Vishu Mtata
JF-Expert Member
- Dec 15, 2019
- 15,954
- 35,415
Binafsi niko na TL, huyo FAM ni wazi ni pandikizi. Moves zake zinadhihirisha hilo.
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
wengine huu mwaka wa14 tangu tuachanae na ujinga wa namna hii nilimpigia slaa kura yangu ilipoibwa na jk basi nikaona haina maana kabisa na kupiga kuraLissu akishindwa tarehe 21 january najiondoa kwenye siasa kabisa sitashiriki siasa Tena katika maisha yangu
Sio lazima Tundu Lisu ashinde, cha muhimu ni uchaguzi wa haki. Na hata kama Tundu Lisu atashindwa bado mageuzi aliyoahidi yatatokea ndani ya cdm. Ntobi ametukana na ameomba msamaha. Hiyo ndio demokrasia.Unafikiri TL anaweza kushinda Ikiwa Uongozi karibu wote ni Machawa wa Mwenyekiti?
UMeona Jinsi wanavyoporomosha Maneno ya Kashfa Mtandaoni?
NIkuulize kama NTOBI angemtukana Mwenyekiti angeendelea Kuwa Kiongozi Mwandamizi wa Mkoa?
Hujazipata hadi sasa?Kama FAM atakua mwenyekiti wa CDM tena, acha nitafute fursa CCM tu.
Ntobi Msamaha wake ni Wa Kinafiki maana Bado ameendelea Kutoa Kashafa Baada ya Hapo soma Post zake za janaSio lazima Tundu Lisu ashinde, cha muhimu ni uchaguzi wa haki. Na hata kama Tundu Lisu atashindwa bado mageuzi aliyoahidi yatatokea ndani ya cdm. Ntobi ametukana na ameomba msamaha. Hiyo ndio demokrasia.
CCM DAIMADemokrasia Imevuliwa Nguo, sura Mpya ya CHADEMA inaanika Changamoto kubwa Iliyokuwa ikifichwa na wengi ya Uongozi wa Milele imebaki wazi na Kuonekana..
Kilichotokea leo, pale FAM alipotangaza kugombea tena nafasi ya uenyekiti wa CHADEMA, kimeacha alama ya fedheha kwa yeyote anayependa siasa za uwazi na demokrasia. Hatua hii imefungua pazia na kufichua uchi wa demokrasia ndani ya chama kinachojinasibu kupigania misingi ya haki na usawa.
Wengi walitarajia kwamba kwa ustaarabu wa hali ya juu, FAM angeamua kumuunga mkono TAL na hivyo kuondoa makandokando yanayoweza kugawa chama na kudhoofisha msingi wa demokrasia. Badala yake, hatua yake imeonyesha wazi kwamba anadhamiria kuendelea kutawala chama hicho ambacho amekiongoza kwa zaidi ya miongo miwili, Pasina Kuonyesha matunda yoyote jambo ambalo linaweza kuligharimu CHADEMA nafasi yake kama mbadala wa kweli wa CCM.
Tukumbuke kauli ya Barack Obama:
“A nation that wants to be strong in the future cannot have leaders who cling to power.”
"Taifa linalotaka kuwa na nguvu siku za usoni haliwezi kuwa na viongozi wanaoshikilia madaraka kwa nguvu."
CHADEMA sasa inakabiliwa na changamoto ya kupoteza uhalali wa kuwa chama cha demokrasia. Mienendo kama hii, ambapo viongozi wanashikilia madaraka kwa muda mrefu, inakidhalilisha chama mbele ya wapenda mabadiliko. Haiwezekani eti taifa likakubali kuongozwa na kiongozi ambaye anaonyesha dalili za kupenda utawala wa kiimla.
Kwa sasa, ni dhahiri kwamba kama FAM atapata nafasi ya kuongoza nchi hii "Maana nasikia Pia Anataka Kugombea Urais mwakani" (jambo ambalo haliwezekani), utawala wake unaweza kuwa mbovu kuliko hata ule wa viongozi waliokumbwa na ukosoaji mkubwa kama Robert Mugabe, Yoweri Museveni, au Idi Amin.
Kama John Adams alivyoandika:
“Because power corrupts, society's demands for moral authority and character increase as the importance of the position increases.”
"Kwa sababu madaraka hupotosha, jamii huhitaji maadili na tabia bora zaidi kadri nafasi ya uongozi inavyokuwa muhimu."
Hili linadhihirika wazi kwa FAM, ambaye licha ya kuwa mkongwe katika siasa za CHADEMA, ameonyesha uwezo mdogo wa uongozi wenye hisia (emotional intelligence) na maono mapana kwa manufaa ya chama na taifa.
maana Kwa sasa Taifa na CHADEMA ilimuhitaji TAL kuliko FAM kwa 100%
TAL, anajulikana na ana ushawishi mkubwa na ujasiri wa kisiasa, alionekana kuwa chaguo sahihi la kuleta uhai mpya kwa CHADEMA. Hata hivyo, nafasi yake imezimwa mapema kutokana na tamaa ya FAM kushikilia madaraka. TAL angeweza kuleta matumaini mapya kwa wanachama na taifa kwa ujumla, lakini kwa hali ya sasa, matumaini hayo yanaonekana kufifia.
Kwa sasa, CHADEMA ni chama Chemye mfano mbaya zaidi wa siasa za vyama vya upinzani. Badala ya kuwa mbadala wa CCM, kinazidi kuonekana kama chama kinachokumbatia utawala wa kiimla. Nafuu Kidogo ACT Wazalendo, ambao pia nao wanahusishwa na serikali kwa sababu wana serikali ya mseto Zanzibar, Kiukweli Chadema wamepoteza nafasi ya kuwa mpinzani wa kweli.
Kwa hali ilivyo, sitaki tena kukiita Chama cha Demokrasia na Maendeleo. Kuanzia sasa, nitakiita Chama cha Kiimla na Maendeleo (CHAKIMA).
“Power tends to corrupt, and absolute power corrupts absolutely.”
"Madaraka huelekea kupotosha, na madaraka ya hali ya juu hupotosha kabisa." - Lord Acton
Kwa wapenda demokrasia wa kweli, huu ni wakati wa kutafakari mustakabali wa siasa za Tanzania na kuona ni wapi tunapokosea. Demokrasia si neno la kupamba hotuba; ni msimamo wa msingi unaohitaji vitendo, siyo ahadi tupu.
na wala sio Kuhonga watu wakulazimishe Ugombee Mitandaoni na Huku Ukijua wewe ndo unawashawishi kufanya hivyo..
#Mungu awabariki..
Nakuunga mkono mkuu, uwezekano wa Lisu kushinda ni haupo, jamaa amekamata mifumo yoteLissu akishindwa tarehe 21 january najiondoa kwenye siasa kabisa sitashiriki siasa Tena katika maisha yangu
Jamaa anafanya biashara ya siasa
Pamoja na maovu ya CCM lakini wanabadilishana madaraka angalau unaona ladha tofauti kidogo, hii ya ndugu yangu Mbowe hapana hapana hapanaForm Moja ya Uenyekiti Wa CCM ni tofauti kabisa na Chadema..
CCM ni chama kilichopo Madarakani Na ili Uongozi uende sawa Hakuwzi kuwa na Mwenyekiti Tofauti na Rais so By Default mwenyekiti wa CCM huwa ni Lazima awe Rais wa Jamhuri ili apate Power ya Kuongoza Chama na Serkali..
Kwa CDM hii hapana hii ni mali binafsi ya MboweKwa taarifa yako pamoja na Mbowe kuzingua, wangalau sasa tunaona demokrasia ya kweli ya ushindani ndani ya cdm kuliko ya kile chama cha fomu moja. Tunaomba uandaliwe mdahalo wa wazi kati ya wagombea wa cdm ili tuone mipango ya hao wagombea. Maana kwa sasa ushindani wa kisiasa umeshaharibiwa na ccm, uchaguzi wa cdm ndio umebaki pekee wenye sura ya demokrasia.
Hapo umechemka mkuu hivi kama wewe unashambuliwa na msaidizi wako WA kazi then umuunge mkono!???Demokrasia Imevuliwa Nguo, sura Mpya ya CHADEMA inaanika Changamoto kubwa Iliyokuwa ikifichwa na wengi ya Uongozi wa Milele imebaki wazi na Kuonekana..
Kilichotokea leo, pale FAM alipotangaza kugombea tena nafasi ya uenyekiti wa CHADEMA, kimeacha alama ya fedheha kwa yeyote anayependa siasa za uwazi na demokrasia. Hatua hii imefungua pazia na kufichua uchi wa demokrasia ndani ya chama kinachojinasibu kupigania misingi ya haki na usawa.
Wengi walitarajia kwamba kwa ustaarabu wa hali ya juu, FAM angeamua kumuunga mkono TAL na hivyo kuondoa makandokando yanayoweza kugawa chama na kudhoofisha msingi wa demokrasia. Badala yake, hatua yake imeonyesha wazi kwamba anadhamiria kuendelea kutawala chama hicho ambacho amekiongoza kwa zaidi ya miongo miwili, Pasina Kuonyesha matunda yoyote jambo ambalo linaweza kuligharimu CHADEMA nafasi yake kama mbadala wa kweli wa CCM.
Tukumbuke kauli ya Barack Obama:
“A nation that wants to be strong in the future cannot have leaders who cling to power.”
"Taifa linalotaka kuwa na nguvu siku za usoni haliwezi kuwa na viongozi wanaoshikilia madaraka kwa nguvu."
CHADEMA sasa inakabiliwa na changamoto ya kupoteza uhalali wa kuwa chama cha demokrasia. Mienendo kama hii, ambapo viongozi wanashikilia madaraka kwa muda mrefu, inakidhalilisha chama mbele ya wapenda mabadiliko. Haiwezekani eti taifa likakubali kuongozwa na kiongozi ambaye anaonyesha dalili za kupenda utawala wa kiimla.
Kwa sasa, ni dhahiri kwamba kama FAM atapata nafasi ya kuongoza nchi hii "Maana nasikia Pia Anataka Kugombea Urais mwakani" (jambo ambalo haliwezekani), utawala wake unaweza kuwa mbovu kuliko hata ule wa viongozi waliokumbwa na ukosoaji mkubwa kama Robert Mugabe, Yoweri Museveni, au Idi Amin.
Kama John Adams alivyoandika:
“Because power corrupts, society's demands for moral authority and character increase as the importance of the position increases.”
"Kwa sababu madaraka hupotosha, jamii huhitaji maadili na tabia bora zaidi kadri nafasi ya uongozi inavyokuwa muhimu."
Hili linadhihirika wazi kwa FAM, ambaye licha ya kuwa mkongwe katika siasa za CHADEMA, ameonyesha uwezo mdogo wa uongozi wenye hisia (emotional intelligence) na maono mapana kwa manufaa ya chama na taifa.
maana Kwa sasa Taifa na CHADEMA ilimuhitaji TAL kuliko FAM kwa 100%
TAL, anajulikana na ana ushawishi mkubwa na ujasiri wa kisiasa, alionekana kuwa chaguo sahihi la kuleta uhai mpya kwa CHADEMA. Hata hivyo, nafasi yake imezimwa mapema kutokana na tamaa ya FAM kushikilia madaraka. TAL angeweza kuleta matumaini mapya kwa wanachama na taifa kwa ujumla, lakini kwa hali ya sasa, matumaini hayo yanaonekana kufifia.
Kwa sasa, CHADEMA ni chama Chemye mfano mbaya zaidi wa siasa za vyama vya upinzani. Badala ya kuwa mbadala wa CCM, kinazidi kuonekana kama chama kinachokumbatia utawala wa kiimla. Nafuu Kidogo ACT Wazalendo, ambao pia nao wanahusishwa na serikali kwa sababu wana serikali ya mseto Zanzibar, Kiukweli Chadema wamepoteza nafasi ya kuwa mpinzani wa kweli.
Kwa hali ilivyo, sitaki tena kukiita Chama cha Demokrasia na Maendeleo. Kuanzia sasa, nitakiita Chama cha Kiimla na Maendeleo (CHAKIMA).
“Power tends to corrupt, and absolute power corrupts absolutely.”
"Madaraka huelekea kupotosha, na madaraka ya hali ya juu hupotosha kabisa." - Lord Acton
Kwa wapenda demokrasia wa kweli, huu ni wakati wa kutafakari mustakabali wa siasa za Tanzania na kuona ni wapi tunapokosea. Demokrasia si neno la kupamba hotuba; ni msimamo wa msingi unaohitaji vitendo, siyo ahadi tupu.
na wala sio Kuhonga watu wakulazimishe Ugombee Mitandaoni na Huku Ukijua wewe ndo unawashawishi kufanya hivyo..
#Mungu awabariki..
Lazma Uone Kuna Shida Haiwezekani Mtu mmoja akawa anashambuliwa na wote haoo..Hapo umechemka mkuu hivi kama wewe unashambuliwa na msaidizi wako WA kazi then umuunge mkono!???
Wacha Kura ipigwe na iwe wazi na haki.kwa mtazamo wangu kama TL akishinda chama kitapotea uongozi ni subira,hekima na busaraLazma Uone Kuna Shida Haiwezekani Mtu mmoja akawa anashambuliwa na wote haoo..
Kipindi. Ha Uchaguzi wa Mwenyekiti mwaka 2009 ilikuwa hivi hivi kwa chacha wangwe..
Mwaka 2012 Ilikuwa Hivi hivi kwa zitto kabwe Na Sasa Ni hivi hivi kwa Lissu..
NA mwaka 2013 na 2014 Kina Kitila Mkumbo et al ..
Hapana Mbowe ana tatizo tena Kubwa na watu walio karibu yake hawamuambii
Ulichoandika hakiendani na misingi ya demokrasia mfano chama cha ANC mwenyekiti anaweza kuwa mtu mwingine na Rais mwingineForm Moja ya Uenyekiti Wa CCM ni tofauti kabisa na Chadema..
CCM ni chama kilichopo Madarakani Na ili Uongozi uende sawa Hakuwzi kuwa na Mwenyekiti Tofauti na Rais so By Default mwenyekiti wa CCM huwa ni Lazima awe Rais wa Jamhuri ili apate Power ya Kuongoza Chama na Serkali..
Mtu kushinda changamoto unasema kuna tatizoLazma Uone Kuna Shida Haiwezekani Mtu mmoja akawa anashambuliwa na wote haoo..