Natubu: Nilikuwa simuelewi Mwamposa, ila kwa idadi ya viwete walioponyeshwa Songea naanza kumuamini

😂😂😂haya ni mazingaumbwe brother. ndo maana hakuna neno linaloubiriwa bali ni usani sanii tu

Sema mnamwinua nyie. ndo maana mnampa utukufu hata Yesu mmeshasahau km anaexist hili la kumpa utukufu na yeye kujipa utukufu ni ishara kubwa si nabii wa kweli wa Mungu. anayestahili kutukuzwa kupewa sifa na utukufu ni Yesu si nabii yeyote yule. hata Yesu alivyokuwa duniani aliishi kwa unyenyekevu mkubwa na wakt mwngine alifanya miujiza alitaka watu walisifu jina la Mungu wasimuangalie yeye na ndio maana alidiriki kuwaambia wengine nendeni mkawaambie mataifa ukuu wa Mungu alikuwa soo hamble ila si haya makidai ya hawa manabii uchwara
 
bandiko la post limelenga kumuinua mwamposa ila si kumtukuza Mungu si shangai ndo maana hakuna sehemu ametajwa Mungu wala Yesu hata kwny matangazo mengine unakuta anasifiwa yeye tu.

Mungu akimuita mtu kuwa nabii ni lazima utukufu apewe Mungu. ila ukiona utukufu hapewi Mungu unajua kwa huyo nabii Mungu hayupo
 
Hayakuhusu

Amini unachoamini na mimi niachie ninachoamini

Katiba ya nchi imetoa uhuru wa kuabudu
Mtu anaruhusiwa kuabudu chochote hata mavi kama Mungu bila kuingiliwa uhuru wake na yeyote

Ndio maana Tanzania kuna waabudu mizimu,Wahindi waabudu ng'ombe nk na Serikali Haina shida nao sababu Serikali Haina dini

Hangaika na hicho kidini chako Sisi waumini wa Mwamposya kaa mbali na sisi
Kama ni shamba Kazana kulima shamba lako usiangalie na kukaa kupiga yowe mtu kwenye shamba lingine ohhh mjinga yule analimaje halimi vizuri!! Hali kwako,halali kwako pambana na shamba lako

Ni aibu mtoto wa kiume kuwa mumbeya kutwa kuongea habari za Majirani wawe jirani zako Mwamposya au yeyote

Acha umbeya mtoto wa kiume huna yako ya kufanya? Leave Mwamposya alone.

Tuachie waumini wake hopeless wewe
 
hahaha umeshindwa kujibu kuhusu kujipa utukufu nilikujua tuu hii spana huwez chomoka nayo. unaishia kutukana punguza jazba mzee njoo na fact twende na fact
 
Sasa unakufuru, unamwangalia Mungu au Mwamposa. Mwamposa ni tapeli tu mwenye kuhubiri utajirisho badala ya kuhubiri imani. Kama anajuwa sala na imani kupitia kwake vinaleta utajiri, kwa nini asiombe yeye akaupata kuliko kuweka tozo. Maana kila ombi lake lina tozo, utafikiri serkali ya SSH.
 
peleka ujinga Facebook kule wajinga ni wengi unaweza wahadaa kwa mafuta si hapa kwa magreat thinker
 
Yeye anatoa neno, anatoa uponyaji, hawez kubaki na karamu
 
Yeye anatoa neno, anatoa uponyaji, hawez kubaki na karamu
sasa si atoe buree maana biblia inasema toeni bure mmepata bure. km ameitwa na Mungu asiwadanganye kwa kuwaitisha pesa hivi wakina petro, paulo, fikipo waanzilishi wa kanisa la kwanza walikuwa wanafanya miujiza mingi ila walikuwa hawataki kupokea hela yoyote. leo hii nabii anaweka mpk hela ya kumuona dah😂😂😂
 
Yule mdada WAKONTA MAPUNDA kila siku wanampita kama hawamuoni, Namuomba mwamposa aende kumuombea yule dada kwa jina la yesu.
 
Ina maana wewe huna imani? Kama ungekuwa nayo ungekubali kuwa CHAWA wa Mwamposa? Mungu angekuteremshia utajiri, akuondolee udhia wa kuwa CHAWA wa Mwamposa. UCHAWA utakumaliza!
 
Mm sijamkufuru mungu Wala kumkumfuru roh mtakatifu Ni mtizamo wangu nimeutoa dhid yake kuwa

Kama Ni wa mungu tutajuwa na Kama Ni wa shetani pia itajulikan hapahapa duniaa
 
Hahaha yaani hata mimi nimeshangaa. Inakuwaje wote wawe na magongo mapya
 
Kama vile MPYA vile!! Zilitumika siku moja tu au !!!!????
Wenyeji wa huko ndio wanajua

Mikutano ya Mwamposya watu hujaa sababu sio ya shuhuda za radiioni au TV tu

Watu wanaopata ufumbuzi wa yanayowasibu huishi mitaani na watu wanawajua vizuri hali zao kabla na baada ya kwenda Kwa Mwamposya. Wanajua huyu kasaidika.Mwenye macho haambiwi tama.Ndicho kinampaisha Mwamposya.
 
Mkuu twende kwa fact, kama huna fact basi muamini mwamposa.
Mbona magongo ni mengi kuliko walemavu? Alafu, kwa nini kila mlemavu asishikilie gongo lake. Yaani hata ukiangalia nyuma hakuna wingi wa walemavu kulingana na magongo.FIGISU HIZO. CHAWA LETA LINGINE.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…