Nauliza swali kuhusu uumbaji

Nauliza swali kuhusu uumbaji

Mi naswali hapo mwanzo Mungu alitumbaa vitu, viumbe na Hawa na Adam, haya Sasa kwanini hadi wazungu waje kutuonyesha dini sahihi na huku Dunia ilishaumbwa mbona hakujitokeza kabla ni baada ya wazungu kutuambia yupo??🤦

Huko ulikosoma, hakuna mahali panapoonesha Mungu aliumba dini, na wala hakuna mahali ambapo huyo Mungu alijionesha kwa wazungu ili waje kuwaeleza watu weusi ya kwamba kuna Mungu...

Kati ya bin adam wa kwanza kujua uwepo wa Mungu, watu weusi walikuwa ni wamoja wapo...

Kihistoria wana wa adam wote kwa ujumla walikuwa 'waasi' na wakawa wanaanzisha imani na kutambua miungu yao, huku wakihama toka eneo moja juu ya uso wa dunia hadi eneo jingine...

Hivyo kwa mantiki hiyo ya human migration, sio kuwa wazungu walikuja kutuletea hayo mafundisho bali walikuja kufanya restoration ya maarifa ambayo babu wa mababu zetu wa kale na kale walikuwa wakiyajua ila waliasi na kutawanyika maeneo ya mbali na ustaarabu wa elimu hiyo ya Yehova...

Kama una ubongo wa kuelewa, soma vitabu vyote vya Musa...
 
Mi naswali hapo mwanzo Mungu alitumbaa vitu, viumbe na Hawa na Adam, haya Sasa kwanini hadi wazungu waje kutuonyesha dini sahihi na huku Dunia ilishaumbwa mbona hakujitokeza kabla ni baada ya wazungu kutuambia yupo??🤦
Hakuna dini sahihi yoyote ile chini ya jua.
Dini ni mpango wa mwanadamu kumtafuta Mungu
 
Mi naswali hapo mwanzo Mungu alitumbaa vitu, viumbe na Hawa na Adam, haya Sasa kwanini hadi wazungu waje kutuonyesha dini sahihi na huku Dunia ilishaumbwa mbona hakujitokeza kabla ni baada ya wazungu kutuambia yupo??[emoji1751]
Usikufuru mambo ya kiimani.. Hayana mwisho mwema...!
 
Wazungu hawajui dini ? Mambo ya dini wazungu sio asili yao, wao wenyewe waliletewa tu, wakafanya ukarabati wanavotaka wao ionekane machoni mwa watu, alaf nd waka anza kuisambaza. Ukitaka kujua dini, tembelea nchi zenye asili ya Dini, nchi zenye chimbuko na asili ya Mitume unayoiamini wewe.(nikiongelea Mitume siongelei kina mwamposa na wenzake wanaojipachika utume na unabii) nadhani umenielewa.
Wazungu kwenye Ukristo ni wajuzi tu hapa
 
Wazungu hawajui dini? Mambo ya dini wazungu sio asili yao, wao wenyewe waliletewa tu, wakafanya ukarabati wanavyotaka wao ionekane machoni mwa watu, halafu nd wakaanza kuisambaza. Ukitaka kujua dini, tembelea nchi zenye asili ya Dini, nchi zenye chimbuko na asili ya Mitume unayoiamini wewe.(nikiongelea Mitume siongelei kina mwamposa na wenzake wanaojipachika utume na unabii) nadhani umenielewa.
Mungu amewahi kushusha dini duniani? Dini gani ambayo siyo man made?
 
Mungu amewahi kushusha dini duniani? Dini gani ambayo siyo man made?
Dini zote ni man made hakuna sehem Mungu amesema amezileta, ispokua dini moja tu ambayo ni Uislam Mungu amesema wazi ameileta yeye na anaetaka kufaulu siku ya mwisho basi awe muislam na afuate mafundisho ya Uislam na atekeleze na yeyote atakaejichagulia dini isiyokua Uislam basi huyo yupo katika khasara kubwa. (Quran 5:3.)

Hiyo ndio dini aliyoishusha Mungu, nenda kasome hiyo 5:3 Quran unaeza soma na zaid kwa ajili ya kujiongezea maarifa, elimu saiz ni bure ndug.

Sasa wewe jiulize unafata dini alioileta Mungu au man made!
 
Mimi nina swali, hapo mwanzo Mungu aliumba vitu, viumbe na Hawa na Adam, haya sasa kwanini hadi wazungu waje kutuonyesha dini sahihi na huku Dunia ilishaumbwa, mbona hakujitokeza kabla ni baada ya wazungu kutuambia yupo??🤦
Labda kama ulitaka muujiza wa Mungu kujidhihirisha kwa watu wote duniani pote kwa wakati mmoja, ila kila kitu kina mahali pa kuanzia kisha kinasambaa. Mfano kwenye ukristo, UKRISTO (kumuamini KRISTO/UFUASI KWA YESU KRISTO) ulianzia kwa yeye YESU kisha kwa wanafunzi wake, baada ya kuwapa training ya kutosha, siku anapaa (kwa imani ya kikirsto) aliwaachia Roho Mtakatifu na maagizo kuwa ,

Marko 16:15-16 BHN​

Basi, akawaambia, “Nendeni ulimwenguni kote mkahubiri Habari Njema kwa kila mtu. Anayeamini na kubatizwa ataokolewa. Asiyeamini atahukumiwa.

Mathayo 28:19 BHN​

Nendeni basi, mkawafanye watu wa mataifa yote wawe wanafunzi wangu, mkiwabatiza kwa jina la Baba, na la Mwana, na la Roho Mtakatifu

Maana yake ni kuwa mpaka Yesu anaondoka alijua wapo watu wengi duniani kote wasiojua habari zake, hvyo wanafunzi wanapokea majukumu nao watawapa wengine vizaz na vizaz mpaka wa missionary walivyotufikia.


Sasa usishangae kuletewa dini na wazungu
 
Back
Top Bottom