lee Vladimir cleef
JF-Expert Member
- Feb 5, 2013
- 9,571
- 35,475
Hapo zamani,Sadam huseini wa Iraq alifanya kama anavyofanya Putin wa Urusi Leo kwa kuivamia nchi ya Kuwait.
Marekani na washirika wake wakaivamia Iraq na kuipiga Hadi ikatoka Kuwait.
Miaka kadhaa baadae Slobodan Milosevic wa Yugoslavia aliwapiga kishenzi waasi na raia waliokua wanataka kujitenga wa mji wa Kosovo Huku wakikimbia bila kujua wanakimbilia wapi.
Yalikua ni mapigano ya kikabila.
NATO wakaingilia kati na kushusha kipigo Cha mabomu Cha Hali ya juu katika miji na vijiji vya Yugoslavia upande wa Serbia iloyokua ikiongozwa na Milosevic aliekua anawashusgia vipigo vikali sana wakosovo,na hatimae Milosevic akasalimu amri.
NATO walifanya hayo hayo kwa Yugoslavia Huku umoja wa mataifa ukipinga kuwa damu itamwagika sana, bila idhini ya umoja wa mataifa NATO walipiga mabomu sana upande wa Serbia.
Marekani alipiga Tena Iraq yeye na washirika wake kwa madai kuwa Iraq ilikua imeficha silaha za maangamizi.(weapons of Mass destruction) WMD.
Wamarekani na washirika wake na wapambe wao walishiriki vita hizo na hatimae Wakamkamata Rais wa Iraq akiwa mzima na kumkabidhi kwa wairaq wasio mpenda wakamnyonga.
Muamar Ghadafi wa Libya nae hakuweza kukwepa mkono mmoja wa Baadhi ya Wanachama wa NATO Marekani na Ufaransa .
Baada ya kuonekana Gadafi anaua raia wake kwa wingi kutokana na guvu ya jeshi lake ,ilibidi Marekani na Ufaransa wakatimia madege kudhoofisha uwezo wa jeshi la Libya na hatimae Gadafi kuzidiwa na kukamatwa na mwisho kuuwawa.
Leo najiuliza NATO wamefikwa na nini?
Matendo anavyofanya Urusi huko Ukraine yanafanana kabisa na matendo ya akina Milosevic,Saddam na Ghadafi.
Marekani na NATO waliweza kushusha mabomu na kuwamaliza nguvu maraisi hao.
Sasa hivi masikini,ukweli nimeingiwa na huruma ,Ukraine inaadhibiwa na Urusi NATO hiihii ambayo ilimpa matumaini Zelensky inaangalia TU jinsi anavyofedheheshwa.
Zelensky Yuko chumbani kwake amevamiwa anapiga mayowe,makele,mwano na Kila aina ya kuomba msaada majirani na marafiki waliokua wanampa matumaini wamesimama pembeni mwa madirisha wanachungulia TU.
Sababu wanayotoa Haina mashiko,kuwa NATO ni kwa ajili ya Wanachama TU.
Ok basi tuache uanachama,tuaangalie na ubinadamu TU,kwa mfano Kuwait,Kosovo,na Libya hazikua Wanachama wa NATO lakini ubinadamu ulikuja na kuwaokoa watu wa nchi hizo.
Sasa kwa Nini NATO inakua na ubaguzi namna hii?
Ukweli sipendi vita,vita inaharibu Kila kitu.watu wasio na makosa ama hatia wanakufa bila sababu wanaacha makazi na kazi zao wanakimbilia kusukijulikana.
NATO- Kuiwait,Kosovo na Libya waliingilia kijeshi lakini nchi zote hizo hazikua Wanachama na kwingine hata umoja wa mataifa haukutoa baraka .
Anachokifanya Urusi Leo kwa Ukraine walifanya akina Sadam,Ghadafi na Milosevic.
Labda tofauti ni ndogo TU,Urusi yeye anasema anaharibu miundimbinu ya kijeshi tuu.