Nawaelewa sasa “Mvuto wa Rais kupungua“

Ukweli ni kuwa ujio wake haukupangwa vizuri. Ila yeye ukimtazama unaiona empathy na kilichotokea. Wapiga picha wake wakaishia kutafuta kapicha na mtoto ka ku trend siku hiyo but ile connection na wahanga nje ya hospitali haikuwepo. Mvuto unatokana na zaidi ya mtu, maandalizi ya matukio ni muhimu. Plus Rais amechoka,kusafiri na mengine tusiyoyajua kuna namna anaonekana mchovu. Apumzike wikiendi hii.
 
Ukiwa na gundu hata ujikombe vipi u- dc utausikua tu.
 
Serikali ikuwa kwenye mkutano wa hadhara na wala si msibani
 

Umeunena uhalisia na ukweli mtupu. Samia wa sasa ni wa kupigania madaraka yake binafsi, wapambe na familia yake, kuliko maslahi ya Taifa. Kwa sasa hana chembe ya uzalendo. Waovu na wahubi wamefanikiwa kumbadilisha na kumshika vilivyo.
 
Mkapa alisemwa pia hana Mvuto lakini haikumzuia kuwa Rais kwa awamu mbili

Mafanikio ya kisiasa sio kuwa na Mvuto tu kwny mikutano ya hadhara

Wakati wa Mkapa, Mvuto mkubwa ulikuwa kwa Mrema, wakati wa Abdul wakeel, Salmin, Karume na Shein Mvuto mkubwa ulikuwa kwa Maalim Seif

wakati wa Jakaya Mvuto mkubwa ulikuwa kwa Lowassa

Mvuto has nothing to do with Presidency

Sent from my SM-G9500 using JamiiForums mobile app
 
Umezungumza kama mpambe kuliko kuwa kama mchambuzi makini.

Mleta mada ameorodhosha mambo mengi ya msingi, la janga ni sehemu tu.

Mtu mzalendo wa kweli wa Taifa huliangalia zaidi Taifa kuliko madaraka yake. Samia wa sasa ni mbinafsi anayeuangalia zaidi Urais wake kuliko Taifa. Hata ule uchafu wa DPW ameangalia zaidi manufaa yake, familia yake na maswahiba wake, siyo Taifa. Maslahi ya Taifa yanatajwatajwa tu ili kuhalalisha maslahi msingi yaliyoegemea kwenye ubinafsi.

Mtu aliyeapa kulinda katiba, aliyeahidi kuhakikisha Taifa linapata katiba mpya, anathubutu kusema kuwa katiba haina maana, ni kajitabu tu. Bahati yake anaongoza jamii yenye wajinga na watu wengi wanafiki. Laiti ingekuwa ni mataifa yale ya watu makini, siku ile ingekuwa ndiyo mwisho wa Urais wake.
 
Poor argument.

Ratiba ya kwenda kuwapa pole wahanga inaisha lini? Mbona humlaumu Rais aliyeenda jana wakati yeye ana kila kitu kuanzia logistics za kufika mpaka resources? Mbona hakufika mara baada ya janga kutokea?. Wewe unataka uwapangie watu tarehe ya kufika wakati hao watu namna ya kufika na pole kwa waathirika, mpaka wachangishe.

Tatizo letu, wengi wa watu wetu uwezo wa akili ni mdogo sana, ndiyo maana unakuta kwenye huu mchango wako, reasoning ni minimum. Wewe lazima ni very low IQ. Uliyo nayo ni ile tu kukuwezesha kula, kuvaa na kutembea.
 
Huyu hakustahili hata kuwa makamu wa rais sasa ghafla amekuwa rais! Ghafla amejizungushia na machawa wanaomsifia kuwa haijawahi kutokea rais kama yeye, analewa madaraka kupindukia
 
Unasubirije uchaguzi wa 2015 ndio kiwe kipimo na unajua kabisa hatujawahi kuwa na uchaguzi huru na wa haki tangu 1995.
 
W
Wewe ndo low IQ, hujui hata janga lilipotokea Rais Samia alikuwa wapi!
CHADEMA ni Chama chenye sera nzuri lakini hakina viongozi wenye maarifa!
Viongozi wao hawana tofauti na wanamuziki wa bongo fleva au waigizaji wa bongo movie tu!
Wao ni kutafuta kiki tu na matukio wakidhani hiyo ndo itawabeba!
Hawana mipango, structures, strategies za maana!
Ni watu wanaodandia matukio tu na kufanya siasa za comedy tu!
Mtafuteni Zitto Zuberi Kabwe awapige msasa viongozi wenu namna ya kuendesha Chama!
CHADEMA imekuwa kama club ya pombe kila mtu ni msemaji!
 
Mimi binafsi hata nikisikia Mheshimiwa Rais Samia Suluhu yupo mtaani kwangu siwezi kupata hamasa ya kwenda kumsikiliza
 
Paskali,
Umekosea sana kulinganisha tukio la ndege vita ya mza, reaction ya mwal. Nyerere ktk tukio lile na hii ya Rais Samia huko Hanang. Mvuto wa kiongozi hautokani na kile unachokiita sanduku la kura hasa pale palipo na udanganyifu mkubwa ktk chaguzi.

Kwenye tukio la Hanang, Rais Samia anapaswa kujitathimini na kuchukuwa hatua. Kama kiongozi wa wananchi wote hakukuwa na sababu ya kuchukulia lile janga kichama au kisiasa. Kujaa kwa uniform za chama kuliko wahanga wa tukio lenyewe si massage nzuri ktk jamii. Pia kumsifiasifia kunakofanywa kinafiki na waandamizi wake kwenye matukio kama haya hakumjengei sifa nzuri.

Kwa siku za karibuni siasa za Samia zimekosa mvuto na ushawishi kwa wananchi hadi kwenye chama chake.. Ni swala la watu wa karibu yake kumwambia ukweli kuliko hii ya kumpaka mafuta kwa mgongo wa chupa.
 
Me naona badala ya samia, wanuweke Dotto Biteko kuwa mgombea,

Mwamwa naona hata teeth wanamuandaa kuwa presidaa ajae,

Anaongea kimamlaka na ana ile ego ya uongozi.
 
KIONGOZI MZALENDO HAWEZI KUTOKA CCM.

Sent from my TECNO BA2 using JamiiForums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…