwann Imprezza zinashuka sana bei. Unaweza ukanunua leo Mil 15 baada ya mwaka Mil 10 usipate mteja.
Ila Crown itakua reliable zaidi, most comfortable, spare na mafuta vitakunyonya. Pia gharama za kununua kama unaagiza zitakua juu sana.
Kusema kweli BMW ungeacha tu. Izo nzuri zikiwa barabarani zimewasha Angel Eyes. Resale value ya ovyo, spare ghali, na sio durable (usiniquote vibaya. BMW ikivuka miaka 10+ tokea itengenezwe inahitaji matengenezo mengi kwasababu izo E90 zina plastic parts nyingi sana kwenye engine, hafu engine yake inapata joto iyo ova tanuli, pia simple service tu unakuta unaacha 250k,)!, kila kitu inataka premium kuanzia oil, mafuta, spare.
Kuhusu mmafuta, usijidanganye eti nitakua na misele michache.
Ukinunua gari unabadirisha marafiki, unakaa Ubungo anaanza kwenda kunywa bia Bagamoyo, kunyoa Posta, Kununua nguo Temeke, bado bavy nipeleke airport baby tutoke.
Namaanisha lifestyle litabadirika, bila ata ww kujua.
Kwahiyo jitahidi upate ambayo ni rafiki kweenye mafuta (Subaru), spare na service cheap (Subaru/Crown).
Alternative unaweza angalia Toyota na Honda.