Kama tunahitaji nishati ya umeme na tukakata miti ili tuipate sioni tatizo, suala ambalo watu wengi hawaelewi ni kubwa wapiga dili wa umeme wa mafuta na gesi walijua mitambo yao itadoda na dili zitaondoka ndiyo hao waliokuwa wanapaza sauti ili ionekane ni uharibu mkubwa, miaka 10 iliyopita kuna mikoa ilikuwa na mapori ya miti (Katavi, Tabora, Kigoma, Geita, Rukwa, Mbeya, Songwe, Ruvuma, Morogoro) nenda sasa hivi uone uharibifu wa mazingira kwa kisingizio cha kulima, kufuga, matumizi ya nishati ya mkaa miti imeteketea na tuko kimya hakuna suluhisho na inazidi kuteketea watu wako kimya