Manjagata
JF-Expert Member
- Mar 7, 2012
- 13,942
- 15,371
Pikipiki mkuu wewe mwenyewe ndiye bodi!Walikata moto kwa ajali ama nini??
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Pikipiki mkuu wewe mwenyewe ndiye bodi!Walikata moto kwa ajali ama nini??
Dar-Shy ni 1000km kasoro kidogo.Unataka kujitafutia shida zisizo na msingi mkuu hivi unajua kama pikipiki inachosha tulikuwa tunazitumia Tabora , Singida na Dodoma kwenda kwenye minada unakodi 10,000 kwa siku unaendesha mwenyewe km 60 kuingia ndani. Ukirudi kama umepigwa magongo kuna mwenzetu yeye ndo alijifanya mpori mpori aliumwa kifua mwezi mzima na homa. Sasa sembuse 750 go and return 1,500 Km plus za kuzunguka.
Na pale kwenye uzi umeandika unataka kujua matumizi ya mafuta.Hesabu haujui kupiga?natokea dar es salaam
Duh, hatari sana!
So 2,000 Km hizo kwa pikipiki hayo ni maafa ya kujitakia na uchovu usioelezeka lile baridi la kuanzia Dodoma , Singida mda wa jioni alafu unaukimbiza kwa speed 80 via 100 baada ya starehe itakuwa kero.Dar-Shy ni 1000km kasoro kidogo.
We nenda kuna mmoja yeye kaenda musoma na sasa anatumia mtambo bila wasiwasiNdugu wanajamvi nategemea kwenda Shinyanga nikitokea Dar es salaam kwa Piki piki boxer cc125 mwenye uzoefu itakuwa vyema ukanisaidia.
Nataka kujua mafuta naweza kutumia kiasi gani. Je, nijiandae kwa changamoto gani barabarani pikipiki hii ninayotaka kuitumia ni mpya. na nina tegea kwenda na kurudi....
View attachment 2760635.
Pikipiki ya 125cc inafanya vizuri masafa hata ya 1000km. Boxer na Tvs zina mfumo wa Timing chain zina utulivu.shukrani sana....kibwa bajeti yangu ni ndogo bila hivyo siwezi kumudu masafa ya huko kwani nikifika nategemea kuzunguka sana...hivyo nilidhani kwenda na pikipiki yangu kutaniepushia gharama za nauli huko vijijini...
Ikiwezekana ubadilishe na oil kabisaAsante sana. nitajaza full tenki nadhani mpaka dodoma nitaongeza tena full tenki nyingine
Hitimisho lako lina maana aachane na hayo mawazo yake ,apande basiMkuu mi Nina boxer cc150 Huwa napiga sana hizo safari mpaka Kuna nyakati nishawahi sinzia nikiwa road kutokana na uchovu, nakumbuka Kuna siku nilisinzia mpaka pkpk ikasimama yenyewe ndipo nikashtuka nlikuwa natumia Honda Manji(cc125).
Kwa safari yako Dar to Shy
Hakikisha pkpk ipo fresh Kwa maana umeifanyia service ya kutosha na hakikisha nat zimekazwa vzr(zinakawaida ya kulegea, ni hatari sana), tairi weka oko(ziwe tubeless), honi iwe poa,sight mirror, breaks zote ziwe vzr, indicators zote ziwe poa, Oil tumia zenye kumudu umbali mrefu km vile Oryx, Mogas, Advanced etc. Pia beba baadhi ya spana muhimu kama vile size 10, 19,20 etc Kwa ajili ya kutatulia matatizo madogo madogo. Funga walau tofali moja la block ili kupata utulivu na kupunguza kuyumbayumba ukipigwa na upepo mkalli.
Kwa upande wako, Vaa jacket nzito sana, kofia ngumu,viatu vya kupanda mpaka kwenye ugoko, miwani, begi ambalo utaweka vinywaji hasa energy na maji.
Kuhusu wese, Lita moja inatoboa km 35 mpaka 45, hivyo ni kupiga tu hesabu zako(tumia minimum km 35 Kwa Lita).
Ukiwa safarini, Vaa earfone zako weka nyimbo au simulizi ufurahie safari na pia ikate usingizi. Pia, ukihisi uchovu simama pumzika, nawa maji usoni au km Kuna huduma ya kuoga is best option, sight mirror iwe unajiupdate muda wote, jitahd kubana upite kushoto Kwa mstari wa road kuepuka kujisahau alafu ukashtuliwa na honi ya GSM au HOOD. Kuwa makini muda wote Kwa kuchukua taadhari zote za kiusalama, kumbuka gari kubwa zikiwa main road huwa hawajali waendesha pikipiki wanawachukulia watu wabishi hivyo hawajali kama nawe unategemewa na familia.
Kumbuka:
Kuomba Dua muda wote, beba vitambulisho Incase ili iwe rahisi, pia toa updates Kwa mtu wako wa karibu ili kama utarest iwe rahisi kufuatilia, kama una familia andika wosia.
Nikutakie safari nje, enjoy the View mkuu.
🙆 Asante sana ndugu. Yangu umenifafanulia vizuri sana..😁😁😁wewe: ulale vizuri unywe maji na uwe na vitu vya kufikiria kwa hayo masaa 10-12 utakayotumia peke yako njiani
safety gears: uwe na helmet sahihi inayofunika
kichwa kizima, yenye shades za jua sio
hizi za 50k kushuka chini. koti na suruali ya mvua, koti na suruali ya kusafiria, na ndani za kuzuia baridi kama sweater. gloves ukipenda. viatu vigumu lakini comfortable shoes, sbb ya upepo beba kitu cha kuzuia kelele cha maskio, dont overdress, be comfortable.
service: service pikipiki vizuri na kagua kila
kitu, paka nati zilizolegea
mafuta: weka mafuta sheli sahihi, na dadisi sehemu gani kuna umbali mkubwa bila sheli
ikibidi uwe na lita 1/2 ya akiba umebeba
stops: full tank inaweza kupa 250-300km. pumzika nusu saa kila full tank ukijaza. kila
ukisimama jinyooshe na unywe na kula vitu light, ukila shibe sana utaanza kusinzia.
njia: kama ni njia mpya kwako, tumia
google maps ikusaidie usijepotea
speed: kwa boxer cruise at 70-90km/hr,
zaidi utaichosha engine maana ni natural
cooled, pia kagua temp au taa yoyote ya alarm
kama inayo.
mvua: angalia weather forecast, kama
mwezi ujao mvua zita anza ni hatari na kero
kuendesha pikipiki kwenye mvua
vibrations: pikipiki ndogo ina vibrations kubwa kwa umbali mrefu uta anza kuskia tofauti kdg, 200-300km ni kawaida, zaidi ya hapo hali inabadilika either ganzi au kupoteza mawasiliano, boresha kiti au vaa sponge trouser
distance: dar shy ni karibu 980km, utatumia 12hrs au zaidi kwa spidi ya boxer (less than 100kph), ukifika dodoma jikague kama uendelee au upumzike hadi kesho yake.
vifaa: beba maji kdg, spana za muhimu, ya kuzibia pancha na pump ndogo ya mkono, ubebe pia nyaraka za pikipiki. beba na kitambulisho au note ata yenye mawasiliano ya watu wako wa karibu ikitokea chochote
donts:
-usiendeshe usiku, kabisa
-usibebe mizigo zaidi ya kibegi cha mahitaji muhimu
-sio mashindano boxer ni pikipiki ndogo, fanya kama unaenda posta tu.
-dont drink
jumla: kama ni adventure usiende mwenyewe tafuta company, au usiende mbali sana (moro panatosha), kama ni kuipelekea shy ipakie lorry tu, kama ni uharaka na adrenaline hutawahi ni shughuli ya siku nzima especially kwa
boxer, kama we sio mvumilivu baada ya km 200 tu utajiuliza sana nani alikutuma ufanye hio safari..