Muislamu unaetaka kupangia wakristo namna ya kuabudu hii si futuhi
Muislamu hawezi nipangia jinsi/namna ya kuabudu
KAFARA YA YESU HAISAIDII CHOCHOTE
Wakristo wanaamini ya kwamba Adamu na Hawa walifanya dhambi kisha wazao wao wote wanarithi dhambi hiyo (dhambi ya asili).
Na Mwenyezi Mungu hawezi kuondoa adhabu ya dhambi ile bila kumwaga damu, na hakuna mtu yeyote anayeweza kuokoka bila ya kafara. Na anatolewa kafara ambaye hana dhambi yoyote. Na wakati wanadamu wote wanarithi dhambi hiyo, yeyote hawezi kutolewa kafara.
Kwa sababu hiyo Mwenyezi Mungu alimtoa Bwana Yesu Kristo atolewe sadaka na damu yake iwe kafara ya dhambi za watu wote.
Lengo la kutumwa kwa Yesu lilikuwa ni kuwaokoa wanadamu kwa kafara ya damu yake.
Katika kurasa zifuatazo nitachunguza na kuzipima hoja zote za Wakristo kuhusu kafara. Na itathibitika ya kwamba kafara ya Bwana Yesu haisaidii chochote.
(i) Mwenyezi Mungu ambaye ni Muumba wa ulimwengu aliye mwingi wa rehema na mwingi wa ukarimu hataki kafara ya watu kama alivyosema.
“Nataka rehema wala siyo sadaka.” (Mathayo 12:7).
Hiyo ni sababu wakati Nabii Musa alipotaka kujitoa kafara, Mwenyezi Mungu hakukubali mawazo yake.
Biblia inasema ya kuwa: “Asubuhi yake Musa akawaambia watu, mmetenda dhambi kuu. Sasa nitakwenda juu kwa Bwana, labda nitafanya upatanisho kwa ajili ya dhambi yenu. Musa akarejea kwa Bwana akasema: “Aa!! watu hawa wametenda dhambi kuu, wamejifanyia mungu wa dhahabu. Walakini sasa, ikiwa utawasamehe dhambi yao na kama sivyo unifute, nakusihi, katika kitabu chako ulichokiandika. Bwana akamwambia Musa, mtu yeyote aliyenitenda dhambi ndiye nitakayemfuta katika kitabu changu.” (Kutoka 32:30-33).
(ii) Ikiwa lengo lilikuwa ni kuwasamehe watu, basi watu walisamehewa kwa maombi ya Nabii Musa tu.
Wala haikuhitajika kumwagika damu ya mtu. Kama Nabii Musa mwenyewe alivyosema:
“Nikaanguka nchi mbele za Bwana siku arobaini usiku na mchana, kama pale kwanza; sikula chakula wala kunywa maji ; kwa sababu ya makosa yenu yote mliyokosa, kwa kufanya yaliyo maovu machoni pa Bwana, kwa kumkasirisha.
Kwa kuwa niliogopa hasira na makamio aliyowakasirikia Bwana kutaka kuwaangamiza. Lakini Bwana alinisikiza wakati huo nao. Bwana akamkasirikia sana Haruni akataka kumwangamiza; nikamwombea Harun naye wakati huo. (Kumbukumbu la Torati 9:18- 20).
Siyo hiyo tu, bali wapo watu kadhaa wale ambao hawana dhambi bila ya kumwagwa damu ya Yesu. Kwa mfano, katika Biblia imesemwa kuwa: “Melkizedeki hana baba, hana mama, bali amefananishwa na Mwana wa Mungu huyo adumu kuhani milele.” (Waebrania 7:3).
Melkizedeki aliumbwa bila ya wazazi wawili, na huyo hana dhambi aliyorithi toka kwa wazazi.
Vile vile Enoko alienda pamoja na Mungu. (Mwanzo 5:22).
Enoko akiwa pamoja na Mungu kwa kuwa hakuwa na dhambi, kwa maana mwenye dhambi hawezi kumkaribia Mungu.
Vile vile Biblia imesema kwamba Zakaria na mkewe Elizabeti hawakuwa na dhambi.
“Zamani za Herode, mfalme wa Uyahudi, palikuwa na kuhani mmoja jina lake Zakaria wa Zamu ya Abiya, na mkewe alikuwa mmoja wa uzao wa Haruni, jina lake Elizabeti na wote wawili walikuwa wenye haki mbele za Mungu wakiendelea katika amri zote za Bwana na maagizo yake bila lawama.” (Luka 1:5-6).
Kama hawa wazee wawili hawakuwa na dhambi ndivyo vivyo mtoto wao Yohana hakuwa na dhambi.
Imesemwa kuwa: “Sababu atakuwa mkuu mbele za Bwana hatakunywa divai wala kileo naye atajazwa roho mtakatifu hata tangu tumboni mwa mamaye.” (Luka 1:15).
Ikiwa watu wote hawa walikuwa wema na hawakuwa na dhambi yoyote, kabla ya damu ya Yesu, sifa hizo walizipata vipi?.
(iii) Bibla inapinga na kufutilia mbali mawazo ya kuwa mtu anaweza kubeba dhambi za mtu mwingine. Kama Mwenyezi Mungu alivyosema:
(A) “Mababa wasiuawe kwa ajili ya watoto wao, wala watoto wasiuawe kwa ajili ya baba zao. Kila mtu auawe kwa ajili ya dhambi yake mwenyewe.” (Kumb. 24:16).
(B) Lakini kila mtu aipime kazi yake mwenyewe, ndipo atakapokuwa na sababu ya kujisifu ndani ya nafsi yake tu, wala si ya mwenzake.” (Wagalatia 6:4).
Wakati mtu hawezi kubeba dhambi za mtu mwingine,Wachungaji wa leo wanahubiri kinyume na fundisho hili la Biblia kwa msingi gani?
(iv) Bwana Yesu hakujua lengo la kutumwa kwake kwamba ni kutolewa sadaka au kafara, kwa sababu hiyo alikuwa na hofu ya hali ya juu ya kuuwawa kwake.
Ndiyo maana alijificha kama isemavyo Biblia:
(A) “Basi tangu siku ile walifanya shauri ya kumuwa kwahiyo Yesu hakutembea tena kwa wazi mpaka mji uitwao
Eframu akakaa huko pamoja na wanafunzi wake.” (Yohana 11:53-54).
(B) Maadamu mnayo nuru iaminini nuru hiyo ili mpate kuwa wana wa nuru. Hayo aliyasema Yesu, akaenda zake, akajificha wasimwone.” (Yohana 12:36).
Mtu ambaye anasemekana kwamba alikuja kumwaga damu yake kwa ajili ya kuwaokoa watu kwa nini alijificha ficha?
Na wakati alipotakiwa kumwaga damu alipiga mayowe?
Kama tuirejeapo Biblia:
“Na kama saa tisa Yesu akapaza sauti yake kwa nguvu akisema “Eloi, Eloi lamasabaktani? Yaani Mungu wangu! Mungu wangu mbona umeniacha? (Mathayo 27:46).
Kama Yesu hakutaka kumwaga damu yake kwa hiyari yake, basi hii si sadaka wala kafara, bali ni kumshinikiza.
Vilevile kama mtu anamsaidia masikini kwa hiyari yake, hii inakuwa ni sadaka, na kama ataporwa na masikini
hiyo haitaitwa sadaka, bali hii itaitwa ni wizi au ujambazi.