Nateseka sana na complicated U.T.I. Naelekea kukata tamaa, nisaidieni niondokane na mateso haya

Tumia AZUMA hii ni kiboko yake, baada siku tatu nipe mrejesho
 
Nimewahi kuumwa hii UTI Sugu. Nilichomwa sindano za mishipa zaidi ya wiki moja ndio nikapona. Sasa dawa waliyotumia ndio sikumbuki but ilikuwa kwenye vichupa fulani hivi wanavunja na kuivuta ile dawa kwa sindano.
 
Kagonge sindano 5 direct kwenye mshipa mkononi wiki tu unapona. Sijui inaitwaje dawa ila ukifika dispensary kokote wanajua. Wanapiga kwenye mshipa inaingia kazini wiki mwili sumu yote kwaheri.
 
Mkuu pole sana,karibu kuzingatia usafi kama vile nguo za ndani,bafuni na chooni,maji unayotawadhia yawe masafi na salama

Ukizingatia hayo jaribu pia kuzingatia mlo wako kwa siku,matunda na vyakula vya asili view muhimu kwako,

Mwisho wa siku jaribu kutumia huu mmea ni nzuri sana kwa UTI ,hakika hutatumia tena madonge ya hospital
 
Kuna tatizo kubwa tunalitengeneza sasa hivi kupitia haya matumizi holela ya dawa za antibiotics.. Huko mbeleni itakuwa ni gharama sana kumtibu mtu mwenye UTI!!

Maana tunatengeneza usugu "super bug" kwa matumizi holela ya dawa za antibiotics. Ushauri wa kuwa na algorithm ya kutibu magonjwa mbalimbali sio UTI tu ni muhimu sana..

Hata ukiangalia muongozo wa matibabu unaotumika Tanzania (STG) ni aibu sana, maana haupo updated kwa current medical issues na hata diagnosis zake zinategemea sana "symptoms" kuliko "signs" na haupromote matumizi ya maabara katika kugundua tatizo kwa mgonjwa.

Kiufupi UTI inatibika ila unahitaji kujua ni dawa ipi sahihi unatakiwa kutumia badala ya kutumia tu madawa ovyoovyo kiholela.. Ni lazima kufanya "urine culture" mapema kabla ya kuanza kutumia dawa yoyote ile kwaajili ya UTI.
 
Uko sahihi mkuu tatizo tunalitengeneza kwa matumizi holela ya dawa hasa ishu kubwa ikiwa hii UTI.
 
Tafuta majani ya mlonge pamoja na mizizi yake chemsha kunywa kikombe kimoja asubui na kimoja jioni! Baada ya week nenda kapime
 
Maumivu huja hadi kwenye kinena!

Mwanaume ana kinena? Pole sana Mheshimiwa
 
Kagonge sindano 5 direct kwenye mshipa mkononi wiki tu unapona. Sijui inaitwaje dawa ila ukifika dispensary kokote wanajua. Wanapiga kwenye mshipa inaingia kazini wiki mwili sumu yote kwaheri.
Nimeshapita hapo pia. Nilichoma Powercef kwenye mshipa kwa siku 5 mfululizo ikifuatiwa na capsules amoxycillin kwa siku 5 tena lakini sikuona tofauti yoyote. Yaani hata sielewi??
 
Tatizo huku mikoani kipimo cha culture and sensitivity hakipatikani.
 
Lazima afanye culture and sensitivity ili kujua dawa iko sensitive au resistant, kuna mda doxy zinakua resistant so lazma ifanyiwe sensitivity kujua itamtibu au vp
Wengi wameshauri nifanye Culture ya mkojo. Nimekuwa kwenye antibiotics kwa muda sasa bila mafanikio. Ni muda gani (duration) unafaa kuacha antibiotics kabla ya kufanya culture maana nasikia ukipima ukiwa unatumia antibiotic au muda mfupi baada ya kuacha kutumia haitoi majibu.
 
Simple dawa, chukua nanasi, osha vizuri, menya, chukua maganda ya juu, tia kwenye sufuria, chemsha na maji, chuja anza kujinywea!! Siku 14!!
 
Unasumbuliwa na Protozoan aina ya trichomoniasis na sio bacteria. Una tabia ya kufanya kinyume na maumbile? Piga nikuelekeze dawa ya hospital na mitishamba utapona. 0762766665
Diagnosis uliyokwishafanya na conclusion uliyofikia sio sahihi. Sijawahi kufanya mapenzi kinyume na maumbile tangu nimezaliwa.
 
Nenda ukapime na tezi dume mana hizo dalili kama zinafanana
Kama maelezo yangu yanavyojieleza, nimepimwa tezi dume nikaambiwa tezi haijaongezeka kutokana na aging kama ilivyo kawaida kwa tezi hiyo ila imevimba (inflamed) sababu ya maambukizi ya uti. . Ndio maana option ya tiba ikawa ni dawa badala ya upasuaji.
 
Nikupe dawa. 0762766665
 
Chemsa majani ya mlonge na majani mti wa ukwaju piga glass kadhaa utaona matokeo bora zaidi
 
Habari Catherine
Naomba ufafanuzi kidogo wa namna ya kutumia hiyo blacks seeds oil na kalinji seeds powder
Namaanisha atumie kiasi gani kwa siku na mara ngapi?
 
Umeblock DM,ila nilikuwa na jambo LA kukuuliza.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…