Erythrocyte
JF-Expert Member
- Nov 6, 2012
- 128,308
- 245,426
Baada ya Uchunguzi wangu wa kina nimeamua kwa dhati kabisa kuunga Mkono na Kupongeza Uamuzi wa Serikali ya Marekani kuondoa misaada yote kwa Nchi za kiafrika.
Hii ni kwa sababu misaada hiyo haikustahili kupewa Nchi hizo, kwa vile zinao uwezo wa kujihudumia zenyewe.
Kwa Mfano, Inawezekanaje kuipa msaada wa matundu ya vyoo Nchi ambayo Mawaziri wake wananunuliwa gari za LC300? unawezaje kusaidia Chanjo ya Polio Nchi ambayo Chama cha siasa kinanunua Mabasi zaidi ya 200 na Bodaboda zisizo na idadi kwa kisingizio cha kufanyia kampeni, Wakati inafahamika kwamba Wanaiba kura na Uchaguzi wote kwa Ujumla? Kwanza Wazungu walichelewa Mno kuchukua uamuzi huu Muruwa!
Inawezekanaje kusaidia Nchi ambazo Wake ama Waume wa viongozi Wanalipwa mishahara mizito hata kama hawafanyi chochote?
Kwa kufupisha, Siungi Mkono watu kufa kwa kukosa ARV za Bure, lakini ni Aibu kuchimbiwa vyoo vya shule na Masoko huku Viongozi wanaokufa wanafumwa wamelundika Malundo ya Hela kwenye vyumba vyao.
Uamuzi huu uwe Fundisho kwa Wananchi Masikini waliochagua kuwa Machawa ili watupiwe Makombo.
MUNGU WABARIKI WAZUNGU