NATO wasema wanafukuzana na wakati kuiwahi Urusi

Webabu

JF-Expert Member
Joined
Apr 29, 2010
Posts
8,870
Reaction score
14,258
Kauli za mataifa yanayounda umoja wa NATO kwa sasa zinatia huruma.Unaweza ukaona hilo katika matamshi ya kiongozi wa umoja huo General Jens Stoltenberg aliposema mataifa hayo yanakimbia na wakati ili kuiwahi Urusi kabla haijakazia katika mashambulio yao makubwa dhidi ya mwenzao Ukraine.

Akaongeza kwa kusema kama mtu mwenye hofu "Na kwa kweli tumeshaona tayari wameanza".... "Kwangu mimi ni muhimu kukimbizana na wakati na kuipatia Ukraine silaha kwa haraka."

Hayo ameyasema Jumanne huko Brussels kwenye makao makuu ya umoja huo alipokuwa akikutana na waandishi wa habari.
 
Na wajitutumue kweli, wakichelewa kidogo tu watawakuta Warusi wameshajimilikisha nchi.
Wahuni wameanzisha jambo lao na lazima walitimize!
 
Secretary General wa NATO ukimwangalia kwa umakini hana tofauti na Zelensky kiakili, wote waigizaji na wendawazimu - hawana habari kwamba maigizo yao yanaweza kusababisha WW3 bila ya kukusudia ie by miscalculation na huo ndio ukuwa mwisho wa Dunina - Putin amewaonya mara nyingi tu, lakini kwa bahati mbaya ujeuri na kiburi cha USA na NATO wanamchukulia Putin poa kabisa!!!

Sasa kama Biden na NATO wanajiona wao zaidi kivita, basi wajaribu kupeleka wanajeshi,ndege za kivita na silaha nzito huko Ukraine wapambane ana kwa ana na jeshi la Urusi ili tuone mwisho wa siku nani zaidi.

Sisi tunacho kishuhudia kila siku ni mikutano makongamano na maazimio chungu nzima ya NATO na USA yasiyo isha lakini deep down hawana ubavu wa kutaka kujiingiza moja kwa moja kwenye vita hii - wanamwachia Zelensky awaswage vijana wadogo teenagers waende kupigana vita ya kipuuzi kwa maslahi ya Merikani na UK -Zelensky anatumika kuwatoa kafara Waukraine wenzake, he doesn't seem to care at all kuwa subject vijana wadogo kwenye meat grinders za jeshi la Urusi na wanakufa kweli kweli, masaa yote anakimbilia kuomba silaha nzito zaidi na fedha, hafikilii hata kidogo kuanzisha mazingumzo ya kuelewana na Putin makamaliza vita kistaarabu after all Waukraine na Warusi ni kama ndugu na Zelensky mwenye is more fluent katika kuzungumza Kirusi kuliko Kiukraine, sijui Zelensky alikubari je kuchonganishwa na wenda wazimu wa magharibi dhidi ya Urusi na Zelensky anakubali kuwasikiliza wanapo mpotosha - he will end up losing everything including his Nation kama ata bahatika kubaki mzima.
 
Sasa kama silaha zinazozalishwa kwa miezi 6 Ukraine aazitumia kwa siku moja alafu bado Urusi anaendelea kumega nchi kimasihara kwanini NATO wasiogope?
Hata ungekuwa wewe lazima uweke mikono kichwani huku ukitafuta uchochoro wa kutorokea 🤣🤣

Kibaya zaidi Urusi akikupiga anakuzunguka weee alafu mwisho anateka silaha uliobaki nazo pamoja na wanajeshi.
Pia kuna habari mbaya kutoka huko NATO kwamba, Urusi akiwateka wanamgambo wa Ukraine hawaui bali anawageuza kuwa jeshi lake na kuwatupa mstari wa mbele.

Urusi ni limbuyu likuubwa kiasi kwamba NATO wakitaka kulitikisa wanajikuta wakitikisika makalio
 
Kauli za mataifa yanayounda umoja wa NATO kwa sasa zinatia huruma.Unaweza ukaona hilo katika matamshi ya kiongozi wa umoja huo General Jens Stoltenberg aliposema mataifa hayo yanakimbia na wakati ili kuiwahi Urusi kabla haijakazia katika mashambulio yao makubwa dhidi ya mwenzao Ukraine.

Akaongeza kwa kusema kama mtu mwenye hofu "Na kwa kweli tumeshaona tayari wameanza".... "Kwangu mimi ni muhimu kukimbizana na wakati na kuipatia Ukraine silaha kwa haraka."

Hayo ameyasema Jumanne huko Brussels kwenye makao makuu ya umoja huo alipokuwa akikutana na waandishi wa habari.
Mkuu mtu mwenye hofu zaidi ni Putin kwamba inakuwaje Taifa kubwa kama Russia tulivyokuwa tunaambiwa hapo kabla kiongozi wao mkubwa wa kijeshi sasa anakuwa chini ya kundi la Wagner Group kwenye vita kule Ukrean kikundi kidogo cha kukodi
 
Putini hana hofu hata kidogo kwani Russia ilijipanga/kujiandaa kitambo sana. Mpango wa USA wa kuidhohofisha Russia kijeshi na kiuchumi ulipangwa kitambo sana na Russia walishausoma kitambo vilevile.
Huyo Zelensky na NATO ni tools za marekani ktk kumdhoofisha mrusi na hawataweza kushinda
 
successfully mkuu., Russia alivyojipanga alibugi sana alisema ataishughulikia Ukraine kwa 72hrs sasa inamkost mwaka 2 tena, budget yake imevurugwa kitambo sana, anapigana kwa hasara, vita ya siku 1 Russia inagaramika Euro 160 million, Urusi sasa amelazimika kukodi majeshi kwa vikundi vya kigaidi dhidi ya Ukraine jesh hana tena, kamaliza vijana wake, wafungwa magerezani na wanajeshi aliplan kuwapeleka mwanzo wote kwisha habar yao, urusi inaenda kuanguka raia wake wanahama nchi kutafuta maisha nchi nyengine
 
Mkuu mtu mwenye hofu zaidi ni Putin kwamba inakuwaje Taifa kubwa kama Russia tulivyokuwa tunaambiwa hapo kabla kiongozi wao mkubwa wa kijeshi sasa anakuwa chini ya kundi la Wagner Group kwenye vita kule Ukrean kikundi kidogo cha kukodi
Acha hizo Hilo ni kundi lake nenda kasome au kasome uchambuz wa @Habibuanga kaelezea vizur kiufupi ni kundi ameunda yeye mwenyewe Putin
 
Hakuna anayekataa kwamba sio kundi lake ni kama huko kwenu unapoamua sasa unapeleka vitani vikosi vya JKT au Zimamoto na Fire ni dalili kwamba hana tena jeshi sasa anatumia hayo makundi na anawalipa hela nyingi kuweka rehani maisha yao, wengi wameuliwa na wanaendelea
 
successfully mkuu., Russia alivyojipanga alibugi sana alisema ataishughulikia Ukraine kwa 72hrs sasa inamkost mwaka 2 tena, budget yake imevurugwa kitambo sana, anapigana kwa hasara, vita ya siku 1 Russia inagaramika Euro 160 million, Urusi sasa amelazimika kukodi majeshi kwa vikundi vya kigaidi dhidi ya Ukraine jesh hana tena, kamaliza vijana wake, wafungwa magerezani na wanajeshi aliplan kuwapeleka mwanzo wote kwisha habar yao, urusi inaenda kuanguka raia wake wanahama nchi kutafuta maisha nchi nyengine
Acha kujidanganya Mzee kwenye vita Kuna kitu kinaitwa propaganda na huwa ni muhimu kweli kweli kama Kuna wana jeshi kwenye huu Uzi watakuelezea . Hizo kauli za wafungwa na blabla zingine ni Moja ya propaganda zenyewe za kivita . Na kuhusu gharama sio kweli maeneo waliyochukua urusi ni yenye utajiri mkubwa Sana wa Mali kwahiyo watafidia haraka sana

Urusi wamechukua ardhi ya Ukraine yenye utajiri wa chuma , utajiri wa chumvi, utajiri wa Aluminum, utajiri wa miji yenye viwanda vikubwa, wamechukua bandari kubwa zote kwenye miji hiyo , wameweza kulinda njia ya kupitisha Bomba lao la kimkakati kupeleka gesi na mafuta ulaya , pia wameweza kupora maeneo yenye utajiri wa mafuta na gesi na kuharibu mpango wa marekan na ulaya kuacha kutumia gesi na mafuta ya urusi na waanze kutumia ya Ukraine. Na Bado amebeba wananchi wa hayo maeneo na atanufaika nao kiuchumi. Na Bado anaendelea kupiga Ukraine na kupora maeneo mengine makubwa zaidi

Mwisho wa siku utajiri huo utafidiwa na kubwa zaid baada ya hii vita kuisha Kuna kitu kinaitwa balance of power inaenda kutokea Sasa hivi rasmi na Dunia itapumua Kwa ujinga wa marekan na vibaraka wake angalau Sasa Kuna block mpya ya urusi mataifa yanawezekana kukimbilia huko na kufanya biashara kama zamani
 
Hakuna eneo hata moja kwenye ardhi ya Ukraine ambayo urusi wamechukua na kuwa comfortable kufanya shughuli za kichumi ni propaganda ya hali ya juu umelishwa, miji waliyotangaza urusi kuchukua ni partially hayako full controlled na urusi vita inaendelea ingawa ni kweli Urusi alikuwa na mpango wakupora hayo maeneo kujimilikisha rasilimali lakini kilichomkuta hakutegemea ndio maana hadi mwaka umeisha bado anapeleka makundi haya na haya kwenye vita wanajeshi wake wanaambulia kufa tu.

Vita alii miscalculate vibaya na sasa anakumbana na changamoto ambazo Urusi kurudi kiuchumi ni ndoto, raia wake wanahama nchi maisha yamekuwa magumu urusi na juzi ametunga sheria kuwazuia raia wake wasiondoke au atawalipisha kodi mara 2 lakini wimbi ni kubwa hata urusi sasa wanaishi kwa khofu.

Marekani wanataifisha hela za matajiri wa kirusi walizoekeza Ulaya na Marekani kuzitoa msaada Ukraine zikiwemo hela za mtoto wa Putin ni vile Putin vita inamugharimu yeye peke yake sasa amekodi silaha kutoka Iran kila ndege na droon inayoangushwa inasoma toka Iran, putin amebakiwa na nuclear ambayo sasa hataweza kutumia alitishia vya kutosha lakini akachemsha watu wanasonga mbele
 
Kauli za mataifa yanayounda umoja wa NATO kwa sasa zinatia huruma.Unaweza ukaona hilo katika matamshi ya kiongozi wa umoja huo General Jens Stoltenberg aliposema mataifa hayo yanakimbia na wakati ili kuiwahi Urusi kabla haijakazia katika mashambulio yao makubwa dhidi ya mwenzao Ukraine.

Akaongeza kwa kusema kama mtu mwenye hofu "Na kwa kweli tumeshaona tayari wameanza".... "Kwangu mimi ni muhimu kukimbizana na wakati na kuipatia Ukraine silaha kwa haraka."

Hayo ameyasema Jumanne huko Brussels kwenye makao makuu ya umoja huo alipokuwa akikutana na waandishi wa habari.
Wewe muhurumie Samia na ccm yake.
Nato ni dunia nyingine haihitaji huruma yako ukiwa mlandege unavuta hewa chafu
 
Hakuna eneo hata moja kwenye ardhi ya Ukraine ambayo urusi wamechukua na kuwa comfortable kufanya shughuli za kichumi ni propaganda ya hali ya juu umelishwa, miji waliyotangaza urusi kuchukua ni partially hayako full controlled na urusi vita inaendelea ingawa ni kweli Urusi alikuwa na mpango wakupora hayo maeneo kujimilikisha rasilimali lakini kilichomkuta hakutegemea ndio maana hadi mwaka umeisha bado anapeleka makundi haya na haya kwenye vita wanajeshi wake wanaambulia kufa tu.

Vita alii miscalculate vibaya na sasa anakumbana na changamoto ambazo Urusi kurudi kiuchumi ni ndoto, raia wake wanahama nchi maisha yamekuwa magumu urusi na juzi ametunga sheria kuwazuia raia wake wasiondoke au atawalipisha kodi mara 2 lakini wimbi ni kubwa hata urusi sasa wanaishi kwa khofu.

Marekani wanataifisha hela za matajiri wa kirusi walizoekeza Ulaya na Marekani kuzitoa msaada Ukraine zikiwemo hela za mtoto wa Putin ni vile Putin vita inamugharimu yeye peke yake sasa amekodi silaha kutoka Iran kila ndege na droon inayoangushwa inasoma toka Iran, putin amebakiwa na nuclear ambayo sasa hataweza kutumia alitishia vya kutosha lakini akachemsha watu wanasonga mbele
bado hujaamka tu!!!
 
Back
Top Bottom