Naunga mkono suala la kubinasifisha Bandari ya Dar es Salaam

Naunga mkono suala la kubinasifisha Bandari ya Dar es Salaam

BLACK MOVEMENT

JF-Expert Member
Joined
Mar 11, 2020
Posts
4,548
Reaction score
11,901
Ifike wakati Serikali iachane na kufanya biashara make huu ni ujamaa na ushakuwa proved haiwezekani zaidi ya upigaji.

Kwa taarifa zaidi soma hapa >> Tanzania inatarajiwa kuingia mkataba na kampuni ya DP World ya Dubai kuendeleza Bandari ya Dar es Salaam

Mashirika ya umma kama Bandari, Tanesco, Maji, sijui Posta, TTCL, ATCL, na zinitakiwa kuingia sokoni kuuzwa.

Hiyo Bandari ya Dar kama ingejengwa ya Baganoyo na ya Bagamoyo ikawa ni private na ya Dar ikawa ni ya Serikali bila shaka meli zingehamia Bagamoyo na ya Dar ingekuwa kama TTCL now.

Tanesco angali utendaji wao, lazima wafuatwe offisini uwe unajuama na mfanya kazi mmoja wapo, na sio tu kufuatana na kuwapa rushwa juu, sasa ingekuwa inasimamiwa na watu weupe unazani kungekuwa na kufuatana offisini?

Angalia TTCL haijulikani kazi zao kwa sasa, hivi TTCL ilikuwa ni ya kushindwa hadi na wakina Haloteli? TTCL ilipaswa kuwa sawa na Vodacom, ila Kwa sababu ni Mali ya Umma hakuna anaye jali pale na imejaa wafanya kazi wengi kuliko ufanisi na hakuna anajali.

Mamlaka za maji zimejaa upigaji tupu, unafuatilia kuunganishiwa maji hadi unachoka na lazima uhonge la sivyo hutakaa uunganishiwe maji.

Kwani Bandari ikikodishwa hao wanao kodisha watakuja kuondoka nayo? Wataihamisha? Tuachane na ujamaaa
 
Kuwaachia kila kitu wawekezaji maana yake tunakiri hatuwezi kujitawala, ni bora sasa tumrudishe mkoloni arudi kwasababu naamini kabisa, jinsi mambo yanavyoendelea serikalini kwa sasa, pia tunahitaji kuibinafsisha serikali yetu.

Hivyo sioni sababu kwanini tuendelee kuwaza kubinafsisha vitu vidogo dogo, wakati kule juu penye tatizo la msingi tunaendelea kupaacha kama palivyo, alaah, kumbe inawezekana hata vichwa vyetu pia vinatakiwa kubinafsishwa, kwasababu fikra zetu nazo ni mgando.
 
Kuwaachia kila kitu wawekezaji maana yake tunakiri hatuwezi kujitawala, ni bora tumrudishe mkoloni arudi kwasababu naamini kabisa, jinsi mambo yanavyoendelea serikalini kwa sasa, pia tunahitaji kuibinafsisha serikali yetu.

Hivyo sioni sababu tuendelee kuwaza kubinafsisha vitu vidogo dogo, wakati kule juu penye tatizo la msingi tunaendelea kupaacha kama palivyo, kumbe inawezekana hata vichwa vyetu pia vinatakiwa kubinafsishwa, kwasababu fikra zetu nazo ni mgando.
It's my opinion too serikali ibinafsishwe
 
Tatizo sio kubinafsisha, tatizo ni yale unayoyataria baada ya kubinafsisha yatapatikana?

Leo mitandao ya simu ni binafsi, wanafanya yale tusiyokubaliana nayo, WAZIRI muhusika kageuka kuwa MSEMAJI wao, nini tunanufaika nacho?

Wauza mafuta, ni binafsi. EWURA wapo, bei ya mafuta imeshuka huko duniani, wauza mafuta wamegoma kushusha, untouchable, ukiuliza, unaambiwa muagizaji mwenyewe ni remotr controller wa nambari uno! Hapa ubinafsi zaidi ndo manufaa labda.

Magufulification ndo mwarobaini!
 
Naungana na wewe serikali kufanya biashara ni kunufaisha watu wachache tu maana wizi ni asili ya watanzania ziwekwe terms nzuri kimkataba ambazo zitaipa pesa za uhakika serikali wawaachie wawekezaji.hata ufanisi utakuwepo sana na malalamiko yatapungua sana
 
Watanzania ni wezi imeshindikana kuwadhibiti kutokana na aina ya viongozi iliyopo na wanalindana sana kwenye wizi wao hivyo serikali haipati pesa zinazo stahiLi kupitia badari bora kuwapa wawekezaji tuu
Basi kama Watanzania ni wezi naunga na mtu moja hapo juu kasema Serekali ndio ibinafasishwe kwasabu kuanzia Raisi Mawaziri wafanyakazi wote Watanzania ambao umesema ni wezi.
 
Kama hadi Bandari inatushinda kuiendesha, basi hakuna kitu Watanzania tutaweza kukisimamia na kukiendesha kwa Ufanisi.

Hapo Bandari na mashirika mengine ya Umma kilichotakiwa ni kubadiri namna ya kuwapata Wakurugenzi Watendaji yaani CEOs, badala ya kuteuliwa kisiasa basi Wangechujwa kupitia Interviews pamoja na kuruhusu Mtu yeyote mwenye sifa kuomba hata kama atakuwa Sio raia wa Tanzania.

Upatikanaji wao uangalie zaidi Merits.

Hao maCEOs wapewe malengo na Serikali iache Utaalamu ufanye kazi badala ya kuingiza Siasa zao
 
Ifike wakati Serikali iachane na kufanya biashara make huu ni ujamaa na usha kuwa proved haiwezekani zaidi ya upigaji...
Hio Bandari ya Dar kama ingejengwa ya Baganoyo na ya Bagamoyo ikawa ni private na ya Dar ikawa ni ya Serikali bila shaka meli zingehamia Bagamoyo na ya Dar ingekuwa kama TTCL now.

Basi kama Watanzania ni wezi naunga na mtu moja hapo juu kasema Serekali ndio ibinafasishwe
Hata mimi kwa hili naunga mkono zaid ya 1000000% serikali inashindwa kuwasimamia watu iliyo waajir yenyewe
 
Hio Bandari ya Dar kama ingejengwa ya Baganoyo na ya Bagamoyo ikawa ni private na ya Dar ikawa ni ya Serikali bila shaka meli zingehamia Bagamoyo na ya Dar ingekuwa kama TTCL now.
H
Hata mimi kwa hili naunga mkono zaid ya 1000000% serikali inashindwa kuwasimamia watu iliyo waajir yenyewe
Sasa hapa Tatizo ni bandari au ni Serekali?

Kwanini unapendekeza bandari ibinafsishwe bada ya Serekali inayoshindwa kusima bandari ndio ibinafsishwe.
 
Akili za hovyo kabisa hizi, kwa hiyo furaha yako uwape wageni wakuendeshee mambo yako wewe uendelee na story za pwagu na pwaguzi kwenye kijiwe cha kahawa.

Kama mnataka kubinafsisha kwa nini msiwambie watanzania wenyewe waunde makampuni waiendesha, au ndo ule jenerali Ulimwengu aliuita ugenishaji.​
 
Back
Top Bottom