Natubu: Nilikuwa simuelewi Mwamposa, ila kwa idadi ya viwete walioponyeshwa Songea naanza kumuamini

Natubu: Nilikuwa simuelewi Mwamposa, ila kwa idadi ya viwete walioponyeshwa Songea naanza kumuamini

Uponyaji wa kiimani haendi kwa utaratibu unao taka wewe..wenye uhitaji walio naimani ndio wanaopata uponyaji.

Karibu kesho ukanyage mafuta dodoma.

#MaendeleoHayanaChama
wewe acha kutudanganya hapa
ina maana mtu ana matatizo mfano cancer ukimpiga neno kisha ukamponyesha si ndiyo imani yenyewe hiyooo?
kila kijiji hakikosi kuwa na walemavu na wagonjwa mbona wale mnaoponya mfano viwete wanatoka mbali?
yaani huyo mwamposa anatangazia dunia kwamba ana ponya ukimwi
uhuni tu
 
Injili haiwezi kwenda bila kuwezeshwa..unadhani ni rahisi sana kuendesha ministry kubwa kama hiyo ya mtume na Nabii Mwamposa??acha kujitoa akili kama wewe tu hapo kwako unahitaji pesa kuendesha familia iweje kwa ministri kama hiyo ya Mwamposa.

Acheni wivu wa kike.

#MaendeleoHayanaChama
haya bwana . ndiyo muwauzie maji, mafuta nk?
unalijua jumba la kakobe pale mbezi beach/kawe/rainbow?
unalijua hekalu la kakobe kule salasala kinzudi ?
 
wewe acha kutudanganya hapa
ina maana mtu ana matatizo mfano cancer ukimpiga neno kisha ukamponyesha si ndiyo imani yenyewe hiyooo?
kila kijiji hakikosi kuwa na walemavu na wagonjwa mbona wale mnaoponya mfano viwete wanatoka mbali?
yaani huyo mwamposa anatangazia dunia kwamba ana ponya ukimwi
uhuni tu
Wewe ambaye sio muhuni umewasaidia nini hao wahitaji na wenye matatizo.

Acha wivu wa kike...

acha kulia anza kuamini.

#MaendeleoHayanaChama
 
Wewe ambaye sio muhuni umewasaidia nini hao wahitaji na wenye matatizo.

Acha wivu wa kike...

acha kulia anza kuamini.

#MaendeleoHayanaChama
hahaha.
hnachekesha kweli wewe.... kuhoji jambo nako ni wivu wa kike? pole mm siyo mwanakondoo
 
Kama kakutuma Ili umpigie Promo hapa rudi Kwake kamwambie GENTAMYCINE namuuliza kama anatibu Vilema Wote mbona Mdogo wake wa Damu ( toka nitoke ) ana Ulemavu ila ameshindwa Kumponyesha?

Mpe pongezi zangu nyingi kwa Siku hizi kuwahama Wanaijeria na sasa Kutumia zaidi 'Ndumba' Kali kutoka Congo DR na Mozambique ambazo zinamsaidia Kuvutia Watu na Kuponya Watu Kiuchawi ( Kiunyangindo )

Mwambie kuwa haya huwa na mwisho.
Hakika Wema na Utukufu ni Wa Mwenyenzi Mungu Mtakatifu
 
haya bwana . ndiyo muwauzie maji, mafuta nk?
unalijua jumba la kakobe pale mbezi beach/kawe/rainbow?
unalijua hekalu la kakobe kule salasala kinzudi ?
Wabongo hamna dogo..angekua analeta umati mkubwa kama huo na akawa kapuku hohe hahe mgeanza maneno kumzodoa.

Akiwa na pesa mnaaza maneno

..uzuri hakuna anaueshikiwa bunduki kutoa sadaka ama kununu hayo maji na mafuta...wanatoa wao kwa hiyari yao wewe kinachokuuma nini.

Nakushauri get a job acha wivu wakike.
 
hahaha.
hnachekesha kweli wewe.... kuhoji jambo nako ni wivu wa kike? pole mm siyo mwanakondoo
Sawa kinachokuuma nini sasa..kuhoji wakati umejazwa maneno ya mitaani...kubali kubadilika wahafidhina huwa mnatabu sana.

Acha kulia anza kuamini.

#MaendeleoHayanaChama
 
Sawa kinachokuuma nini sasa..kuhoji wakati umejazwa maneno ya mitaani...kubali kubadilika wahafidhina huwa mnatabu sana.

Acha kulia anza kuamini.

#MaendeleoHayanaChama
kuhoji mambo sio uhafidhina mkuu. labda kama neno lenyewe limepata tafsir nyingine ya TUKI
 
kuhoji mambo sio uhafidhina mkuu. labda kama neno lenyewe limepata tafsir nyingine ya TUKI
Sawa ila ukitaka kuhoji jaribu kumsikiliza mahubiri yake sio kusikiliza story za mitaani.

#MaendeleoHayanaChama
 
Mambo ya imani ni magumu sana, sema imani na akili vinatakiwa viwe na uwiano 50%|50% ila imani ikizidi ndo tunapata mazombie/misukule inayomwabudu na kumwamini mtu.
 
Weka hapa majina ya watu watatu amabo walikuwa ni vipofu wakaponywa. Kata zao na vijiji wanavyotoka pia.
Kama kichwa cha habar hapo juu, ujio wa Mwamposa, Songea ni neema.

Umeleta uponyaji mkubwa sana, vilema wanatembea, vipofu wanaona, hiyo haina kupinga.

Mimi nilikuwa simuamini lakini kwasasa naanza kumuamini.

View attachment 2387081
 
Nani yuko tayari kuwa spie, tuprove miujiza ya mzee ni ya kweli au movie.
Script itakuwa hivi...hakikisha unaudhururia mikutano ya mzee na umepata picha na video za wanaodaiwa kupokea miujiza ya kuponywa sehemu za mwili zinazoonekana kama upofu, kiwete wa sehemu za viungo km miguuni na mikono.
Ukipata hzo picha na video, zoezi linalofuata ni kuwafuatilia waliopokea muujiza kwa kuspie, kuuliza majirani na wanaowafahamu ili wathitishe kama kweli walikuwa na huo ulemavu.

Ukifanikisha hilo, naamini una stori nzuri ya kupublish na ikapata followers wengi.

Uwe makini sana kwa sababu unagusa mfuko wa mtu hapo.
Ongezea maelezo mtu aingie kushoot 😂
 
Hata kipindi YESU KRISTO alipoishi kama mwanadamu walimuona waliishi nae lakini hawakuamini...

Ila mimi na nyumba yangu nitamwabudu YESU KRISTO milele
 
Hata kipindi YESU KRISTO alipoishi kama mwanadamu walimuona waliishi nae lakini hawakuamini...

Ila mimi na nyumba yangu nitamwabudu YESU KRISTO milele
Chagueni Leo mtayemtumikia, Lakini Mimi na nyumba yangu tutamtumikia Mungu.

Kumtegemea Mungu raha sana.
 
Kunakaribia kukucha mkuu shituka
Wwe si waende muhimbili kufanya maajabu

Mbugila mbugila ni chakula ya wajanja town hapa
 
Nitakuwa mtu wa mwisho kuamini hayo maigizo yenu.
yaani uwe kilema (mlemavu wa viungo), halafu from nowhere, utembee kwa sababu ya kuombewa na Mwamposa!!

Magongo yenyewe karibia yote yanaonekana kuwa ni mapya! Hakika hii nchi ina wajinga wengi kweli kweli. Wacha tu ccm iendlee kunufaika kupitia huu ujinga wa Watanzania walio wengi.
Ni vizuri ungetufahamisha mtu ajulikanaye mtaani kwako ambaye ameponywa.
 
Back
Top Bottom