sinza pazuri
JF-Expert Member
- Aug 16, 2014
- 3,344
- 9,066
Kwenye pen game hakuna msanii wa kike wa bongofleva amewahi kufikia uwezo wa Zuchu toka bongofleva izaliwe nasema hakuna.
Jide ni msanii mkali, anauwezo mkubwa kafanya hitsong nyingi namheshimu kwa ilo ila huu mjadala nimeuona uko kuwa Jide anaweza andika kumzidi Zuchu haupo sahihi.
Jide ni mkongwe ila ngoma nyingi ameandikiwa, Zuchu 97% ya ngoma zake anaandika mwenyewe.
Nafikiri mnaona uhandishi wa Zuchu hata wasanii wa kiume wengi hawamuwezi.
Nyimbo kama Raha, Kwaru, Nisamehe, Naringa ni uhandishi wa kiwango cha juu sana cha sanaa.
Huu mjadala usiendelee popote nimeumaliza rasmi.