NATO wasema wanafukuzana na wakati kuiwahi Urusi

Hakuna kitu ambacho mrusi hakukijua toka mwanzoni,,,, wamagharibi michezo yao ni ileile hawana mbinu mbadala na mrusi alishajua akishawagusa ukraine nini kinafata,,,,,,hii vita anaitumia kuipa nguvu brics na kuionyesha dunia maisha bila wamagharibi yanawezekana.............hao wamekumbatia madola ambayo kwenye mtikisiko wa uchumi ujao hayatasaidia kitu, huku mrusi anajikusanyia rasilimali na akibeba hilo eneo la ukraine atajiongezea utajiri mkubwa kuliko hivyo vidola walivyovifungia mabepari, maana maeneo anayoyataka mrusi nchini ukraine kiuchumi yana umuhimu mkubwa,,,,,,vita itaisha kwa mrusi kuimega ukraine na kule kiev kuweka kibaraka wake........yule mfungwa ambae ndo alikua kiongozi mkuu wa upinzani nchini ukraine anaweza akapewa nchi na mrusi,,,,,jamaa wana hesabu ndefu.......hawezi kuomba raia 1 tu kwa wanajeshi kibao wa ukraine huku akiwaacha wanajeshi wake mateka halafu amchukue raia mmoja tu wa ukraine......................
 
Na yalivyo wazi yanamwaga ule ugali uliharbika sababu ya spiringi za mlango taka kuwa legevu.
 
Tatizo USA na NATO hawakujua strategy ya Russia. Mpango mkubwa wa Russia ni kuchukua nuclear plant kubwa kuliko zote in Europe na maeneo muhimu kijeshi na kiuchumu na amefanikiwa kwa 100%.

Ile ya kujifanya anataka kuichukua kyiv ni war plan ya kuwazuga. Hayo maeneo aliyoyachukua plus nuclear plant ni kujiakikishia usalama wake kwa asilimia kubwa sana.

My friend USA, NATO na Zelensky wameshapotea vibaya sana na wanachoendela kufanya ni kuiteketeza Ukraine kabisa
 
Huruma gani kwa kauli hizo??
Anaetia huruma ni puti aliye piga mkwala mandonga eti atakae msaidia Ukraine naye atachukua kichapo!
Leo wanao msaidia Ukraine wanajidhihirisha bila hofu mchana kweupe ww unasema wanatia huruma [emoji15][emoji12]
Uko sawa kweli ww?!
 
Puti alibugi alipo linganisha uvamizi wake kule Chechinya ambao hawakuwa na silaha nzito zaidi ya rpg na jihadi ya kujitoa muhanga, hawakusaidiwa na Taifa lolote mjomba! lakini mrusi alionja joto la jiwe!
Sasa Ajìangalie mbinu ile aliyoitumia Chechinya itamgharimu kule Ukreine ambako wana Mjomba na silaha nzito!
Mwaka sasa unaisha![emoji15]
 
Umeongelea upande mmoja🤣🤣🤣 Marekani naye alipoingia kibubusa hapo chechnya nini kilimpata??
 
Vita ilishaisha kitambo sana. Kilichobaki saa hizi ni zelensky kutaka kurudisha maeneo yaliyotwaliwa na mrusi huku NATO wakimwangalia tu bila msaada wa maana. Ukraine wanataka msaada wa ndege hasa F16(Falcon Fighters), NATO wanaogopa kumpa zelensky ndege hizi sababu wanajua fika Ukraine wataanza kuzitumia Kwa kushambulia maeneo ya ndani kabisa ya Urusi. NATO wanaogopa majibu ya Urusi baada ya kuona anaanza kushambuliwa barazani, na Kwa upande wa Putin atakuwa na vitu viwili, siraha za nuclear na kupoteza vita. Maexpert wa NATO wamefanya calculations na kung'amua kuwa raisi Putin atachagua kutumia siraha za nuclear na siyo kushindwa vita,. Vilevile wanahisi Urusi ataanza kuongeza eneo la vita hasa kwenye mataifa yaliyotoa hizo ndege.. Marekani na mabest wake siyo mafala
 
Wakati sisi tumelala na tunafuatilia propaganda za NATO huko Urusi walikoteka wameshabadili kila kitu na hata wananchi waliokuwa waukraine wamekubali. Mji kama Mariupol na Severodonest hata kuitaja tena Zelensky hawezi.Barabara na madaraja yamejengwa na watu wametulia hawana habari na Ukraine.
 
Malizia na kile kinu cha nyuklia kinacho zalisha umeme (kinaiywa "zaporoshie") ambacho urusi ameruka nacho juu juu sasa kimeunganishwa na grid ya taifa ya urusi!
 
Aiseee, pole sana kijana.

Unajua Kyiv Russia alipoteza askari wangapi? Alipoteza silaha ngapi pale Kyiv? Mwezi mpaka March 2022 Russia alipoteza askari zaidi ya 1,500 kwa mujubu wa Putin ktk ile speech yake ya mwezi March.

Zaidi ya askari 1,000 inasemekana walipotea ktk ile battle ya Kyiv. Kumbuka ni msafara uliokuwa wa 64km ukisheheni silaha za maangamizi kutoka Russia, msafara ukilindwa na air defences bora zaidi za s300 n.k

Hizi drones za Byaktar, Javeline the Don na Stinger si mchezo mzee. Russia walikimbia kwa miguu kwa kuacha silaha zao Kyiv.
 
mpaka kufika machi mwishoni, 2022 jeshi la ukraine lilikuwa imevurugwa kwa 95%. Walikuwa hawana tena nguvu. Ndio misaada ikaanza. Ukraine kwa sasa nusu wa wapiganaji wake ni mamluki toka nchi mbalimbali.
 
Watu wanachukulia CIA ni kama TISS.

NATO walisema mapema kabisa toka vita vinaanza kuwa wanahitaji kuona hii vita ikichukua muda mrefu zaidi. Na wakaitengea hii vita bajeti ya miaka mitano, wote tulioona NATO ni kama imewehuka, tuliamini vita haiwezi kumaliza mwezi. Lakini leo tunazungumzia mwaka.

Russia ataendelea kuchukua maeneo ya Ukraine ila hatochukua kwa kasi kubwa sana, watachukua sababu NATO wanataka vita vichukue muda mrefu zaidi, sasa itachukuaje muda mrefu endapo hakuna maeneo ya kupiganiwa? Ni lazima russia amege sehemu kisha ipambaniwe hiyo sehemu.

Kadri siku zinavyozidi kwenda, NATO wanaonesha kuikabili vyema Russia kijeshi, kiuchumi, kidiplomasia walishammaliza mpaka sasa.
 
Hiyo miji itakuja kutapikwa tu, mbona Kharkiv ilikamatwa na ikaachiwa? Mboja Kherson zilipandishwa bendera za Russia na mpaka sasa zmedondoshwa. Hii vita itakuja kuisha vibaya kwa upande wa Ukraine na Russia, Ukraine ina nafasi kubwa ya kujengwa vizuri huko mbeleni.
 
Angekuwa hana Jeshi angeendelea kuteka miji kila kukicha? Please use your common sense mkuu!!
 
mpaka kufika machi mwishoni, 2022 jeshi la ukraine lilikuwa imevurugwa kwa 95%. Walikuwa hawana tena nguvu. Ndio misaada ikaanza. Ukraine kwa sasa nusu wa wapiganaji wake ni mamluki toka nchi mbalimbali.
Hizi silaha zote zinazopelekwa Ukraine zimeonesha matokeo chanya, na hiki ndicho kinaipa Ukraine matumaini.

1. Javeline, mpaka sasa tunaona idadi ya vifaru kutembea ktk hii vita imepungua kwa zaidi ya asilimia 90, Russia haingizi vifaru kizembe, hata vile vifaru vyake bora zaidi ameogopa kuviingiza Ukraine sababu ya Javeline.

2. Stinger, hakuja uchafu wa helkota yeyote ya Russia wala jets zinazopasua anga la Ukraine.

3. HIMARS, huyu ndo mnyama, mnyama haswa. Amebadili upepo mzima wa vita. Huyu ndo amemwaga roho za warusi kama uchafu. Zipo zaidi ya 30 hapo Ukraine na hakuna mpaka sasa hata moja iliyoangushwa.

Sasa fikiria NATO ikapeleka ndege, launchers zingine hapo Ukraine. Au tufanye zinaingizwa HIMARS za long range, HIMARA ziwe 200 hapo Ukraine, watu watapoteana.

Russia amebaki kupiga mabomu akiwa kwake tu, kisha ndo apeleke watu, ile approach ya kwanza ya kupeleka watu na vifaa ameshafeli vibaya sana.
 
Angekuwa hana Jeshi angeendelea kuteka miji kila kukicha? Please use your common sense mkuu!!
Njia alokuwa akiitumia mwanzo kwa sasa haipo tena. Russia ni anapga akitokea mbali, na hii imeonesha namna gani Ukraine ameimprove ktk mapambano.

Kasi ya Russia kuteka miji imepungua kwa zaidi ya asilimia 80, unless uwe haufatilii hii vita kwa undani zaidi.
 
Mkuu upo vitani Ukrean nini??
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…