Ushahidi wa kuwa kimeletwa na mola wa walimwengu ni kule kubaki kwenye asili yake zaidi ya miaka 1440 sasa hakuna mabadiliko hata ya herufi moja na hili ameliahidi mwenyewe allah kwenye kitabu chake pale aliposema.
"Hakika sisi ndio tulioteremsha ukumbusho huu{quran}, na hakika sisi ndio tutakaouhifadhi"
Quran 15:9
"Ni uteremsho utokao kwa bwana wa walimwengu wote.."
Quran 56:80
sema mkuu haujafungua moyo wako, haya maneno yana ufasaha na utaalamu wa hali ya juu ambayo hayawezi kupatikana kwenye utunzi wowote wa mwanadamu wala jini na Qur'an yenyewe imetoa challenge ya kiumbe yeyote anaeweza alete mfano wake na imetoa ruhusa ya kushirikiana viumbe wote wakitaka, na haijawezekana mpaka leo na haitowezekana.
"Waambie: Lau wangelikusanyika watu wote na majini wote ili walete mfano wa hii Qur'ani hawawezi kuleta mfano wake, ijapokuwa wakisaidiana wao kwa wao.."
Quran 17:88
Mimi sijapatapo kuona maneno matamu na yenye ladha kwenye moyo kama hii quran, hata uwe na stress vipi ukiisoma moyo unapata utulivu na amani unasahau shida zote.