Nauliza, Mwalimu Nyerere nchi ilimshinda kuongoza?

Wewe umeandika stori za kusoma vitabuni ambazo ziliandikwa kwa ajili ya kuwapamba Viongozi,Tofautisha viwanda alivyofitaifisha Nyerere na viwanda alivyovijenga. Ninachojua mimi baada ya Azimio la Arusha selikali ilitaifisha vitu vingi Sana, kumbuka hivi viwanda,makampuni zilikuwa na management zake,baada ya kutaifisha ilibidi waweke manegement za selikali ambazo watu wake hawana uzoefu taratibu zikaanza kupungua ufanisi mpaka kufa kabisa mfano kiwanda cha kusindika Nyama Tanganyika Pekers,kilikuwa kinaajiri zaidi ya wafanyaka 2000 kabla ya kupata uhuru na kilikuwa kinauza nyama iliyosindikwa inje ya inchi na kuiingizia Tanganyika pesa za kigeni,leo hii ni uwanjwa wa maombi,hapo wa kulaumiwa siyo Nyerere

Chukulia mfano mdogo South Afrika ya makaburu ilikuwa bora zaidi kuliko ya sasa,Nelson mandera hakuwa mjinga hakuna alichotaifisha kutoka kwa wazungu,lakini Mugambe alijikuta inaharibu uchumi wa Zimbabwe baada ya kutaifisha mashamba ya walowezi, kiuharisi aliyoyafanya Nyerere hayana tofauti na aliyoyafanya Mugabe

Kwa hiyo waafrika wazawa wa Afrika kusini wana maisha mazuri kuliko watanzania .

Kweli tuna watanzania wa ajabu sana.

Hivi ukichukua nyumba na ardhi ya watanzania wazawa mpaka vijijini utawalinganisha na waafrika kusini. ?

Watanzania karibu kila mtu ana ardhi ya baba na babu zake ya asili. Huo ni utajiri mkubwa sana ambao nchi nyingi zenye vita sababu kubwa ni kukosekana kwa ardhi.

Ingekua ardhi haina maana basi hata Saudi Arabia tungependa kununua maeneo yenye mafuta na kuishi huko . Zanzibar uchoyo wao mkubwa kwa watu wa bara sio kingine ni Ardhi kwa sababu wenzetu wale walitangulia mbele sana kisiasa na kiuchumi hivyo wanajua thamani ya ardhi.

Viwanda vilihujumiwa baada ya wazungu kufukuzwa na wazawa wenyewe ambao wengi wao walikua na tamaa ya mali . Mbaya zaidi ikatokea vita ya Uganda miaka miwili.

Vita ya miaka miwili ni vita kuna sana . Lazima uchumi uyumbe kwa nchi changa kama ilivyokuwa Tanzania.

Viwanda vilivyojengwa na Nyerere ni vingi sana ukilinganisha na vichache kama tule twa kuchinja vingine pale Kawe. Aliyeua Tanganyika packers sio Nyerere. Aliyeuza General tyre sio Nyerere.
Hivi umewahi kujiuliza ni kwa nini Sementi inauzwa ghali wakati asilimia karibu 90 ya malighafi inatola Tanzania.

Hivi unajua unapompa nafasi kila mtu alimbikize mali bila serikali kuhoji chanzo unaua kila taasisi ya umma.

Tanzania taasisi zote zimekufa . Zote hakuna hata moja isipokua Jeshi la Wananchi pekee yake na miradi inayoisimamia japo kwa angalau kidogo. Ila hata miradi yao ya Nyumbu inauawa na Serikali ya CCM kwa kutowawezesha kwa kununa magari wa wanayotengeneza.

Mfano mimi wakati wa Supermarket za RTC wafanyakazi walikua wanashindana kuiba kila mtu jioni anatoka na sabuni,sukari,mikate ,siagi, mchele ,asali , n.k.
Wengine wanakwenda kuuza kwenye maduka binafsi ya walanguzi . Matokeo yake wananchi maskini wanashindwa kwenda kununua kwa watu binafsi kutokana na ulanguzi wa bei. Wanasubiri sukari ikiletwa ya bei rahisi wanapanga foleni . Serikali ilikua inatoa sukari kulinagana na idadi ya watu lakini wafanyakazi wa RTC walikua wanaiba sukari na kubakiza kidogo inauzwa siku moja inaonekana imeisha.
Sasa hapo Kosa la Nyerere ni lipi wakati nchi imetoka kwenye ukoloni watu ni maskini sana na wanaishi maporini kama Sup
 
Kuendelea kumtupia lawama Mwalimu Nyerere miaka 25 baada ya kifo chake ni uvivu tu wa kufikiri. kuamini kwamba matatizo yetu yote yameletwa na mtu mmoja wakati mfumo wa kuongoza nchi ni kazi ya taasisi nyingi zinazofanya kazi kwa pamoja.
 
Alianzia na wakoloni tulipopata uhuru akahamia serikalini. Lakini Mwalimu Nyerere alijenga barabara chache za lami.

Tulikua watu mil.12
Na tulikua hatulipi kopi nje . Kodi yetu na mapato ya Almasi na mazao ya kilimo yalitumika vizuri mana hawakua wanajilimbikizia mali . Aliwasomesha watanzania wengi nje ya nchi hasa madaktari na Mainjinia . Cha ajabu waliporudi wakawa wataalamu lakini walevi na wapenda starehe ndio maana kuna wakati tuliamini Kuwa madaktari wengi ni walevi muda wote .

Nyerere akaiacha nchi ikiwa na wasomi waliosoma Nje kwa ajili ya kuiendeleza nchi.
Aliyejaribu ni Mwinyi kwa kutodhibiti uwekezaji na wale wasomi waliokabidhiwa mashirika ya umma.
China haikuendelea Kwa lelemama . Ukitumia kamba yako kula nje ya stahiki zako unanyanganywa mpaka mali ulizoiba . Kwetu MwanaCCM akiiba hakuna hatua inayochukuliwa zaidi ya kuonekana ni mzalendo wa kujipamba chama kwa sifa. Nani atakua msafi kwa hali hiyo. ?

Iddi Amini Dada alifanya alichofanya Nyerere. Alitaifisha mali za wageni na kuzirejesha kwa waganda . Kwa muda mfupi Uganda ilipiga hatua wa anayojivunia mpaka leo.
Bila kutaifisha mali za wageni leo Uganda ingekua na waganda maskini sana kama ilivyo Kenya huku wachache wakiwa mabilionea .
Leo Uganda chini ya utawala mahiri na wa kizalendo wa Kaguta Museveni wanajitegemea kwa kiwango kikubwa na wanajeuri dhidi ya mashetani wa Ulaya na Uarabuni.

Hata Libya ,Ujerumani, China, Irani, Irak, n. k. zote zilifanya mapinduzi ya kisiasa na kiuchumi kwa kuwatimua mashetani yaliyojivika ngozi za binadamu.

Gadaffi alivyohujumiwa ndivyo na Nyerere alihujumiwa na nchi sasa nchi inauchumi wa chini sana ukilinganisha na rasilimali zilizopo chanzo kikiwa ni watawala kuwapigia magoti wageni na kuwaachia wapore rasilimali zetu kwa gharama nafuu chini ya Demokrasia feki inayosimamia na utawala wa kidikteta na kimapinduzi katika utendaji wake wote.

Wezi wanapewa madaraka lakini wale wanaowapinga wezi wanauawa na kutekwa nani ataacha kuiba
 
Pamoja na kwamba alikosea lakini yapo mengi mazuri aliyofanya! Elimu bure,Huduma ya Afya,Maji ilikuwa bure.
Nachomlaumu ni kutuachia Chama pendwa kilichokwisha geuka kuwa Chama Cha Mashetani.
Otherwise RIP Founder of National.
 
Kuendelea kumtupia lawama Mwalimu Nyerere miaka 25 baada ya kifo chake ni uvivu tu wa kufikiri. kuamini kwamba matatizo yetu yote yameletwa na mtu mmoja wakati mfumo wa kuongoza nchi ni kazi ya taasisi nyingi zinazofanya kazi kwa pamoja.
Sio kwa Tanzania ambapo Rais wa nchi amehodhi madaraka yote kikatiba. Anabeba mzigo wote.

Siku itakapokubaliwa na katiba ikarekebishwa, kwanza, kumuweka Rais na viongozi wote chini ya sheria na, pili, kuhamisha baadhi ya mamlaka stahiki kwa mihimili mingine na taasisi kuu za kitaifa, ndipo hiyo kauli ya “mfumo wa uongozi wa mihimili na taasisi” itakuwa na maana.

Nyerere alisimika mfumo wa imperial presidency ambao warithi wake huko CCM hawataki kabisa ubadilishwe. Wanaulinda kwa “jasho na damu” wakitumia vyombo vya dola kutisha na kuangamiza upinzani ndani na nje ya chama.
 
Kiongozi hapaswi kuwatia tabu anaowaongoza, akifanya hivyo ni kiongozi wa hovyo
Ndiye huyu huyu na huyo Mwinyi unaye mzungumzia. wewe.
Kugawa hovyo hovyo raslimali za nchi kwa wageni kama hao wawili walivyo fanya ni kuwatia tabu kubwa wananchi. Lakini kwa mtu wa aina yako huwezi kujuwa haya. Unabaki kuchekelea mipasho tu basi kama unavyo fanya hapa.
 
Fafanua kugawa rasilimali ni kupi?
 
Yale yale unarudia kila mara. Hivi huna hata moja unaloweza kujitahidi na kujitafutia taarifa; unasubiri tu upewe!
Atc,trc,ttcl,pride,mwatex,urafiki nk vyote tulidhindwa kuviendesha,mkapa akaanza ubinafsishaji,leo airtel iliyokua celtel na zain zamani,ilichukua rasilimali za ttcl,na vijana wa kitz wamepata ajira humo,kadhalika crdb, uwekezaji siyo kugawa/kuuza,acha a na fikra mgando za kijamaa
 
Ukitaka mjadala huo, tutajadilana sana, tena vizuri kabisa; ila kwa sasa hivi nikufahamishe moja tu:
Kugawa mapori yetu kwa kisingizio cha uwekezaji ni uenda wazimu.

Huo mjadala wa hizo TTCL na nyinginezo, nitafute nikiwa na muda mahsusi wa kujadili hayo.
Usikimbilie kila mara kutumia neno "UJAMAA" kama kinga ya kuvuruga raslimali za nchi.
Ujamaa hauelekezi huo uharibifu. Hiyo ni tafsiri ya watu wasiokuwa na fikra za kudadisi mambo kwa kina.
 
Mapori ni kama ttcl tu,na usitumie kugawa kana kwamba nchi haiingizi kitu kupitia uwekezaji huo,huo ni ubinafsishaji kama ilivyo kwa tbl,nbc nk
 
Hapo sasa ndipo kwenye tatizo na inaonekana huelewi kitu mpaka nifundishe.
Kazi ya kiongozi yeyote si kugawa mali za nchi hovyo hovyo. Huo sio uongozi.
WaTanzania hawawezi kushindwa kuiendeleza nchi yao kiasi kwamba kila kitu tukigawe kwa watu toka nje.

Kama wewe unafikiri hiyo ndiyo uongozi, basi mimi nasema wakati umefika tubinafsishe hiyo nafasi ya uongozi alionao/aliokuwa nao Samia/Mwinyi.

Na sita shangaa hata kidogo kama bado huelewi kitu nilicho eleza hapa.
Nakwenda zangu kwa sasa. Ukitaka mjadala ni huko baadae.
 
Back
Top Bottom