Wewe si umetaka bandari tusimpe mtu(dp) bali tuwekeze wenyewe atakachowekeza dp,kwanza tusomeshe watu wa kufanya hizo kazi...hili linashangaza sababu ticts wanaendesha bandari kwa miaka 25 sasa,au hatutakiwi kumpa mwarabu tu!?..ndiyo nikahoji kipindi hiki tunasomesha watu wawe na ujuzi wa dp,nani atakua akiendesha bandari!?..pili,ulidai tutie nguvu kusimamia utendaji,toka uhuru tumeshindwa kutia hiyo nguvu,miaka 63 tutaweza leo?!..tatu kwa nini hela za kuwekeza bandari Ili mwarabu asichukue tusiziwekeze kwingine?..maana kea mwarabu tutaweza kuongeza pato bandari kwa 67%+
Mkuu 'Gallow', naona unaning'ang'ania huku huelewi ninacho eleza.
Sasa ngoja nikueleze kwa kifupi sana na kwa utulivu. Fungua akili yako, acha kuniangalia kama mpinzani wako.
Ni hivi: Mimi naamini kwa dhati ya moyo wangu yote, kwamba waTanzania kwa sasa, hapa tulipo fikia, tunao uwezo wa kutosheleza kabisa kufanya mambo mengi sana sisi wenyewe bila ya kuhitaji kutegemea watu toka nje waje watufanyie kazi tunazoweza sisi. Kinacho kosekana ni uongozi wa kusimamia juhudi zetu hizi.
Ngoja nieleze tena mfano huo wa Bandari.
Tuliamua kwenda kukopa pesa World Bank ili tuiboreshe Bandari yetu iweze kufanya kazi vizuri. Kazi ilifanyika ya kukarabati kilicho hitajika kukarabatiwa. Uendeshaji wa Bandari tukaona hatuwezi. Tukawapa DP World mkataba wa miaka 30 au hata zaidi. Kwanza nieleze hili; kwa nini hatuwezi kuendesha bandari? Tunaambiwa na viongozi wetu kwamba wizi ni mwingi hapo Bandarini; viongozi wetu hawa wanaona ni kazi kubwa sana kuzuia wizi hapo. Ni kazi isiyo wezekana hadi tumtafute mwekezaji aje azuie wizi!
Kwamba waTanzania hatuna uwezo wa kuelewa mambo ya kuendesha bandari? Kama na wewe unakubaliana na sababu ya kipuuzi hii, hapa ndipo tusipoweza kuelewana hata kidogo; kwa sababu hakuna 'rocket Science) ya kushindikana waTanzania wasiweze kuielewa kwa muda wa miaka 30??... Licha ya hapo; nimekupa na mfano kwamba ni katika dhana hiyo hiyo potofu, inayotokana na viongozi wabovu, kwamba tumekaa na TICTS zaidi ya miaka 25 na bado tukawa hatuwezi kujifunza namna ya kuendesha Bandar???
Kwa hiyo; maoni yangu ni kuwa kutakuwa na sababu nyingine zinazo fanya viongozi wetu na baadhi yetu, kama wewe na huyo tapeli "Mtamu Sana" ya kutaka kila mara tutafutew watu wa kutufanyia kazi, huku sisi tumebutaa. Huu siyo uongozi.
Na usije ukadhani kwamba napinga uwekezaji, la hasha; kwa sabau ya utapeli tu wengi mnakimbilia huko; kama mnavyo fanya kuhusu mambo ya Ujamaa au Ukabaila, haya ni maswala ambayo yanatumika tu sasa hivi kuchanganya akili za watu. Si Ujama, au Ukabaila unaoendesha nchi yoyote duniani. Hizo zilikuwa ni siasa za nyakati hizo, zimekwisha pitwa na wakati.. Nenda Marekani kama hutakuta vimelea vya ujamaa huko; na ukienda China utakutana na vimelea vya ukabaila huko, pamoja na wao kujitambulisha kuwa wakomunisti.
Tunacho takiwa hapa kwetu Tanzania ni kuwa na uongozi unao lenga kuwajengea uwezo waTanzania waweze kuendesha sehemu kubwa ya kujiletea maendeleo ya nchi yao. Viongozi wapo kutafuta watu watakao kuja kutuletea maendeleo, jambo ambalo haliwezekani kamwe.
Bandari tunaweza kabisa kuendesha wenyewe. Wizi siyo sababu ya sisi kukimbia kwenda kutafuta watu. Wengine wanasema waTanzania ni WAVIVU? Hii nayo ni sababu? Kama ni teknolojia ambayo hatuna, hatuwezi kuinunua/kuikodi? Hatuwezi kuajiri 'consultants' wenye ujuzi huo kwa muda nasi tukijifunza?
Lakini, hapana, kazi rahisi kwa viongozi wetu wabovu ni kuwapa wageni waendeshe Huu ni ujinga.
Ni siku nyingi nime pendekeza kwamba nafasi ya kwanza kabisa tunayotakiwa kupata mgeni aje atuendeshee shughuli zetu ni palepale nafasi ya juu kabisa serikalini. Tumtafute mtu/watu toka nje waje waendeshe shughuli zote za serikali tukimjumuisha na Rais mwenyewe. Hawa tulio nao kazi hawawezi.