Nauli ya Zanzibar kuwa Tsh 25,000 vigezo gani vimetumika?


Yako majahazi yanaenda Kwa elf kumi mpaka elf Saba, pia kuna mashua na mitumbwi inaenda Kwa elf tano so ww Tu utaamua kupanda chombo gani
 
Ukiruka Zanz kwa ndege dk 5 unaiona bandari ya ya Dar, ajabu nauli ni 90k hadi 105k
 

Hapa sasa hoja yako imeeleweka.

Wataalamu watakuja kukupa majibu
 
M
Biashara Kama haina ushindani hiyo ni fursa wenye uwezo wa kuweka vyombo vya usafiri lazima wanufaike ila kukiwa na ushindan mbona naul itarud kawaida tu
Maji ya lita 1.5 tulikuwa tunauziwa 1500 , sasa hv makampuni yameongezeka tunauziwa 500 , wakati wale wa heritage water wauza lita 1.5 kwa sh 300
 
Mkuu bei hio ni fast boat tu kama Kilimanjaro.

Ukitumia sealink lile limeli Azam sea link bEi ni rahisi ila Jiandae kukaa masaa ya Kutosha Baharini


Pitia hapo kuona safari, Assume kama una Book Tanga pemba utaona. Maana route hio haina Fast Boat.
 

Kutoka nyamisati kwenda Mafia km 105 masaa manner ni shilingi 16000 tu
 
Kutoka nyamisati kwenda Mafia km 105 masaa manner ni shilingi 16000 tu

Unaenda na pantoni au mashua, hata dar Zanzibar Kwa mashua au pantoni ya Azam sea link ni bei hizo hizo elf 15
 
Ukiona ni karibu piga mbizi au tumia boti yako. Ni rahisi sana ukiwa haumiliki chombo kuona mtoa hufuma anakunyonya..ila ukishakumbuka kuwa gharama yake huiwezi..basi ni vema kukumbuka kuwa alowekeza pia anahitaji kutengeneza faida yake pia...
 
Yako majahazi yanaenda Kwa elf kumi mpaka elf Saba, pia kuna mashua na mitumbwi inaenda Kwa elf tano so ww Tu utaamua kupanda chombo gani
Kiukwel bei iko juu, nikikumbuka naul ya mwanza ukerewe ni 7000 na Mnasafir masaa3.
Hapo ilitakiwa angalau hta15000/- kutokana na uclassic wa hizo bot
 
Unguja ipo karibu na Dar, Pemba Iko karibu na Tanga. Kutoka Dar kwenda Unguja ni karibu kuliko kutoka Unguja kwenda Pemba.

Kama unaenda Pemba kutoka Dar, unapita Unguja kwanza ndio mnaelekea Pemba.
HV kuna boti ya moja kwa moja
 
Hivi ile Flying horse inayosafiri usiku kucHa kwa bei ya bwelele bado ipo?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…