NATUBU: Kama Niliwahi Kukitukana Chama Changu cha CCM kuhusu kuwa na misingi Mibovu ya Kidemokrasia Naomba kwa Dhati kabisa Nisamehewe

Demokrasia Imevuliwa Nguo, sura Mpya ya CHADEMA inaanika Changamoto kubwa Iliyokuwa ikifichwa na wengi ya Uongozi wa Milele imebaki wazi na Kuonekana..

Kilichotokea leo, pale FAM alipotangaza kugombea tena nafasi ya uenyekiti wa CHADEMA, kimeacha alama ya fedheha kwa yeyote anayependa siasa za uwazi na demokrasia. Hatua hii imefungua pazia na kufichua uchi wa demokrasia ndani ya chama kinachojinasibu kupigania misingi ya haki na usawa.

Wengi walitarajia kwamba kwa ustaarabu wa hali ya juu, FAM angeamua kumuunga mkono TAL na hivyo kuondoa makandokando yanayoweza kugawa chama na kudhoofisha msingi wa demokrasia. Badala yake, hatua yake imeonyesha wazi kwamba anadhamiria kuendelea kutawala chama hicho ambacho amekiongoza kwa zaidi ya miongo miwili, Pasina Kuonyesha matunda yoyote jambo ambalo linaweza kuligharimu CHADEMA nafasi yake kama mbadala wa kweli wa CCM.

Tukumbuke kauli ya Barack Obama:

“A nation that wants to be strong in the future cannot have leaders who cling to power.”

"Taifa linalotaka kuwa na nguvu siku za usoni haliwezi kuwa na viongozi wanaoshikilia madaraka kwa nguvu."

CHADEMA sasa inakabiliwa na changamoto ya kupoteza uhalali wa kuwa chama cha demokrasia. Mienendo kama hii, ambapo viongozi wanashikilia madaraka kwa muda mrefu, inakidhalilisha chama mbele ya wapenda mabadiliko. Haiwezekani eti taifa likakubali kuongozwa na kiongozi ambaye anaonyesha dalili za kupenda utawala wa kiimla.

Kwa sasa, ni dhahiri kwamba kama FAM atapata nafasi ya kuongoza nchi hii "Maana nasikia Pia Anataka Kugombea Urais mwakani" (jambo ambalo haliwezekani), utawala wake unaweza kuwa mbovu kuliko hata ule wa viongozi waliokumbwa na ukosoaji mkubwa kama Robert Mugabe, Yoweri Museveni, au Idi Amin.

Kama John Adams alivyoandika:

“Because power corrupts, society's demands for moral authority and character increase as the importance of the position increases.”

"Kwa sababu madaraka hupotosha, jamii huhitaji maadili na tabia bora zaidi kadri nafasi ya uongozi inavyokuwa muhimu."

Hili linadhihirika wazi kwa FAM, ambaye licha ya kuwa mkongwe katika siasa za CHADEMA, ameonyesha uwezo mdogo wa uongozi wenye hisia (emotional intelligence) na maono mapana kwa manufaa ya chama na taifa.
maana Kwa sasa Taifa na CHADEMA ilimuhitaji TAL kuliko FAM kwa 100%

TAL, anajulikana na ana ushawishi mkubwa na ujasiri wa kisiasa, alionekana kuwa chaguo sahihi la kuleta uhai mpya kwa CHADEMA. Hata hivyo, nafasi yake imezimwa mapema kutokana na tamaa ya FAM kushikilia madaraka. TAL angeweza kuleta matumaini mapya kwa wanachama na taifa kwa ujumla, lakini kwa hali ya sasa, matumaini hayo yanaonekana kufifia.

Kwa sasa, CHADEMA ni chama Chemye mfano mbaya zaidi wa siasa za vyama vya upinzani. Badala ya kuwa mbadala wa CCM, kinazidi kuonekana kama chama kinachokumbatia utawala wa kiimla. Nafuu Kidogo ACT Wazalendo, ambao pia nao wanahusishwa na serikali kwa sababu wana serikali ya mseto Zanzibar, Kiukweli Chadema wamepoteza nafasi ya kuwa mpinzani wa kweli.

Kwa hali ilivyo, sitaki tena kukiita Chama cha Demokrasia na Maendeleo. Kuanzia sasa, nitakiita Chama cha Kiimla na Maendeleo (CHAKIMA).

“Power tends to corrupt, and absolute power corrupts absolutely.”

"Madaraka huelekea kupotosha, na madaraka ya hali ya juu hupotosha kabisa." - Lord Acton

Kwa wapenda demokrasia wa kweli, huu ni wakati wa kutafakari mustakabali wa siasa za Tanzania na kuona ni wapi tunapokosea. Demokrasia si neno la kupamba hotuba; ni msimamo wa msingi unaohitaji vitendo, siyo ahadi tupu.

na wala sio Kuhonga watu wakulazimishe Ugombee Mitandaoni na Huku Ukijua wewe ndo unawashawishi kufanya hivyo..

#Mungu awabariki..
Hameni kimya kimya,kwani mlipojiunga mlikuja hapa kututangazia?
😝😝
Siasa za kufuata mtu zitawaua nyie

Kapige kura wewe,kila dk mnafungua mada mpya
 
Mbowe amekubali kirahisi kukivuruga chama chake.
 
Wacha Kura ipigwe na iwe wazi na haki.kwa mtazamo wangu kama TL akishinda chama kitapotea uongozi ni subira,hekima na busara
Hapna Kabisa Bob Nyanga Makani Alikuwa Ni mtu dizaini ya Lisu na aliiongoza CHADEMA kama Mwenyekiti mpaka alipostaafu 2004 akachukua Lissu Mbona Chadema Ilikuwa Imara?

Ulikuwa na Miaka mingapi Kwenye Uongozi Wa Bob Nyanga?
 
Nimeanza kupiga Kura 1995 na nilikuwa naudhuria mikatano ya vyama mbalimbali.Wakati upinzani ulikuwa NCCR Mageuzi
 
Back
Top Bottom