Kaka, mimi ni mwanamke nilishasumbuliwa sana na UTI Japo yangu sio hiyo complicated, bali ilikuwa sugu, nilikunywa sana antibiotics, nilichoma sana pawercef ila tatizo linarudi wiki tu baada ya kumaliza dose, maumivu ya tumbo kwenye kinena yalinisumbua mpaka nikahisi nina tatizo kwenye kizazi ikabidi nikamuone gynecologist nikakuta kizazi hakina shida, yeye mwenyewe akabaini ni UTI inanisumbua, akanipa dawa bila mafanikio, nikahamia upande wa tiba miti(medicinal plants) nimekunywa blacks seeds oil na kalinji seeds powder mpaka nimepona. Kuanzia mwaka juzi mpaka leo nikipima UTI sina. Nenda maduka ya asili wana dawa nyingi za kutibu hayo maradhi kaka ulizia unga wa habat soda au mafuta ya habat soda uwe unakunywa katika chai au uji, maduka ya asili yaliyo karibu nawe utapata