Natubu: Nilikuwa simuelewi Mwamposa, ila kwa idadi ya viwete walioponyeshwa Songea naanza kumuamini

Natubu: Nilikuwa simuelewi Mwamposa, ila kwa idadi ya viwete walioponyeshwa Songea naanza kumuamini

Zingzingzing

JF-Expert Member
Joined
May 13, 2014
Posts
735
Reaction score
667
Kama kichwa cha habari hapo juu, ujio wa Mwamposa, Songea ni neema.

Umeleta uponyaji mkubwa sana, vilema wanatembea, vipofu wanaona, hiyo haina kupinga.

Mimi nilikuwa simuamini lakini kwasasa naanza kumuamini.

20221014_175248.jpg
 
Kwa yule ninaemjua ni mlemavu akipona nitajua ni kweli, sio hawa wa kuletwa. Jamaa alikuwa anawapa watu ndevu za ajabu, na kuwapa mafunzo maalumu ili washuhudie walikuwa misukule na wamefufuka. Ni maujanja tu ya kupiga pesa kimazingira.
 
Kama kichwa cha habar hapo juu, ujio wa mwamposa songea ni neema. ,umeleta uponyaji mkubwa sana, vilema wanatembea, vipofu wanaona, hiyo haina kupinga. Mimi nilikuwa simuamini lakini kwasasa naanza kumuamini, .
Daaah ndugu yangu, Elimika ndugu hao ni Usanii unafanyika hapo au labda nikuambie ukweli hayo ni maigizo tu hayana uhalisia wowote ndugu
 
Nitakuwa mtu wa mwisho kuamini hayo maigizo yenu.
yaani uwe kilema (mlemavu wa viungo), halafu from nowhere, utembee kwa sababu ya kuombewa na Mwamposa!!

Magongo yenyewe karibia yote yanaonekana kuwa ni mapya! Hakika hii nchi ina wajinga wengi kweli kweli. Wacha tu ccm iendlee kunufaika kupitia huu ujinga wa Watanzania walio wengi.
 
Back
Top Bottom