Mkuu awa;li ya Yote pole na Nakupa hongera sana kwa Ujasiri ulioufanya hasa kwa kuwa Mkweli na Muwazi na hata kudhirisha kuwa wewe Una Muheshimu Mke wako.
Awali ya yote hiyo imekuwa Mbinu Kuu siku hizi ya wadada au wanawake kujitongozesha na unapokataa huja na Gia hiyo ya kusema Mimi nitaonekanaje kama Mwanamke kukwambia hisia yangu kwako halafu unanikatalia. Wanaume wengi huanguka sana Wakisikia Kauli hiyo. Huingiwa na Huruma na mwisho wa siku Huingia huo Mtego na Mwishowe hufanya lile tendo kwa kisingizo kuwa ni Siri.... Mimi ni Mhanga wa Kutongozwa tena Sana na hizo ndiyo zimekuwa kauli zao....
Mkuu kwenye Hiyo Mbinu kwa huyo Mpangaji wako Kuna Yafuatayo ambayo unatakiwa Kuyaangalia.
- Kwa haraka Haraka Unaweza hisi kuwa Mke wako Anakujaribu Uaminifu wako Kupitia Changamoto hiyo ya huyo Mpangaji,.. Hii Itategemeana na mazoea waliyo nayo.
- Au, Mke wako hana mahusiano Mazuri na Huyo Mpangaji sasa anataka kumuonyesha kuwa anaweza Kumchukua Mume wake na baada ya kufanikisha utaone Kitakacho Tokea.
- Au Huyo Mpangaji amejiona mjinga kama uliishi Pale kabla ya Kuoa na umekuja Kuoa mwanamke mwingine ilihali yeye yupo Pale na ana Vigezo Vyote.
- Au Kweli alikukuwa anakuhitaji ila hukuonyesha initiative ya kumuapproach hivyo ameamua kuwa mkweli na inaweza kuwa ndivyo ilivyo.
Mkuu nina Imani kuwa katika hayo hapo Juu huyo Mpangaji wako ataangukia kwenye mojawapo.
Suluhisho,
- Usimwambie Mke wako Lolote linaoendelea na Usithubutu hata Siku Moja na Pindi Ukifanya hivyo Basi tarajia Ndoa yako Kuingiwa na Mgogoro Mkubwa kwa sabab umeitikia vikao zaidi ya Viwili bila kumhusisha Mkeo, sasa Ukimhusisha sasa hivi itakuletea matatizo Makubwa.
- Tafuta Nyumba Nyingine na Uhame hapo Mara Moja kama haupo Tayari kutimiza Matakwa ya huyo Mpangaji.
Ngoja niishie hapo kwanza nitarudi baadae