Naumia, nami ni binadamu

Naumia, nami ni binadamu

Agy pole. Ila ngoja nikushauri nikupe ushauri tofauti.
Yawezekana hawakufanyii makusudi, kupishana huku jukwaani ni kawaida sana. Kujibiana shombo ni kawaida sana. Sasa pengine wewe unahisi wanafanya hivo kwa sababu wamekusaidia.

Na hata kama wapo wanaofanya hivyo labda ni mmoja au wawili pasikufanye ukaona watu wote 10+ wanakufanyia hivyo.

Kuhusu kuwalipa, hauwezi kuwalipa kabisa. Nakazia kwamba HAUWEZI KUWALIPA KAMWE. kwa sababu ile sio hela tuu walikupa Bali walikufanyia WEMA, WALIKUINUA KIPINDI UMEANGUKA, WALIKUFANDILI. Hela utawapa lakini hela sio kitu , Fadhila walizokutendea hauwezi kuzirudisha kwa sababu hazirudishwi kwa pesa.

Usizire. Muombe Mungu akupe uvumilivu na ujasiri. Na pia jaribu kuishi kama hamna kilichotokea.

Watu waliokufanyia WEMA lazima wanajisikia vibaya kwa hivi unavyoviandika, mara utawarudishia, Mara unawajua wote. Kila mtu anaweza akawa anahisi unamwona adui kisa alikusaidia.

Kosa la mtu mmoja au wawili lisikufanye uone watu wote waliokusaidia wanakunyanyasa.
What a post!!!
 
Asante joanah..but kuna mda mwingine naelemewa na masimango ya watu.najiona nna mzigo
Naomba kukuuliza hao waliotoa msaada hapa jf ndio haohao wanao kusimanga? Kama ndio ni wote waliotoa ndio wanakusimanga? Anae toa maisha yote hasemi alichotoa lakini wapambe ndio wanao simanga. Uzi wako ulisomwa na wengi wachache walikusaidia wengine wanabakia kusimanga wakati hata senti 1 hawakutoa. Ushauri wangu kama yupo alie toa na kukusimanga mpatie hela yake lakini kama hakuna. Ukiwarejeshea utawapatia unyonge kwenye mioyo yao kwasababu walikusaidia kwa moyo safi.


Nangatukaa 🏃‍♂️🏃‍♂️🏃‍♂️
 
All will be well😘
NB.usiwape attention mwaya,its better to pretend like nothing happened ila najua ni ngumu unapaswa kuwa na roho ngumu asee ili upate auweni moyoni mwako.
Fanya kama huoni kumbe unable
 
Back
Top Bottom