Uchaguzi 2020 Naunga mkono aliyoyazungumza Lissu kwenye “ufunguzi wa kampeni” mengi aliyoyasema hatukuyafahamu. Nashauri afanye hivyo kila mkutano

Ni sahihi kabisa.

Lisu ni lazima kwanza auseme uovu wote ulifanywa awamu hii, halafu baadaye aeleze yeye atafanya nini, tofauti na uovu uliofanywa na awamu hii.

Aeleze jinsi alivypshambuliwa, sababu ya kushambuliwa kwake, alivyonyimwa matibabu, wabunge wa CCM walivyozuiwa kwenda kumwona, polisi walivyoamua kutochunguza.

Aeleze wengine waliopatwa na madhila ya aina mbalimbali kama vile Ben Sanane kwa kuhoji elimu ya jiwe, Azory kwa kuweka wazi mauaji ya raia, madiwani waliouawa kwa kukatwa mapanga na watu wa CCM.

Aeleze jinsi hela za umma zinavyotapanywa kwa kununua ndege, kujenga uwanja wa ndege Chato, majengo makubwa kama ya TRA kujengwa Chato badala ya Geita, bohari ya kanda ya madawa kujengwa Chato, n.k.

Aeleze pia dalili za upendeleo zinazoonekana kama vile teuzi mbalimbali kuegemea kanda moja, ndugu kuwekwa kwenye nafasi kubwa za serikalini, n.k.

Kisha azungumzie jinsi Serikali yake itakavyofanya kuwapunguzia madhira ya awamu ya 5, na kisha mifumo itakayozuia kiongozi mwingine kuliingiza Taifa tena kwenye madhira kama ya sasa.
 
Hapana aisee. Hata nafsi inakusuta. Ila bado ana chance kubadili upepo.
Hana haja ya kubadili upepo hata kidogo. Kwanza jana ni kwasababu wameamuwa kutafuta haki kwanza iliyopokwa na tumeccm
 
Maghufuli akishinda, ina maana watanzania wengi wana mambo ya kishetani, jambo ambalo sikubaliani nalo hata kidogo. Watanzania ni watu wenye huruma na ubinadamu. Kenya wenyewe huwa tunawashangaa!
 
Kazi na dawa.
 
Maghufuli akishinda, ina maana watanzania wengi wana mambo ya kishetani, jambo ambalo sikubaliani nalo hata kidogo. Watanzania ni watu wenye huruma na ubinadamu. Kenya wenyewe huwa tunawashangaa!
Sijataja jina hapa usiletee Mambo ya kiduanzi
 
Yah huyu mzee alifariki kwa ajali ya ndege huko mikoa ya nyanda za juu kusini km sijakosea!
 
Arejeshe na ajenda ya kupambana na ufisadi, ccm wanafanya kampeni kwa pesa ya ufisadi trillioni 1.5 na pesa ya vitambulisho vya machinga.
 
Yote hayo hata mimi sikuyafahamu. Pia sikufahamu kuwa serikali ya Kenya ilimpatia ulinzi rasmi.
 
Arejeshe na ajenda ya kupambana na ufisadi, ccm wanafanya kampeni kwa pesa ya ufisadi trillioni 1.5 na pesa ya vitambulisho vya machinga.
Naam, hii ya ufisadi asiache hata kidogo. Bado yule mkaguzi mkuu wa serikali aliyegunduwa ufisadi hajazungumziwa. Watanzania hawakuruhusiwa kuongea lolote maana kesi za uhujumu na kupotezwa ni kawaida kabisa na ccm huwa wanafurahia na kuchekelea. Sijui ni watanzania wa aina gani hawa?🤦🏾‍♂️
 
..amewataja Khadija Akukweti, Amina Abrahman Kanyama, na Adam Mohamed Bakari, ndio waliomuwahisha hospitali Dodoma.
 

Kabisa Mkuu. Hapa Lissu na team yake wakazie
 
..amewataja Khadija Akukweti, Amina Abrahman Kanyama, na Adam Mohamed Bakari, ndio waliomuwahisha hospitali Dodoma.

Majina hayo yanadhihirisha waislamu wana mchango mkubwa katika historia ya Lissu. Mambo hayo yanampa mtu mmoja kiwewe hadi anaamua kuendesha mchango wa ujenzi wa msikiti akiwa kanisani!!

Mfumo wa kisiasa wa nchi hii umekuwa designed makusudi kuhakikisha wapinzani hawawezi kuwaunganisha waislamu na wakristo katika chaguzi kuu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…