NATO wamefikwa na Nini? Mbona waliweza Kuwait na wakaweza Kosovo,wanashindwa Nini Ukraine?

Kongole kwako, umenena vema sana.
 
hivi weweeeee unaijua 'geopolitics' za ulaya na urusi weweeeee? Hayo mataifa ya ulaya yamekuwa 'overrated sana' kumbuka kuna mchina yupo nyuma ya mrusi! By the way, waarabu wanamsapoti urusi katika hili unasemaje hapo sasa!
hivi weweeeee unaijua 'geopolitics' za ulaya na urusi weweeeee?
Hayo mataifa ya ulaya yamekuwa 'overrated sana' kumbuka kuna mchina yupo nyuma ya mrusi! By the way, waarabu wanamsapoti urusi katika hili unasemaje hapo sasa!

WAARABU WANA NN HAO CHA MAANA!?
OHOO WESTERN WAPO OVERRATED ILHALI HAO NDIO WALIOUNDA UN NA MKASHOBOKA KUJIUNGA NA KUWEKA BENDERA ZENU MAKAO MAKUU PALE NEW YORK.
Bank ya dunia ipo kwao.
Mashirika makubwa ya fedha yapo kwao.
Utasemaje wako overrated!?
Hiyo China uisemayo wewe haijitoshelezi kuisaidia Russia ikainuka .
Ndugu mtake msitake uchumi wa dunia umeshikiliwa na hao mabwana.
 
Sometimes it's better not to drop your comment if you know you don't have a bit of substance to drop here. Sasa lini USA alijaribu kuingia Russia wakati wa WW 1& 2 akashindwa. Mbona mnatufanya mazuzu humu. Kwani ukija na hoja zenye ushahidi wa kihistoria tutakataa?
 
Safi Sana.. WWI Urusi alipigana ndani ya muungano unaoitwa wa Allies, na ule muungano unaoitwa wa Central (ulioongozwa na ujerumani) walipotaka kuingia Russia walikwama. Kwenye world war ii Russia alipigana kwenye muungano wa allies tena na axis walipotaka kuichukua Russia walishindwa..sasa key point yangu hapo hizo nchi zinaunda NATO sasa hivi kama Germany, Hungary, Czechoslovakia, Turkey nk kwenye world war ii walikuwa upande wa Axis ( mjerumani) na walijaribu kuiteka Russia wakashindwa. Kwahiyo kuwepo marekani na hao kwenye NATO will not make any difference
 
Nice explanation! Lakin unasahau kua au maybe hujui mataifa gani yalikua frontline kupigana na aggressors wa WW 2? Russia na Marekani uadui umeanza rasmi na kuiva baada ya ya WW 2, baada ya USSR kushida ulaya mashariki kwa kumtandika Germany na Marekani kushinda Far East kwa kumtandika Japan. Sasa mbona kama hapa wote walishirikiana kuleta balance na amani duniani kwenye hii vita, lini Marekani alijaribu kuingia Russia kwenye huu wakati wa WW 2?
 
Nimemchanganya marekani na NATO kama kitu kimoja, hata hivyo marekani amekua akijaribu kuingia Russia by the back door kwa kutumia nchi jirani za Russia kwa muda mrefu sasa ( Georgia, Crimea nk). Lakin amekwama
 
Nimemchanganya marekani na NATO kama kitu kimoja, hata hivyo marekani amekua akijaribu kuingia Russia by the back door kwa kutumia nchi jirani za Russia kwa muda mrefu sasa ( Georgia, Crimea nk). Lakin amekwama
Sina shida na wewe kuchanga mkuu. Shida yako ni kutoa evidence isiyo support huo mchanganyo wako. Refer ulichoandika hapa chini[emoji116]

"Kifupi ni kwamba marekani na NATO wameshajaribu kuingia Russia mara 2, kwenye world war I na World war II, walipigwa vibaya sana na hawatothubutu tena."
 
Wala Nato hawaiogopi urusi tatizo urusi ina silaaa za nyuklia endapo akipigwa na nato anaweza kuzitumia na kuleta maafa makubwa kwa dunia

Sent from my SM-J250F using JamiiForums mobile app
 
Huyo Russia anayesumbuliwa na ka nchi kama Ukraine kwa siku ya 12 leo hajauteka hata mji mkuu ndo apambane na mataifa makubwa yenye silaha za kisasa?

Putin hadi anatishia kutumia nyuklia ni dalili tosha ameelemewa.

NATO na Marekani hawashindwi kuingia vitani hata kidogo ila ni mbinu ya kumdhoofisha Russia kiuchumi kwanza hadi atie adabu.

Vita vya siku hizi havihitaji physical battle angalia Mchina yupo tuli anajiimarisha kimya kimya kiuchumi.
 
Tatizo chizi anamiliki mabomu ya nuklia na ametishia kuyatumia.
 
Wala Nato hawaiogopi urusi tatizo urusi ina silaaa za nyuklia endapo akipigwa na nato anaweza kuzitumia na kuleta maafa makubwa kwa dunia

Sent from my SM-J250F using JamiiForums mobile app
Si bora unyamaze sio kuchangia. Kwani hizo silaha zimetengenezwa kama mapambo? Si zimetengezwa kwa ajili ya kutumika?

Mpo katika mapambano unamchaguliaje adui silaha? Kwani NATO hawana hizo silaha? Siku nyingine shirikisha ubongo bro unavyochangia ili kuepusha kudharaulika hata na watoto wako kama wamo humu, mtoto anaona mchango dhaifu kama huu bila kujua ni wa mzazi wake anakushambulia na kukudharau
 
Mkuu nadhani we ndo una matatizo ya kutoshirikisha akili vizuri.

Just a reminder; Bomu la nyuklia limetumika mara mbili tu katika historia ya Dunia Kule Nagasaki na Iroshima, hivyo kila mtu anajua scale ya uharibifu wa hilo bomu. Na kwa taarifa yako Nuclear weapons are owned by super powers for being used as "Deterrence" weapons and not as war weapons. And such detterence reasons apply in situations like these of Ukrane's, hence bringing equal balance between world's powers.

Akitokea mmoja akatrigger huu mzigo wa Nuclear hata wewe hapo ulipo iwe bonyokwa au katavi hutasalimika. Narudia tena hutasalimika! So sometimes ni heri tusiropokee kwenye kuchangia mambo ya muhimu.

Bila Nuclear msuguano wa vita kati ya mataifa ungekua mkubwa zaidi ya hivi uonavyo leo. Lakin kumiliki silaha za Nuclear kunafanya wakubwa wa dunia waheshimiane na kucompromise ili Dunia ibaki mahala salama kwa viumbe hai.
 
Wazungu ni wanafiq tu, Mara zote wanajidai kulinda haki za raia mahali pengi duniani hususani bara la Africa mbona sasa hivi moto unawaka kwao na hawafanyi yale waliyokuwa wakiyafanya kwenye baadhi ya Nchi kama Libya,Syria, Lebanon..Africa ya kati na kwingine

Wameingilia baadhi ya nchi na hatimaye viongozi walioko madarakani hawakubaliki kila uchwao tunashuhudia mapinduzi ya kijeshi.

Tunataka kuona Umoja wa Ulaya na Nato zikiichukulia hatua kali Urusi kama, Wao kama Baba wa Demokrasia lazima waonyeshe mfano.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ungekuwa unajua NATO nn wamekusudia kwa URUSI hata wewe ungefanya hivyo hivyo anavofanya Putin .Mimi namuunga mkono sana na yule Raisi wa Ukraina ndio mjnga wa mwisho kabisa kachuuzwa na NATO kaitia nchi yake ktk vita na kuharibu Infructure zote yaani namuona bonge la mbumbavu wa mwishoo any way tuombe vita imalizike na ipo dalili ya kumalizika israili wameingilia kati ya kupatanisha sababu raisi wa Ukraine ni Myahudi mwenziwao.
 
Iraq alipovamia Kuwait nilikuwa huko na nilishiriki
Kuwait ni rafiki mkubwa wa wazungu na wanamlinda kwa mkataba wa miaka dhahari

Kuwait wakati huo population ilikuwa 1m tu ukijumlisha na expatriates
Saddam alipovamia walikuwa askari zaidi ya 1m na mgambo na wale wa akiba walikuwa takriban 3m

Sasa ili kulinda maslahi ya Kuwait na washirika wengine kama Saudia, na GCC wengine ilibidi USA na [emoji636] wamuondoe Saddam hata kama ni rafiki yao maana Iraq na GCC yote bora hao wanawalipa hela ndefu sana

Sasa Ukraine anawapa nini?
Kama ni humanitarian sawa watasaidia wakimbizi ila kwa maslahi mzungu anaangalia tumbo lake tu
 
Kitu unatakiwa kujua vita vyote vya world war I na World war ii, marekani alipigana either kwa kwenda front au kwa kutoa support kwa Allies. Hivyo kushindwa kwao ni kushindwa kwake.
 
Yaani Russia kama ni kupigana kwa mapanga basi anampiga Ukraine na panga lililo ndani ya Hala yake kwa kuwa hataki kumuua ndugu yake! Anamsubiri USA na wapambe wake wajitikeze ndio awachomolee panga!
Huyo USA unayemuabudu ni mhuni TU, anataka asaidiwe na Dunia yote kumdhoofisha Russia!
Hana hata huruma kwa wa'ukraine!
By the way wanaopigana Ukraine sio wukraine TU Bali mamluki wa magharibi waliovalia kiraia!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…