Naumia, nami ni binadamu

Naumia, nami ni binadamu

Asante.nimeshawafahamu vema.
Lengo ni kuwapa tu ujumbe,lakini kama siwezi kuwabadili ntawakabili.
Masikini pole sana mama, ndio walimwengu tulivyo. Usiwe ma moyo mwepesi wa kubeba mambo kiasi hicho dear. Hii dunia ina mengi na hayo ndio kwanzaaa kumekucha. I feel yo pain na nafikiri niliona hivyo vijembe kutoka kwa wawili wa waliokusaidia ila usipate taabu maana nafikiri tayari unawafahamu ni watu wa aina gani. Haupaswi kuwapa nafasi kabisa ya kuizuia furaha yako.

Hauna haja ya kurudisha hizo pesa, ichukulie tu kama funzo kwako na endelea na maisha yako. Mshukuru Mungu uko na afya njema sasa, muombe azidi kukupa afya ili upambane ufikie malengo yako.
Yakikuelemea mlilie Mungu, lia kwake, yaseme yote kwake upate ahueni. Ukimaliza nyanyuka chapa mwendo. Sie binadamu tusikusumbue kichwa kabisa.
 
Asante suriya
Ni Mungu pekee awezae kuubadili moyo wako na kuufanya kuwa mgumu,
Kwani akikaa ndani yako na utaenenda kwa jinsi ya kiroho.
Wanadamu hawata kutenda kitu.

Lakini ukitegemea uwezo wako mwenyewe, wanadamu lazima wakuvyoge vyoge na kukuumiza.
 
Mkuu sikua na ahadi za sina hiyo.labda yeye ndo a nawaza hivo.
Na wala sina hisia za mapenzi nao
Masikini hutujui sie! Alikuwa anadhani huo msaada ni mtama kwa mtoto. Tatizo haoni ukijiongeza. Huwa nawatahadharisha mabinti kupata misaada kutoka kwa wanaume ambao si wa tumbo moja. Hilo lielewe leo
 
Agy pole. Ila ngoja nikushauri nikupe ushauri tofauti.
Yawezekana hawakufanyii makusudi, kupishana huku jukwaani ni kawaida sana. Kujibiana shombo ni kawaida sana. Sasa pengine wewe unahisi wanafanya hivo kwa sababu wamekusaidia.

Na hata kama wapo wanaofanya hivyo labda ni mmoja au wawili pasikufanye ukaona watu wote 10+ wanakufanyia hivyo.

Kuhusu kuwalipa, hauwezi kuwalipa kabisa. Nakazia kwamba HAUWEZI KUWALIPA KAMWE. kwa sababu ile sio hela tuu walikupa Bali walikufanyia WEMA, WALIKUINUA KIPINDI UMEANGUKA, WALIKUFANDILI. Hela utawapa lakini hela sio kitu , Fadhila walizokutendea hauwezi kuzirudisha kwa sababu hazirudishwi kwa pesa.

Usizire. Muombe Mungu akupe uvumilivu na ujasiri. Na pia jaribu kuishi kama hamna kilichotokea.

Watu waliokufanyia WEMA lazima wanajisikia vibaya kwa hivi unavyoviandika, mara utawarudishia, Mara unawajua wote. Kila mtu anaweza akawa anahisi unamwona adui kisa alikusaidia.

Kosa la mtu mmoja au wawili lisikufanye uone watu wote waliokusaidia wanakunyanyasa.
 
Loh!sawa mkuu

Asante mkuu

Kwa marafiki na jamaa wa jf.
Mwaka 2018 nilipata tatizo la ghafla na kuugua,na pia sikua na uwezo ama kujiaandaa kukabiliana na hill tatizo.kwani nlitoka kwenye kipindi kigumu cha kumuuguza ndugu yangu na sikua na kipato,hali ilivozidi kuwa mbaya ikanilazimu kuomba msaada kwa baadhi ya marafiki wa jf,kuna watu walijitokeza na kunisaidia kupata 300K ya bima ya Afya nkaleta na mrejesho
Lakini tatizo liko hapa;
Kuna baadhi ya member mnaniweka kwenye masikitko na huzuni,its like Mimi ndo wa kwanza kupata matatizo na kuomba msaada jf?
Imekua too much kwa sasa,lisitokee jambo mtu kaibuka na kuongeea msaada nliopata,kuna wengine mnafikia hata ya kunidhalilisha kwa makosa yasiyojulikana,makosa ambayo siyajui na hapana ukweli kabisa.

Kuna mda mwingine nakubali nakosea,nakubali na naomba mkumbuke Mimi ni binadamu kama wengine sio malaika.
Lakini kinachoshangaza na kuumiza mtu anakuja na kuingiza habari za msaada kwenye hayo masuala..its inhumane.
I appreciate what you did to me,ni kitu kikubwa ambacho kilinisaidia mno,lakini the way mnavolikuza na kuliongelea ni kama nlipewa mkopo na si msaada wa kibinadamu..
Whenever you get a chance u use it to insult me..why!
Mimi ndo wa kwanza kuomba msaada humu jf?kama kwenye matatizo wore wangetreatiwa hivi ni yupi angekua na amani mbele za watu?
guys,nlipoteza wazazi wore wawili nkiwa mdogo sana.nkachukuliwa na familia ya mtu,nkakua kwao,lakini kila nikikosewa au kufanyiwa ubaya kama binadamu nkiongea kuonyesha nlivokereka maneno ntayorudishiwa ni "huna baba wala mama,tumekulea hadi umekua nk.!
Nnapopokea kauli kama hizi natamani nifanye malipo,angalau kupunguza maneno,,lakini malipo ya wema na utu ntayalipaje,kama ni chakula ntawalisha nkifanikiwa.
Na kwenu pia,nashukuru sana kwa mda wenu,kujitoa kwenu na upendo wenu mlioonyesha.wenyezi Mungu Atawalupa kwa hili.
Lakini kwa upande wa pesa angalau ntawalipa.nko imara kwa sasa hapo sio kikamilifu lakini nna nguvu ya kufanya mengi ukilinganisha na mda uliopita.
Ntajitahidi kwa kadri ya uwezo wangu nirudishe kidogo kidogo angalau maneno yapungue.maana najiona nna deni kwa jinsi hali ilivo.

Watu walionifanikisha msaada wapo 13.kipindi napokea msaada niliwanote kwenye diary, na wote nawajua I'd zao na amount ya kila mmoja.ntajitahidi taratibu kurudisha angalau nipate nafuu.
Nawapemda wote!
Aggy!
Pole sana, usife moyo wakati mwingine huna budi kupuuza japo inaumiza[emoji26][emoji26]
 
Pole sana aggyjay

Siku zote dawa ya mjinga ni kumnyamazia na huwezi kuzuia mtu kuongea/kuandika anachotaka...sometimes ni suala la kuignore unachokisoma

Unadhani ukiwarudishia hizo pesa ndio watakosa cha kukuattack?kimsingi ningekuwa mimi nisingerudisha hata cent,hukushikia mtu bunduki akusaidie na haitasaidia chochote kwao kuendelea kuongea

Ni ngumu sana kumplease binadamu na huwezi kupendwa na kila mtu
You have grown up enough,you are matured enough!
 
Manengelo dadangu unaweza sema najistukia.but ukiangalia wanaenda straight kwenye hili bila kificho.watu wananijulisha pm,wanahangaika sijui kufukua thread za nyuma for what?
Halafu ukiangalia vitu havihusiani kabisa na wao,wanajistukia,wanatumia kigezo cha msaada kuattack.kwa nini wao wasikae mbali na Mimi na kuacha kuongelea yalopita?
Si wapi attention,Bali kelele zao zinanikera.
Duh ...pole...au unajistukia tu mwenywe...!kama Serikali yenyewe inasaidiwa sembuse binadamu...ww songa mbele..usiwape attention..alikusaidia yamepita...usiweke mazoea nao!usirudishe ht mia
 
Manengelo dadangu unaweza sema najistukia.but ukiangalia wanaenda straight kwenye hili bila kificho.watu wananijulisha pm,wanahangaika sijui kufukua thread za nyuma for what?
Halafu ukiangalia vitu havihusiani kabisa na wao,wanajistukia,wanatumia kigezo cha msaada kuattack.kwa nini wao wasikae mbali na Mimi na kuacha kuongelea yalopita?
Si wapi attention,Bali kelele zao zinanikera.

Mie ndo najua leo uliwah saidiwa naijua tu tmuzi wako m1 ultamani kujiua .. ss mbona hapo patamu??wafate pm waambie jaman kunisaidia kusinifanye nishindwe kujiachia usipumue kisa ?khaaa ..mm humu@KingY aliwah nisaidia hela ila akiongea shit jukwaa za siasa nampa dislike kbs..iweje wakuonee hvyo !ww unawaogopa..wachane live
 
Back
Top Bottom