Nimekupata Kiongozi
Kabla Sijatoa Thread Hyo Nikaona Kwanza Nitoe Hili Dukuduku Langu
Kweli Kila Mtu Na Uchaguzi Wake
Yaani Huoni Jukwaa Lilivyopoteza Hadhi?
Chunguza Hizo Thread Hapo Nje Ndo Utajua Nnachoongea Kina Maana Gani!
Mkuu Mimi natembelea sana na kuchangia sana hili jukwaa ndio maana nimeandika hivyo!
Kwa sababu ni jukwaa la celebrity ni lazima wajadiliwe celebrity na si kwasababu ya kuwa celebrity bali kwasababu wako hot kipindi hiki!
Hata kwenye maradio watu hulalamika nyimbo Fulani ndio zinapigwa sana kumbe wana sahau kuwa hizo zinapigwa kwa kuwa ziko kwenye chat na walaji ndio wanapenda kuzijadili!
Pengine wewe una shangaa watu wawili au mmoja kutawala jukwaa pengine majibu ni Yale Yale kuwa hao ndio wanao uza na hao ndio wana jadilika maana kuna kitu cha kuwafanya watu wajadili!
Na kuna ushahidi usio tia shaka wanao trend sana humu kwa mijadala ndio wanao ongelewa kwenye media zote bongo kwa kila siku bila shaka kwenye hili hutoomba ushahidi maana huko wazi!
Hata Mimi ningependa tusiwajadili au tusimjadili mtu mmoja kwenye jukwaa hili lakini ukiniuliza unataka tumjadili nani na kwasababu gani pengine naweza nisikupe jibu la haraka!
Pengine njia pekee ya kuondokana na hilo unalo fikiri ni tatizo ni kuanzisha mada zingine na uangalie...pengine ni wakati wao hao na ndio wanao uzika sana!
Pengine hadhi ya jukwaa Mimi na wewe tunaitafsiri tofauti .kwangu Mimi ninapo ona jukwaa linapata wachangiaji wengi kwenye mada hapo hadhi yake hiko juu na imeongezeka! Jukwaa hili unalo sema hadhi yake imeshuka lilikuwa limepooza sana miaka miwili iliyopita lakini kwa sasa ni Moja ya majukwaa hot hapa jf kama wewe si mgeni humu!
Pengine hadhi ya jukwaa ni zaidi ya kujadili watu wengi!