Nature preserved! Only for nature lovers

Screenshot_20211222-083815.jpg
 
Bonsai technique nataka nijifunze nifanye kama nitaweza.
Nilijifunza miaka ya 80,
1. Chagua aina ya mti unaopendeza porini.
2.Tafuta kifaa cha kupandia.
3.Panda mti wako na mwagilia uanze kukua.
4.Punguza matawi yabaki machache kwa staili inayopendeza, tumia kitu kikali kama mkasi maalum.
5.Chimba chini ya mti ili ukate mizizi, usikate yote kata mmojammoja kwa wakati kufuatana na inavyopona, uangalifu ni muhimu sana.
6. Unyime maji taratibu ili usikue haraka na uendelee kupunguza matawi na mizizi mingine kwa zamu mpaka iishe yote, uangalifu muhimu.
7. Hakikisha unapata jua lote na maji kidogo sana sana, usiwe kivulini, huu ni wakati wa mateso kwa mti wako ili udumae.
8.Utahitaji kila siku asubuhi na jioni uuangalie ukuaji wake uwe wa taratibu na unaweza kuufunga na waya ili ukue kwa staili unayoitaka.
Miti unayoiona ina umri wa zaidi ya miaka 15 na vizuri uchague miti yenye magamba makavu na inayovumilia mateso.
 
Shukrani sana baba.

Kwa hapa bongo ni miti gani ambayo yaweza kufaa? Wewe unayo mpaka sasa?
 
Maeneo kama kaskazini na nyanda za juu kusini iko aina nyingi na sehemu zenye mawe unaweza ukabahatika uliokulia juu ya jiwe na ukateseka, ila unahitaji uangalifu kuung'oa na kuupanda, tumia vyungu vifupi na mdomo mpana sana.
Nilikuwa nao ila ulipata ugonjwa ukafa.
 
Sawa mkuu. So ni rahisi zaidi kama mtu ukipanda miti inayopatikana sehemu zenye ukame. Miti ambayo inavumilia shida nyingi sio?
 
Back
Top Bottom