Uchaguzi 2020 Naunga mkono aliyoyazungumza Lissu kwenye “ufunguzi wa kampeni” mengi aliyoyasema hatukuyafahamu. Nashauri afanye hivyo kila mkutano

Uchaguzi 2020 Naunga mkono aliyoyazungumza Lissu kwenye “ufunguzi wa kampeni” mengi aliyoyasema hatukuyafahamu. Nashauri afanye hivyo kila mkutano

jmushi1

Platinum Member
Joined
Nov 2, 2007
Posts
26,329
Reaction score
25,263
Wanajamvi,

Nimeona malalamiko mengi kutoka kwa wana CCM, eti hawajasikia Lissu akizungumza atakayoyafanya! Na leo kwenye uzinduzi wa kampeni yao, mwenyekiti wao eti anajidai kufuata ushauri wa wananchama wake ambao wanaumizwa kweli kweli wakisikia Lissu akizungumzia kuumizwa kwake, na msaada alioupata kwa watanzania na duniani kote!

Yani sikufahamu kuwa Dr Mpoki ambaye alikuwa katibu mkuu wa Wizara ya Afya, alikubali apelekwe Nairobi, sasa hivi amekuwa “demoted” kwa kuonyesha ubinadamu, na sasa ni balozi.

Anachofanya Lissu, kitampa ushindi. Kama hotuba hii ya kwanza ilisikilizwa na wengi, basi hoja kuu ni haki! Watanzania wengi, wanahisi hawatendewi haki na serikali hii. Kuanzia wafanyabishara hadi watumishi wa umma.

Pia hotuba hii, imeitayarisha mioyo ya Watanzania kuanza kumsikiliza Lissu, kwani wanaona kama ndiyo sauti yao ambayo imezimwa na udikteta Unaofurahiwa na wale “minions” wenye kunufaika!

Namshauri Lissu, hata kama ikitokea wanaanza kuelezea sera, asiache hata kidogo kuzungumzia madhila yaliyompata yeye na Watanzania wengi tu. Asiache kumtaja Ben Saanane vile vile. Na baada ya hapo, aendelee kuyazungumza mengi mazuri ambayo alikuwa ameshaanza kuyazungumza. Yote ambayo ni tofauti na serikali hii.

Maoni ya Retired

Lissu yuko very focused na strategic. Wafungue mawazo/fikra watu kwanza wajitambue kuwa wanaonewa! , ni watumwa, HAKI ZAO ZA BINADAMU ZIMEKUFA etc, then baadaye tandaza sera! AU awe anaanza na sera, then dakika 20 za mwisho ni kuwafungua watu wanavyonewa, wanavyoibiwa na Jiwe, wanavyokosa haki zao etc etc
 
Lissu kachemka sana na wewe kamanda unazidi kumpalia mkaa aendelee kuchemka.

Haya ndiyo chaguo lenu makamanda msiyo na depo
 
Jitihada kubwa zinafanywa na WanaCCM ili Lissu asiseme mateso aliyopitia kwa sababu ushahidi unaelekea mlangoni kwa Mfalme.
Uchunguzi wa Aliyekua Waziri wa mambo ya nje wa Kenya Marehemu Auko ulipoanza kuonesha kuwa Mfalme wa nchi hiyo anahusika uchunguzi ukasitishwa gafla.
 
...
Yani sikufahamu kuwa Dr Mpoki ambaye alikuwa katibu mkuu wa wizara ya afya, alikubali apelekwe Nairobi, sasa hivi amekuwa “demoted” kwa kuonyesha ubinadamu, na sasa ni balozi.
.....
Mkuu, Mimi bado ninaamini kuwa, wewe bado unajenga hoja objectively! Kwa imani yangu hiyo hiyo ninakuomba utoe ufafanuzi usiotiliwa shaka ikibidi utumie na takwimu kuimarisha ufafanuzi juu ya namna gani Dr. Mpoki amekuwa Demoted.

Pia itakuwa vyema sana ukifafanua vizuri kazi aliyokuwa anifanya hapo kabla na baada ya Yeye Dr. Mpoki kutoa msaada wa kibanadamu na wa kidaktari kwa Lissu.

Karibu, Mkuu.
 
Sikujua kwamba aliyemuwahisha TL hospitali ni binti wa Mzee Juma Jamaldin Akukweti[r.i.p].

Juma Akukweti alikuwa mbunge wa Tunduru na alipata kuhudumu ktk serikali za Raisi Mkapa.

Huyo binti alikuwa msaidizi wa TL ktk bunge la 2010 to 2015, na sasa hivi ni msaidizi wa Dr.Tulia Ackson.

Sasa huyu binti wa Akukweti alikwenda kuitwa na msaidizi wa nyumbani wa TL, na pamoja na dereva, wakamkimbiza hospitali.

Bila msaada wa haraka wa hao watatu, nadhani tungekuwa tunazungumza habari nyingine leo.
 
Lisu yuko very focused na strategic. Wafungue mawazo/fikra watu kwanza wajitambue kuwa wanaonewa! , ni watumwa, HAKI ZAO ZA BINADAMU ZIMEKUFA etc, then baadaye tandaza sera! AU awe anaanza na sera, then dakika 20 za mwisho ni kuwafungua watu wanavyonewa, wanavyoibiwa na Jiwe, wanavyokosa haki zao etc etc
 
Kumbe ndio maana hampati watu kuja kusikiliza sera zenu kumbe mnachoongea ndio hiki. Afadhali mnarahisisha uchaguzi kwa wapinzani wenu maana mnajipiga risasi nyie wenyewe..
 
Jitihada kubwa zinafanywa na WanaCCM ili Lissu asiseme mateso aliyopitia kwa sababu ushahidi unaelekea mlangoni kwa Mfalme.
Uchunguzi wa Aliyekua Waziri wa mambo ya nje wa Kenya Marehemu Auko ulipoanza kuonesha kuwa Mfalme wa nchi hiyo anahusika uchunguzi ukasitishwa gafla.
Umegonga penyewe mkuu! Ni kama moto unaowachoma, sasa wanataka uzimwe!
 
Kumbe ndio maana hampati watu kuja kusikiliza sera zenu kumbe mnachoongea ndio hiki. Afadhali mnarahisisha uchaguzi kwa wapinzani wenu maana mnajipiga risasi nyie wenyewe..
Lissu alijipiga risasi mwenyewe? Hata siku anakuja si mlisema hakuna atayekwenda kumpokea tena na biti la Sirro?😂

Kadri mnavyishangazwa, watu waelewa ndiyo wanawashangaa zaidi.
 
Lisu yuko very focused na strategic. Wafungue mawazo/fikra watu kwanza wajitambue kuwa wanaonewa! , ni watumwa, HAKI ZAO ZA BINADAMU ZIMEKUFA etc, then baadaye tandaza sera! AU awe anaanza na sera, then dakika 20 za mwisho ni kuwafungua watu wanavyonewa, wanavyoibiwa na Jiwe, wanavyokosa haki zao etc etc
Very very well said!
 
Kazi anayo kubwa aisee kama ataamua kiwa mwl wa uraia
Maana kila anakopita lazima amwage notes kwa wananchi huku wenzake wakichanja mbuga kumwaga sera zaoo hahahaaa

Ualimu sio kazi nyepesi mjue, hadi wakuelewe watu ushapoteza muda mwingi wa kumwaga sera haahaaaa,

Lisu inabidi aachane na Uraisi ili aitumikie nafasi ya ualimu vyema aisee
 
Back
Top Bottom