Mussa Myahudi lakini ametoka katika kizazi cha Yaakubu na Yaakubu alizaliwa na baba yake anaitwa isaka na isaka baba yake ni Nabii ibrahimu. Na hivyo hivyo Mtume Muhammad Rehema za Mungu ziwe juu yake pamoja na mani kizazichake kimetoka kwa ismail mwana kuwachinjwa na Nabii ibrahimu . Kwa hiyo Nabii ibrahim alikuwa ni Muislam pamoja kizazi chake chote ni waislam Dini ya kiislam ameanzisha Nabii ibrahimu sio Mtume Muhammad alikuja kuiendeleza uarabuni tunawezakusema Mtume muhammad ndio aliye leta dini ya kiislam uarabuni lakini Mwanzilisha wadini ya kiislam alikuwa ni Nabii ibrahim . Na Nabii ibrahim alikuwa ni Baba a Mataifa yote ya wayahudi pamoja na waarabu enzi hizo. Usahahidi Nabii ibrahim ndio aliye anzisha Dini ya kiislam soma aya ya Qur'am Sura. 22 AYA YA 78.
78. Na fanyeni juhudi kwa ajili ya Mwenyezi Mungu kama inavyo stahiki jihadi yake. Yeye amekuteueni. Wala hakuweka juu yenu mambo mazito katika Dini. Nayo ni mila ya baba yenu Ibrahim. Yeye (Mwenyezi Mungu) alikuiteni Waislamu tangu zamani, na katika hii (Qur'ani) pia, ili awe Mtume shahidi juu yenu, na nyinyi muwe mashahidi kwa watu. Basi shikeni Sala na toeni Zaka na shikamaneni na Mwenyezi Mungu. Yeye ndiye Mlinzi wenu, Mlinzi bora kabisa, na Msaidizi bora kabisa
Tafsiri yake
*78. Na wanieni katika Jihadi ya kunyanyua Neno la Mwenyezi Mungu na kutafuta radhi zake mpaka mwashinde maadui zenu na myashinde matamanio yenu. Kwani Yeye Subhanahu amekukaribisheni kwake, na amekuteueni muinusuru Dini yake, na amekujaalieni muwe Umma wa katikati. Wala hakukulazimisheni katika aliyo kuwekeeni Sharia lolote lenye mashaka juu yenu msilo weza kulichukua. Na amekufanyieni mepesi katika yanayo kuleteeni mashaka, na katika msiyo yaweza amekufanyieni ruhusa namna mbali mbali. Basi ishikeni Dini hii, kwani hii ndiyo Dini ya baba yenu Ibrahim katika misingi yake. Na Yeye Subhanahu ndiye aliye kuiteni Waislamu, (yaani Wanyenyekevu) katika Vitabu vya mbinguni vilivyo tangulia, na pia katika hii Qur'ani kwa ut'iifu wenu kwa yale aliyo kutungieni sharia. Basi kueni kama alivyo kuiteni Mwenyezi Mungu ili muwe mwisho wenu mnamshuhudia Mtume kama amekufikishieni ujumbe nanyi mkatenda aliyo kufikishieni, mpate kufanikiwa, na muwe mashahidi kwa kaumu zilizo tangulia kwa yaliyo kuja katika Qur'ani kwamba Mitume wao nao walifikisha ujumbe. Na ilivyo kuwa Mwenyezi Mungu amekuchagueni nyinyi khasa kuwa ni wat'iifu kwake, mkashika Sala kwa ukomo wa ukamilifu wake, basi ni waajibu wenu kulipa hayo kwa kumshukuru na kumt'ii, mshike Sala kwa utimilifu wake, na mwape Zaka wanao stahiki, na mumtegemee Mwenyezi Mungu katika mambo yenu yote, na mchukue kwake msaada, kwani Yeye ndiye Msaidizi wenu na ndiye wa kuwanusuru. Yeye ndiye Mbora wa ulinzi na Mbora wa kunusuru.
Kwa hiyo Mtume Muhammad a Nabii Mussa na yesu Babu yako alikuwa ni Mtume ibrahim aka Baba wa Mataifa yote 2 waarabu na wayahudi. Na Nabii ibrahimu alikuwa ni Muislam.
Ninakuuliza wewe swali Nionyeshe katika Biblia je ni wapi Nabii ibrahimu alikuwa ni Mkristo?