Nauza bajaj niliyoichukua kwa mkopo, atakayeitaka atatakiwa kurudisha rejesho

Nauza bajaj niliyoichukua kwa mkopo, atakayeitaka atatakiwa kurudisha rejesho

Ukiwa na shida ya njaa Mkuu, kisha ukaoneshwa chakula kilipo, unakuwa kama kipofu. Yaani unaweza sema nipeni hiyo Bajaji hata kwa rejesho la laki kwa siku mie nitapambana kufa kupona nilete. Narudia tena, njaa si rafiki mwema...
Hakikaa mkuu...kuna siku nilikuwa sina kitu halafu na shida na helaaa nikaenda kwenye zile za kukopesha mtaani mwana anasema laki kila siku 4000 😀 😀 😀 😀 hapo nilikuwa sitegemei kupata hela soon nikaona huu ni mtego mkali snaa
 
sema mwishoni atabaki na bajaji....so sio mbaya sana ila uwe na uwakika wa abiria na ufanye trip barabara ya lami
Hata wa mkataba sio hivyo.

Huyu ni sawa kanunua bajaj 2

Watanzania wengi hawasomi makaratasi, wao wanapigiwa hesabu za wiki au mwezi wanaziona ndogo

Sent from my M2006C3LG using JamiiForums mobile app
 
Siyo kwa riba hiyo.

Hii ni sawa na wale jamaa BAYPORT.

Sema tu BAYPORT unapewa Pesa ila kwa hawa jamaa unapewa chombo. Ila model ya unyonyaji kwa watu maskini bila huruma ni ileile. Mungu atunusuru na huu unyonyaji kwa sababu ya umaskini wetu sisi wabongo!
Bayport nlitska nimalize den bank niende bayport sababu riba ni ndogo
 
Nakuomba ufanye re-view ya maamuzi yako usije jutia. Sipo hapa kuharibu biashara ya watu, ila ndugu yangu, mvuja jasho mwenzangu, nakuomba ufanye maamuzi yako kwa umakini mkubwa usije jutia hapo mbeleni..
😂😂😂😂Onyo Kali Sana hili..Riba bhana mbaya Sana,hao jamaa ukiambiwa wanatoka UK unaweza kuzimia,,
 
Kwa siku malengo ni tsh 20000 kwa 140000 wik ina mana haina siku ya dereva so inabid kama unachukua iwe yako yaan, dereva ndo awe mwenyenayo na bado baada ya miez sita ndo chuma uanza kuisha vitu hivyoo unatakiwa anagalau uwe una akaiba lau ya tair 3 ambay ni tsh 255000 hapo bado vit vingine kutoboa labda uwe na chuma nyingne ndo zitasaidiana hiv hiv mav ya mav mkataba unakuw mbwanda kala mbwanda. MUNGU tusaidie si wazeee wa NJE CUP.
 
Ni hatari sana; hizi hesabu ni ngumu
Rejesho kwa wiki 139,400 kwa muda miezi 24

Kimahesabu: 139,400 X 4 = 557,600/- kwa mwezi

557,600 x 12 = 6,691,200/- kwa mwaka

6,691,200 x 2 = 13,382,400/- kwa miaka miwili

Ili urudishe huu mkopo wa namna hii unahitaji ''discipline'' ya hali ya juu.
Hii mikataba ya kinyonyaji riba zaidi ya 58.33% kwa mwaka,
 
Nilikopa bajaj TVS KING TUKTUK mpya kwa kampuni flani ila nilitanguliza Tsh 1m kama dhamana, imetembea km 300 tu na ina bima ndogo, ina fire extinguisher, Latra na triangle zake ikiipata ni road tu.

Rejesho ni 139,400 kwa wiki nimesharejesha mwezi kama na kitu. Kwa anaehitaji hii bajaj na deni lake ili akimaliza deni iwe yake aje pm mi nahitaji laki 8 tu kati ya milioni niliyotanguliza,kisha namkabidhi.

Karibuni na picha hizi hapa;

Mbona bado miezi mingi sana ya kurejesha?
 
Back
Top Bottom