Nategemea kwenda Shinyanga kwa pikipiki aina ya Boxer, CC 125

Vipi mdau, hapa hospitali ya shinyanga tukuandalie kitanda cha wodi ipi mkuu?? Chafua Wodi ya wagonjwa wa ajali? ICU? Wodi ya wagonjwa wa mfumo wa upumuaji??
ndugu yangu nitakuja tu kukusalimia...nimeendesha pikipiki mwaka wa 10 huu kwenye jiji lililopo busy la dar es salaam.. hivyo ninauzoefu mkubwa sana
 
shukrani sana....kibwa bajeti yangu ni ndogo bila hivyo siwezi kumudu masafa ya huko kwani nikifika nategemea kuzunguka sana...hivyo nilidhani kwenda na pikipiki yangu kutaniepushia gharama za nauli huko vijijini...
Safari ndefu mimi nafanyaga Hivi... mara nyingi december huwa nakua ARUSHA.

nikifika arusha nina survey maeneo sana kwahyo nahtaji usafiri wa uhakika.

Naanzaga isafirisha pikipiki gharama ni LAKI 1 tu,inatangulia ARUSHA.

ikifika tu mimi naondoka huku dar naenda ARUSHA nakuta chombo kinanisubiri. Naanza misele na ratba zangu zinaendelea

Nikimaliza,natumia utaratbu ule ule kuirudsha pk pk DAR.
 
ni wazo zuri...kwa shinyanga naenda tu mara moja na kurudi...nitatumia tu siku 2 panapo majaliwa
 
kweli kabisa ila kwa safari ndefu haki vile hii ndio safari yangu ya kwanza. na nitaleta mrejesho hapa
 
Weka kwanza side mirror ndo uje tuongee,,,,yaani mkifika Road tukiwapigia hone badala ya muangalie kwenye mirror mnaanza kugeuza vichwa
 
Unatumia mnyama gani kiongozi
 
Weka kwanza side mirror ndo uje tuongee,,,,yaani mkifika Road tukiwapigia hone badala ya muangalie kwenye mirror mnaanza kugeuza vichwa
mirror, zipo kiongozi hizo ni picha tu...nipe neno lako ndugu. pengine litanijenga
 
ila kwa dar es salaam hii pikipiki naizurulia siku nzima kuanzia asubuhi saa 11 hadi usiku saa 6 bila kupumzika, hivyo nadhani itahimili, japo natamani nipate wazoefu ambao walishawahi kwenda longtrip kwa usafiri kama huu
Zingatia sana adjust ya mnyororo ndo ugonjwa safari ndefu
 
Mkuu tembea tu mwendo wa kawaida 70-100 baada ya km kama 300 hivi pumzisha engine kidogo lakini usiinzime
Kuwa makini na mashimo ya barabarani
 
Kuna wale madogo waliamua kwenda Karatu kwa pikipiki aina ya SanLG kutokea Morogoro, hata Dumila hawakuiona wakakata moto! Kuna mwalimu aliamua kusafiri kwa pikipiki kwenda kumzika mamake huko Simiyu akitokea Dodoma Msalato sec. Hata Manyoni hakuiona akakata moto! Tutofautishe pikipiki za masafa marefu wanazotumia Wazungu na hizi bodaboda! Kwa bahati unaweza kufika salama lakini iwe "at your own risk!"
 
Mkuu tembea tu mwendo wa kawaida 70-100 baada ya km kama 300 hivi pumzisha engine kidogo lakini usiinzime
Kuwa makini na mashimo ya barabarani
kweli ndugu yangu barabara zetu ni hatarishi sana kwa sisi waendesha piki piki sio salama hata kidogo
 
shukrani ndugu yangu...ushauri wako nitauzingatia sana
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…