Kwa wewe ambaye unahitaji kuchukuliwa transcript NACTEVET unatakiwa uandike barua ya utambulisho wa anayekuchukulia ikiwa na anwani yako na anwani ya NACTEVET,ikiwa na taarifa kama namba yake ya kitambulisho cha taifa,sababu ya wewe kuagiza kuchukuliwe na kiambatanisho kama kitambulisho chako cha taifa,kama huna hicho kitambulisho unaweza kuambatanisha kopi ya cheti cha kidato cha nne,na mwishoni uji-commit kua NACTEVET haitahusika na upotevu utakaowezakutokea wa transcript husika.
Karibu uhudumiwe kama wenzako,huna sababu ya kusafiri kwa jambo lisilokulazimu wewe kutumia gharama nyingi.
Endelea kufanya kazi kwa maendeleo yako na taifa.