NATO wasema wanafukuzana na wakati kuiwahi Urusi

Angekuwa hana Jeshi angeendelea kuteka miji kila kukicha? Please use your common sense mkuu!!
Wewe mpaka leo hujajua Ukraine wanavyoitesa urusi? ukraine wana tabia ya kuwaacha urusi waingie katika miji halafu wanawazunguka na kuwarambisha mchanga., tokea vita imeanza habari ni hii wanayokumbana nayo russia, unaeza ona kijii kimetekwa kumbe wanasubiriwa wajazane, ndio mana urusi wamepoteza wanajeshi wao kama kumbikumbi mtindo nu huo sasa wanakodi makundi ya kigaidi wagner group, russia hana tena jeshi
 
Haya yako ya mwisho inaogopesha sana..
 
Sasa wanatuma silaha kumsaidia kama nani pia sialisha peleka maombi ya kujiunga huko wamkubalie fasta wapate sababu mashoga hao
Kujiunga NATO siyo kama kujiunga CCM kwamba unaomba leo jioni unapewa alafu hata akipewa uanachama leo hawezi kuanza kusaidiwa kama member maana mpaka ipite miaka 2 tangu umejiunga ndo ibara ya 5 itaanza kufanya kazi.

Mwisho nimesema umoja wa NATO haujamsaidia kitu Ukraine wala hauwezi kujivika uhusika wa kumsaidia bali ataendelea kusaidiwa na washirika mbalimbali individually haswa wale wanaomwona Russia kama adui na ambao wanajiona wako atarini kumegwa kama inavyotaka kutokea kwa Ukraine, mfano Poland.
 
Msaada anopata zaidi ni vifaru na magari, vita ya Karne hii inapigwa angani
 
NATO hawafanyi tena kitu.Wameamua kumuwacha Zelensky ateketee na vita alivyovianzisha. Fikiria wote wameshasema wanaunga mkono lakini ndege anazotaka hawatampatia.Na vifaru vya leopard wale waliosema watampatia mmoja mmoja anabadili maamuzi. kwa kujua muelekeo wa vita kusaidia chochote ni hasara tu.
 
Malizia na kile kinu cha nyuklia kinacho zalisha umeme (kinaiywa "zaporoshie") ambacho urusi ameruka nacho juu juu sasa kimeunganishwa na grid ya taifa ya urusi!
waUikrane wakaanza kuuziwa umeme na Putin ilihali kinu ni chao,,tena na bei akapanga putini.

Hii SMO Kama maigizo flani[emoji15][emoji15][emoji15]
 
Russia is closing in pale Bakhmut.

Vyombo vya habari vya magharibi haviwezi kusema haya.

Ukraine yajiandaa kujibu mapigo mwezi ujao baada ya kupokea shehena ya silaha jambo ambalo linawafanya wapoteze uwezo huo.
Habari kuu hapo juu inaonesha ugumu kwa Ukraine kwamba hizo silaha zaidi ni ahadi wakati mrusi ndio anasonga mbele.Mataifa yote ya NATO yanalalamika kupungukiwa na silaha baada ya kuzipeleka Ukraine na nyingi zimeangamia bila kutoa matokeo mazuri. Utengenezaji wa hizo silaha upya wataalamu wa kijeshi wanasema hauwezi kufanyika kwa haraka hasa kutokana na kuporomoka kwa uchumi na hatua za kiufundi za utengenezaji ambazo huwa hazihitaji pupa.
Nchi kama Uiengereza inasemekana ndio iko hoi zaidi.
 
Maeneo anayotaka kashachukua unataka ateke nn tena
 
Ona hiyo misaada[emoji15][emoji15][emoji15]
 
Binafsi naona kushindwa vita kwa US/NATO hakutoshi - kumaliza ujeuri na upenda penda vita wa genge hili ovu ni vema Urusi kuiteka Ukraine nzima nzima ikaungana na Russian Federation na kuwa taifa moja,Urusi ikikosea kutekeleza jambo hilo nyeti basi wakumbuke kwamba USA itabuni plan "B" ya ku-destroy Russia in totality ie militarily and economically.

Lakini Urusi ikisha nyakuwa Ukraine basi hiyo itaifanya USA ipate wakati mgumu wa kuanzisha tena vitimbi vyake dhidi ya Russia kwa kuwatumia Ukraine na Poland kwenye proxy wars zake - who knows wanaweza kujitokeza ma Jenerali wenye traits za kamikaze ambao wanaweza kujaribu kuishambulia Urusi kwa silaha za Nuclear - Majenerali wendawazimu wa type kama hiyo wapo sana kwenye jeshi la Merikani ambao wanaichukulia Urusi/Putin poa kabisa!!
 
Kama Ukraine isiyokuwa na jeshi la maana, isiyojitosheleza kwa silaha mpaka isaidiwe ndo inamsumbua hivi Russia takriban mwaka sasa, hakika NATO inaweza ikamburuza Russia itakavyo. Jambo pekee linalohofiwa hapo ni silaha za Nuclear.
Kila siku naku hoji, hivi: Jeshi la Amerika liliwachukua muda gani kupigana na walima mpunga na wavaa sandals zilizo tengenezwa kutokana na mabaki ya matairi ya magari na matairi ya B-52 zilizo tunguliwa na hao hao WavietCong.

Jeshi la Amerika walipigana na wanamgambo hao kwa miaka 10 (kumi) na USA military walishindwa vibaya sana na kuabika kimataifa - angalia video clips zinazo onyesha WavietCong wakikaribia kuuteka mji wa Saigon in 1975 zipo kwenye search engines zote za mtandaoni - video zinaonyesha USA troops pamoja na majenerali wao cutting and running like mad with their tails between their legs, yaani unaona wazi wazi kwamba gallant VietCong troops were scaring a living daylights out of US five star Generals in VietNam never mind other ranks.

Nchi ndogo kabisa ya Yugoslavia iliwachukuwa NATO/USA miezi karibu minne kuishinda na hapo USA kama kawaida yake katumia mbinu zake za kikatiri "shock and awe" carpet bombing taifa dogo mabom mfururulizo bila huruma, wakaenda mbali na kutumia depleted Uranium kulipua Main battle TANKs huku USA ikijuwa wazi wazi kwamba mabom hayo ni hatari yana sambaza vumbi la mionzi ya Uranium hewani na aridhini na kudhuru raia/watu kiafya kwa miaka nenda rudi, nenda Serbia na Iraq utashuhudia watoto wanazaliwa vilema na watu wazima wanakufa kutokana na ugonjwa wa kansa unao sababishwa na vumbi la mlipuko wa ammutions tajwa hapo juu na USA wala hawajali na sijawahi kusikia UN au taifa lolote likipendekeza kuwaburuza mahakamani ma Rais Clinton na Bush kujibu war crime committed in Yugoslavia na Iraq kwa kutumia WMD (depleted Uranium) hipo kwenye kundi hilo.

Now back to the main point, nyinyi mnatujia hapa kila siku na stori za kushangaza eti "mbona inawachukuwa muda mrefu jeshi la Urusi kushinda vita in Ukraine" conveniently avoiding to mention muda Merikani iliyo upoteza ikipigana vita huko VietNam na kwingineko.

Tukiachana na aibu ya USA in VietNam fiasco, je, hawa NATO na USA wanao jifanya vifaru wa kutuniana misuri na Putin, mbona juzi juzi hapa walivurumishwa mkuku kutoka huko Afghanistan na wajukuu wa Mulla Omari baada ya USA Military kupoteza 20 years chasing shadows ie what did they achieve at the end of the day, nothing - need I say more??
 
We uko dunia gani man .ebu fanya uchunguzi bila kueka mapenz upande mmoja .utaona ukweli .Kama suala la urusi kuishiwa wanajeshi huo Ni utoto usiongee mbele za watu wazima utaonekana punguani
 
We uko dunia gani man .ebu fanya uchunguzi bila kueka mapenz upande mmoja .utaona ukweli .Kama suala la urusi kuishiwa wanajeshi huo Ni utoto usiongee mbele za watu wazima utaonekana punguani
Namaanisha majeshi aliyoplan kuivamia Ukraine na kuibuka mshindi yameshindwa na kuuliwa jeshi alilonalo ni la kulinda Urusi kama nchi ndio maana anakodi hayo makundi, alichagua vita lakini hana jeshi kwa lugha nyepesi
 
Kama Ukraine isiyokuwa na jeshi la maana, isiyojitosheleza kwa silaha mpaka isaidiwe ndo inamsumbua hivi Russia takriban mwaka sasa, hakika NATO inaweza ikamburuza Russia itakavyo. Jambo pekee linalohofiwa hapo ni silaha za Nuclear.
Russia nu weak na ndio maana hadi leo kashindwa fika Kyiv kabaki kulipua majengo tu.
 
Namaanisha majeshi aliyoplan kuivamia Ukraine na kuibuka mshindi yameshindwa na kuuliwa jeshi alilonalo ni la kulinda Urusi kama nchi ndio maana anakodi hayo makundi, alichagua vita lakini hana jeshi kwa lugha nyepesi
Tarehe 24/02 hadi April elites na wazoefu wengi waliuawa.

Na ndio maana hadi sasa Urusi kashindwa fika Kyiv.
Mwanzoni alifika mapema sababu alifanya surprise Ukraine ikaretreat, wengine wakakimbia
 
Ukreini itatema bungo
 
Kila mtu anasema lake

Tukisema wote mnaleta propaganda hapa nitakua nimekosea
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…