Mkuu mi Nina boxer cc150 Huwa napiga sana hizo safari mpaka Kuna nyakati nishawahi sinzia nikiwa road kutokana na uchovu, nakumbuka Kuna siku nilisinzia mpaka pkpk ikasimama yenyewe ndipo nikashtuka nlikuwa natumia Honda Manji(cc125).
Kwa safari yako Dar to Shy
Hakikisha pkpk ipo fresh Kwa maana umeifanyia service ya kutosha na hakikisha nat zimekazwa vzr(zinakawaida ya kulegea, ni hatari sana), tairi weka oko(ziwe tubeless), honi iwe poa,sight mirror, breaks zote ziwe vzr, indicators zote ziwe poa, Oil tumia zenye kumudu umbali mrefu km vile Oryx, Mogas, Advanced etc. Pia beba baadhi ya spana muhimu kama vile size 10, 19,20 etc Kwa ajili ya kutatulia matatizo madogo madogo. Funga walau tofali moja la block ili kupata utulivu na kupunguza kuyumbayumba ukipigwa na upepo mkalli.
Kwa upande wako, Vaa jacket nzito sana, kofia ngumu,viatu vya kupanda mpaka kwenye ugoko, miwani, gloves ngumu za mikono ili kujikinga na baridi nyakati za usiku, begi ambalo utaweka vinywaji hasa energy na maji.
Kuhusu wese, Lita moja inatoboa km 35 mpaka 45, hivyo ni kupiga tu hesabu zako(tumia minimum km 35 Kwa Lita).
Ukiwa safarini, Vaa earfone zako weka nyimbo au simulizi ufurahie safari na pia ikate usingizi. Pia, ukihisi uchovu simama pumzika, nawa maji usoni au km Kuna huduma ya kuoga is best option, sight mirror iwe unajiupdate muda wote, jitahd kubana upite kushoto Kwa mstari wa road kuepuka kujisahau alafu ukashtuliwa na honi ya GSM au HOOD. Kuwa makini muda wote Kwa kuchukua taadhari zote za kiusalama, kumbuka gari kubwa zikiwa main road huwa hawajali waendesha pikipiki wanawachukulia watu wabishi hivyo hawajali kama nawe unategemewa na familia.
Kumbuka:
Kuomba Dua muda wote, beba vitambulisho Incase ili iwe rahisi, pia toa updates Kwa mtu wako wa karibu ili kama utarest iwe rahisi kufuatilia, kama una familia andika wosia.
Nikutakie safari njema, enjoy the View mkuu.