Nawaelewa sasa “Mvuto wa Rais kupungua“

Hili neno!.
P
 
Kamundu wewe ni Chadema na walio karibu na wewe tunajua hilo. Ulitegemea useme nini zaidi ya kuwasema vizuri mabosi wako wa Chadema wanaokufanya wewe na familia yako kwenda chooni?
 
Unazidi kudhihirisha ulivyo low.

Kwa fikra zako, Rais kama leo yupo Dubai, akitaka kesho awepo Tanzania, atashindwa? Rais ambaye anaweza kuchukua ndege nzima akaenda yeye pekee yake au na watu anaowataka, unaamini akitaka hata kusafiri usiku huu atashindwa?

Rais ana resources zote za kwenda popote wakati wowote na watu wowote anaowataka, na kwa kutumia usafiri wowote. Hivyo vyote anavyo kwa sababu sisi Watanzania wote tunamhudumia. Huwezi kumlinganisha na mwingine yeyote ambaye kusafiri kwake kunategemea mambo mengi ikiwemo resources na logistics.
 
Rais alichagua kusafiri na wahuni kwenye safari yake ya kisiasa hayo ndo aliyoyatafuta
 
Kamundu wewe ni Chadema na walio karibu na wewe tunajua hilo. Ulitegemea useme nini zaidi ya kuwasema vizuri mabosi wako wa Chadema wanaokufanya wewe na familia yako kwenda chooni?
Tuambie namba yake ya kadi
 
Haya ndio mambo mama anawaandalia watanzania tuwe makini na huyu mzabzibari!
 

Attachments

  • 1702060694626.png
    158.3 KB · Views: 1
Mimi binafsi naandika haya kwa masikitiko makubwa sana na naona kabisa sasa viongozi wanavyo anza kulewa madara na kuwa watu tofauti na Mama Samia naye naona hajaweza kukwepa mtego huo
Wewe unafahamika siku zote ni mtu wa Mbowe, au niseme CHADEMA kwa hisia potofu za kudhani viongozi hao wapo karibu zaidi na nchi jirani unayoipigia upatu wewe kila mara kwa sababu iliyo wazi kwa wanaokufahamu.

Sipingi mawazo yako juu ya Samia. Samia ni mwigizaji mzuri, lakini hana uwezo wa uongozi. Sasa hivi ni dhahiri kabisa, sifa hiyo ya uigizaji ndiyo iliyomfikisha hadi hapo alipo sasa hivi. Lakini, kama ilivyo kawaida ya tabia za uigizaji na ulaghai, hazidumu. Sasa imebaki kutumia nguvu nyingi sana kuimba nyimbo za Samia kila mahali, na mapicha tele; lakini haya yote hayawezi kubadili picha la uigizaji na ulaghai wanaouona watu.
 
Magufuli alisababisha watu waanze kuvaa nguo za CCM hadharani kwa majigambo; kuna hatari nguo za CCM zikaanza kuzomewa tena kama ilivyokuwa wakati wa Kikwete.
Lakini wakati huo (wa Kikwete), CHADEMA ilikuwa imepamba moto kweli kweli; siyo kama hii iliyopoa kwa sababu zisizojulikana kabisa. Tena imepoa baada ya kutoka kwenye tanuru la moto alilokuwa kawaweka Magufuli! Sasa haieleweki kwa nini imekuwa hivi, ilivyo sasa chini ya Samia.

Kutakuwa kuna sababu maalum, na siku moja itajulikana tu.
 

Nchi gani jirani! Mimi naishi USA tangu 1997 mwezi wa nane! nikupe habari za bure. Pili Mimi sijawahi kuwa na Chama kwa wanao nifahamu na kujua hoja zangu. Mimi nipo Jamii forums toka 2006 kasome nimeandika mangapi ya Samia ya kumsifu. Ukiacha chuki zako binafsi ambazo ni vigumu kujua chanzo chake utagundua mimi sio mtu wa vyama au upande.

Huwezi kuendelea kwa kumchukia mwenzako. Be you
 
Huhitaji kujitetea. Kama ulivyosema, ni kweli JF huwa haifuti kitu, kwa hiyo mtu mwenye kutaka kujua historia ya mtu yeyote katika kuchangia humu JF, hata kama ni zama hizo za 2006, rekodi hiyo ipo, haiwezi kujificha.

Sina chuki na wewe, hilo ni wazo unalojiwekea hofu wewe mwenyewe.
 
Kwa hiyo Chadema mlikwenda Hanang ili kutafuta mvuto wa kisiasa nchini?

Tukisema Chadema mnapenda kick za matukio kupata Political Mileage mnasema tunakosea?

Chadema jipimeni kwa k8na maana kwa uhalisia ni kwamba mnahitaji uongozi mpya wenye kuweza kufanya mabadiliko makubwa na ubunifu wa sera na mbinu za ufanyaji siasa kuendana na wakati uliopo.

Viongozi waliopo kwa sasa pumzi yao nduo imefikia ukomo kisiasa!
Hawana mbinu mpya za kukabiliana na CCM wanaobadilishana vijiti kila baada ya miaka kumi(10).

Mbowe ameisgazunguka uwanja mpaka amepitiliza na sasa anakimbia peku kwenye lami.
Msaidieni......
 
Mkuu Kamundu,
Nakuunga mkono 100% humu JF kuna watu wana chuki binafsi za ajabu dhidi ya wenzao!. Enzi nafanya kipindi cha Kiti Moto, by then hicho kipindi kilikuwa favourite program kwa enzi hizo, one day niko kwenye msiba fulani wa Wahaya fulani rich and influential, mimi nimevaa sunglasses na Capello ni usiku sijulikani, nikamsikia jamaa mmoja anasema kati ya vipindi anavyovichukia ni kiti moto!, nikimuona yule mtangazaji wake P on the screen, nazima TV!.

Kuna mwingine akamuuliza kwanini uzime TV, si change tuu station utazame channel nyingine?. Jamaa akajibu akiniona tuu, anatibuka na ku loose interest to watch anything!. Jamaa simjui, wala hanijui!.

Kuna Mhaya mwingine kwenye group hilo akatoa kubwa kuliko!. Akauliza hicho kipindi kwenye dish kiko Channe number l ngapi?, akajibiwa kinaonyeshwa kwenye local TV ya DTV, akasema mimi kwangu ni dish, kama kitu hakionyeshwi kwenye dish, hawezi kuangalia!, akasema kwani Tanzania kuna TV yoyote ya kuangalia?, ni takataka tupu!. Mimi naangalia CNN, BBC, Aljazeera na DSTV ndio kuna vitu vya maana vya kuangalia!.

Kiukweli nilijitokea nje kimya kimya!.
Hivyo nimeisha zoea kuna watu wana chuki tuu na watu wengine for no apparent reasons, mimi nashukuru sana, hata nikikutana na watu hawa, nawatwangia tuu likes za kutosha!. Hata mtu akinitukana humu, anakula likes!.
P
 
Nimekupata Mkuu Pasko hapo wenye..mivuto ya ukweli tutaiona Oktoba 2025......
 
Wewe mwenyewe umepoteza mvuto baada ya kujigeuza Chawa.
Mimi sijawahi kuwa chawa!. Chawa kazi yake is to sing songs of praise and never criticize!. Mimi kwenye mazuri nasifu, kwenye mabaya nakosoa na kushauri!. Pongezi Zangu ni Bonafide-Genuine! Sisaki Teuzi, Sitaki Teuzi, Niko Naye Mbeya, Nitamweza!

Kwa wenye uwezo to read in between the lines, wananijua mimi ni mtu wa spana mkononi! Kumuenzi Magufuli: Tujikumbushe 'spana' za JF zilivyomsaidia Hayati Magufuli na Taifa. Je, Samia pia tumsaidie kwa 'spana' au tumkune tu tusimpare?
P
 
Nimekupata Mkuu Pasko hapo wenye..mivuto ya ukweli tutaiona Oktoba 2025......
Mkuu MENGELENI KWETU , the end justifies the means, the one who laughs last, laughs most!, kumaanisha atakaye cheka mwisho ndie aliyecheka zaidi, kama ilivyo kwa mlaji ni mlaleo, mlajana kala nini?.

Watu wanababaishwa na nyomi za makundi ya watu na kukubalika, kipimo cha kukubalika kwa ukweli ni 2025!, tena hata Hai, Chairman anaweza kurejea Bungeni kwa mlango wa nusu mkate tuu, vinginevyo hatoboi!.

Hili la nyomi nimelizungumza sana humu!, hakuna mtu aliyekuwa anakubalika kama Eddo ile 2015, na nyomi zake ni usipime!, Kwa Hali Niliyoishuhudia Leo Old Bagamoyo Rd: There is No Way CCM Inaweza Kushinda! kisha nikawaonyesha watu Elections 2015 - Hii 'Vox Populi' ni 'Vox Dei' Kuhusu 'Jiwe Walilolikataa Waashi'? lakini huwezi amini Kama kipimo cha ushindi ni idadi ya watu, Lowassa ndiye rais wetu
Hivyo haya mambo ya mvuto wa kweli tutaujua 2025!.
P
 
Unahisi hapo umechangia? Lissu ni Makamu Mwenyekiti wa Chadema. Unaweza kutwambia namba yake ya kadi? Pumbavu!!!
Lissu na Chadema wengine wanajulikana wazi kwa kujitambulisha.

Haya tupe utambulisho au conset ya mtoa hoja kuwa ni wa huko
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…